Je, ni vyuo gani vinaongoza kwa kutoa wasomi walioiva vizuri Tanzania?

Nimepata kuwa kwenye Gymnasium sköla tulikuwa tunaangalia ubora wa vyuo hasa vya Afrika, ni aibu

Kwa Tanzania UDSM baada ya maprofesa kuingiza siasa na kushindana kuandika mathesisi,
Kimeshuka sana, japo Kwa TZ hakina Mpinzani ,
Pili chuo wali ki dismantle kwa kukigawa gawa mara UCLAS MUHAS vikaondoka,

Ukija upande mwingine, IFM, DIT, SUA na Mzumbe wako vema sana, baada ya UDSM

Udom siasa na UCCM mwingi sana., hata miundombinu si ya kutosha kwa baadhi ya Faculties

Britannica Encyclopedia
Hivi kwani nini UCLAS ( Ardhi university) na MUHAS waliviondoa UDSM?

Maana baada ya kuondolewa UDsm ukitoa coet na coist na wale wa agriculture kozi nyingine za ovyo ovyo tu
 
Dar es salaam maritime institute, Africa viwili tu kingne magharibi njoo kwa mabaharia pale watu wachache wanajua nn wanafanya Unique africa achana na mbwembwe za udsm na aridhi
Hiyo institute ndo unalinganisha na university kama UDSM ARDHI UNIVERSITY au MUHAS?hebu kuwa serious
 
Ina maana MUHAS wanaokutibu,na Ardhi university wanakujengea nyumba hawana kitu?
Anyway labda Kwa kuwa yalikuwa matawi ya udsm Zamani

wote hao ni matawi ya udsm na bado wahadhiri wa udsm ndo wanaofundisha matawi hayo sasa mtu anakuja kulinganisha udsm na SEKOM kweli
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, karibuni tujadili bila upendeleo wala chuki yoyote. Mfano inajulikana wanafunzi wengi wanaosoma University of Dodoma ni wale ambao alama zao hazikutosha kusoma University of Dar es salaam n.k hivyo kujikuta wanaangukia kwenye kapu la Udom.

Vivo hivyo wanafunzi wengi wa SAUT ni wale ambao wamejikongoja kutoka shule za kata na wengine wale waliofaulu kwa kurudia mitihani( reseaters) na wale ambao wameunga unga kwa nguvu kuanzia certificate, diploma mpaka degrees.

Kuna wale wa vyuo kama Sebastian Kolowa, Meru University, St Joseph and the likes ambako wanaenda wale ambao lengo lao ni kusomeka ana degree bila kujali hiyo degree imetoka chuo gani.

NB: Karibu tuchangie kwa uhuru na bashasha
Wasomi walioiva vizuri wanapikwa kwa gesi maana yenyewe inawahisha. Ila ukitumia mkaa na vile vyungu vya asili, huwa wanakuwa na ladha nzuri
 
mtu ukikosa sifa ya kwenda UDSM unabadiliia na kuwa hater wa UDSM. UDSM ni chuo kinachochukua cream yote ya ufaulu yaani div one na two kali ndo wanadahiliwa UDSM sasa mtu unapokuja kulinganisha UDSM na OPEN mara na SEKOM au SAUT nakua na mashaka na elimu yako na uwezo wako wa kufikiri
Kabisa mkuu

Hebu angalia watu wanaodahiliwa pale ni dv 1 na two Kali sambaba na Ardhi university kuna mapgm na mapcm kibao pale

MUHAS sasa bila point sita udokta usahau

Sasa eti mtu analinganisha hivi vyuo na UDom au sauti vyenye watu WA point 17
 
Hakuna chuo TZ kinachotoa wasomi walioiva. Atakayetaja chuo anijibie haya maswali mawili.

1. Ukiowaondolea wasomi wetu kujua kusoma na kuandika unahisi watabaki na nini cha kujivunia kuwa walikipata huko vyuoni?

2. Ukiwaondolea ajira walizonazo muda huu je, wana mbinu mbadala za kuendesha maisha nje ya ajira ambazo mbinu hizo wamezipata huko chuoni?

NB. Elimu yetu inahitaji marekebisho MAKUBWA SANA ili imukomboe Mtanzania kutoka pale alipo kifikra, kijamii, kiuchumi, nk
Haya maswali Mkuu yanajibika hasa kwa wale waliosomea ICT katika vyuo vingi tu hapa Tz
 
Huo si ukweli.
Lile somo la Human resources management ni la nn.
Mm hapa nina diploma ya clinical medicine na nimejiajiri kwa korokoro kibao na now najisomesha degree ni upeo tu wa mtu msisingizie mfumo wa elimu
Tatizo unejibu kibinafsi sana bado hujajibu kijamii zaidi.

