Je, ni vyuo gani vinaongoza kwa kutoa wasomi walioiva vizuri Tanzania?

marisi schwein

JF-Expert Member
Dec 3, 2013
1,009
3,024
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, karibuni tujadili bila upendeleo wala chuki yoyote. Mfano inajulikana wanafunzi wengi wanaosoma University of Dodoma ni wale ambao alama zao hazikutosha kusoma University of Dar es salaam n.k hivyo kujikuta wanaangukia kwenye kapu la Udom.

Vivo hivyo wanafunzi wengi wa SAUT ni wale ambao wamejikongoja kutoka shule za kata na wengine wale waliofaulu kwa kurudia mitihani( reseaters) na wale ambao wameunga unga kwa nguvu kuanzia certificate, diploma mpaka degrees.

Kuna wale wa vyuo kama Sebastian Kolowa, Meru University, St Joseph and the likes ambako wanaenda wale ambao lengo lao ni kusomeka ana degree bila kujali hiyo degree imetoka chuo gani.

NB: Karibu tuchangie kwa uhuru na bashasha
 
Hakuna chuo TZ kinachotoa wasomi walioiva. Atakayetaja chuo anijibie haya maswali mawili.

1. Ukiowaondolea wasomi wetu kujua kusoma na kuandika unahisi watabaki na nini cha kujivunia kuwa walikipata huko vyuoni?

2. Ukiwaondolea ajira walizonazo muda huu je, wana mbinu mbadala za kuendesha maisha nje ya ajira ambazo mbinu hizo wamezipata huko chuoni?

NB. Elimu yetu inahitaji marekebisho MAKUBWA SANA ili imukomboe Mtanzania kutoka pale alipo kifikra, kijamii, kiuchumi, nk
 
Uwezo Wa mwanafunzi na uwezo Wa chuo wakati mwingine ni vitu tofauti unaweza soma chuo chenye sifa kubwa lakini uwezo wako ukawa Mdogo kuliko aliyesomea chuo cha kawaida tumeshuhudia katika mazingira ya kawaida tu msomi anaishindwa kazi anakuja kuifanya mtu ambae elimu yake ni ya kawaida sana
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, karibuni tujadili bila upendeleo wala chuki yoyote. Mfano inajulikana wanafunzi wengi wanaosoma University of Dodoma ni wale ambao alama zao hazikutosha kusoma University of Dar es salaam n.k hivyo kujikuta wanaangukia kwenye kapu la Udom.

Vivo hivyo wanafunzi wengi wa SAUT ni wale ambao wamejikongoja kutoka shule za kata na wengine wale waliofaulu kwa kurudia mitihani( reseaters) na wale ambao wameunga unga kwa nguvu kuanzia certificate, diploma mpaka degrees.

Kuna wale wa vyuo kama Sebastian Kolowa, Meru University, St Joseph and the likes ambako wanaenda wale ambao lengo lao ni kusomeka ana degree bila kujali hiyo degree imetoka chuo gani.

NB: Karibu tuchangie kwa uhuru na bashasha
Kwa sasa Chuo kikuu kinachotoa wahitimu Bora ni Open University of Tanzania. Chuo hiki kinaenda na mabadiliko ya Technology,kina platform moja ya kujifunzia online inaitwa "Moodle" ambayo nadhani hakuna Chuo chochote hapa Nchini kinayo! Pili Wanafunzi wa OUT wanasoma kwa mfumo " Kuku wa Kienyeji", wanajitafutia materials na hawasomi handouts " madesa" kama Vyuo vikuu vingine!
Na hivyo kwa Wanafunzi wa OUT ambao wako serious wako deep sana!
Tatu,nafasi ya degree za " chu.pi " hakuna kwani Instructors na Wanafunzi kukutana ni mara chache sana !
 
Takataka. Tena kifutwe.
 
Back
Top Bottom