Jifanye una diploma ya ualimu/sheria/ugani unawezaje kuitumia nje mfumo rasmi wa ajira? Kumbuka wakati unajibu uwe ni mtoto wa kutoka familia masikini yaani wewe msomi na tajiri pekee kutoka kwenye familia yako.
 
Hakuna chuo TZ kinachotoa wasomi walioiva. Atakayetaja chuo anijibie haya maswali mawili.

1. Ukiowaondolea wasomi wetu kujua kusoma na kuandika unahisi watabaki na nini cha kujivunia kuwa walikipata huko vyuoni?

2. Ukiwaondolea ajira walizonazo muda huu je, wana mbinu mbadala za kuendesha maisha nje ya ajira ambazo mbinu hizo wamezipata huko chuoni?

NB. Elimu yetu inahitaji marekebisho MAKUBWA SANA ili imukomboe Mtanzania kutoka pale alipo kifikra, kijamii, kiuchumi, nk
Ahhaahh! Definitely n respect kwa kuliona hili mkuu...
 
Haya maswali Mkuu yanajibika hasa kwa wale waliosomea ICT katika vyuo vingi tu hapa Tz
Mkuu nahisi bado hujanipata pointi yangu ilipo. Ninachotaka kusema hapa ni kwamba tunasoma ili tuajiriwe BASI kijana anapokosa ajira kinachofuata ni kilio haijalishi amesomea wapi na fani ipi.

Tuamke leo hii hakuna ajira serikalini wala taasisi binafsi je, jamii yetu ina njia mbadala wa kujikwamua na kutatua changamoto kimaisha nje ajira?

Au ndio hivyo tumemezwa na wanaohimiza vijana wajiajiri wakati wao wakipewa huduma zote za kibinadamu kwa kodi zetu bure. Kwanini wanaohamasisha kujiajiri wasiache kazi zao na kujiari kama kweli kujiajiri ni dili?

Mkuu tunahitaji kujiuliza maswali magumu magumu na kukipata majawabu yake kama taifa/jamii basi tutatoka pale tulipo.

Huo ushabiki wa UDSM na UDOM mimi binafsi nauona ni utoto na ulimbukeni tu sababu hata waliopita huko waneshindwa kuisaidia jamii wamebaki kuvaa nusu uchi na kata k huku wakiijita eti ni WASOMI.
 
KARUME INSTITUTE OF SCIENCE AND TECHNOLOGY. Chuo kipo vizuri sana, kipo ZANZIBAR. Ukimpata mmoja wa aliyesoma chuo hiki utajionea.

Ni moja ya vyuo vichache duniani vyenye CCTV CAMERA katika chumba cha mtihani.
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, karibuni tujadili bila upendeleo wala chuki yoyote. Mfano inajulikana wanafunzi wengi wanaosoma University of Dodoma ni wale ambao alama zao hazikutosha kusoma University of Dar es salaam n.k hivyo kujikuta wanaangukia kwenye kapu la Udom.

Vivo hivyo wanafunzi wengi wa SAUT ni wale ambao wamejikongoja kutoka shule za kata na wengine wale waliofaulu kwa kurudia mitihani( reseaters) na wale ambao wameunga unga kwa nguvu kuanzia certificate, diploma mpaka degrees.

Kuna wale wa vyuo kama Sebastian Kolowa, Meru University, St Joseph and the likes ambako wanaenda wale ambao lengo lao ni kusomeka ana degree bila kujali hiyo degree imetoka chuo gani.

NB: Karibu tuchangie kwa uhuru na bashasha
 
mtu ukikosa sifa ya kwenda UDSM unabadiliia na kuwa hater wa UDSM. UDSM ni chuo kinachochukua cream yote ya ufaulu yaani div one na two kali ndo wanadahiliwa UDSM sasa mtu unapokuja kulinganisha UDSM na OPEN mara na SEKOM au SAUT nakua na mashaka na elimu yako na uwezo wako wa kufikiri
Kuchukua watu wenye sifa si kigezo cha uhalalisho wa hoja yako mfu,ukiishi kwa kukariri maisha ni shida sana,na kama umeoa au kuolewa namwonea huruma mkeo au mumeo kwa hasara hii ndani ya familia,hopeless kabisa wew ngamia
 
Mi nipo nasoma chuo cha KKKT nasomea ubunge mimi na mleta uzi.

Mleta uzi darasani ni hopeless kabisa, ana walakini ubongoni kama dhaifu wetu wa kijani
 
Back
Top Bottom