Je ni vizuri kuwaambia rafiki zako matatizo yako au siri zako

bakarikazinja

Senior Member
Nov 9, 2009
177
8
Wanajamii nimeamua kuwa letea jamvini nanyi muweze ni shauri kwani maranyingi nimekuwa na marafiki katika maisha tukisaidiana ktk mambo mbalimbali lakini ya kimaisha na mwingine unamuona kama ndugu yako au zaidi ya ndugu yako na kuanza kumshirikisha katika mambo mbalimbali ya kiwemo ya kifamilia lakini mwisho wa siku huwa anayatoa nje pale mnapo tofautina
hivyo wanajamii ni vizuri kuwambia rafiki zako matatizo yako au siri zako
 
inategemea siri/tatizo lenyewe limekaa vipi?mfano una mchumba/mme lakini kuna wakati mkaka flani anakuchanganya unaweza kumwambia yeyote kama si hapa JF tu ambapo hatufahamiani physically but just electronically?

When you tell the right person your problems unapata ahueni fulani ila soi kumwambia everyone who come across.
 
Marytina ameeleza vizuri. KWa mfano mimi nina marafiki wengi tu lakini kuna mmoja tu ambaye namwamini sana kwani ni rafiki wa siku nyingi, tumepitia mengi na tumesaidiana mengi tu. Namwamini naye ananiamini, hivyo huwa tunashare concern zetu. Unapobaki na tatizo bila kupata msaada wa mawazo linakuwa mzigo kwako na kupelekea msongo usioisha.
 
appreciate!!! ndio maana ukiwa na tatizo usilodhubutu kumweleza hata mchungaji/ padri wako lilete JF watakukejeli ila utapata ahueni flani.
 
Ukweli ni kwamba marafiki wanatofautiana lakini kama ni tatizo ambalo sulution ipo wazi jitahidi kutoa maamuzi mwenyewe. Hii itakusaidia kujenga confidence na kuepuka lawama endapo ushauri ambao ungeupata toka kwa rafiki yako usingekufaa. Pia unakuongezea usiri ambao hautahitaji gharama kubwa ya kumuheshimu rafiki yako kwa kuwa anakujua vyema. Kumuweka al least kila wazi kuna madhara ya mtu kukujua vyema mapungufu yako na hivyo kupelekea kukudharau endapo mtakorofishana.
Njia sahihi ni kujishauri mwenyewe kupitia kusoma vitabu au kuwa na mwelekeo wa ufanyaje katika shauri lako ila rafiki unayembambia ni kutaka kujiridhisha je uamuzi wako ni sahihi. Vile vile uelewe ushauri unaweza kuufanyia kazi au kuuacha. Kumbuka huwezi kushauriwa bila kuweka tatizo lako.
 
Kuna mtu mmoja aliwahi kwenda kupeleka malalamiko kwa mkwe wake kuwa mkewe siui ana nini mara oohhh kimepanda kikashuka ile kufika tu kwa mkwe wake nje ya nyumba loohh akakutana na matusi na maneneo makali yanatoka kwa mkwe wake wa kike anamtukana wa kike akaona duhh kumbe ni afadhali hata yale ya kwangu home akageuza kurudi home kimya.

so unaweza kuona mambo kama hayo wewe kufa na tai shingoni bana kama mwanaume
 
Mzee wa Rula ameeleza kwa ufasaha, ni vyema kujijengea utaratibu wa kutatua matatizo yako mwenyewe kuliko kushirikisha watu ambao siku mkitofautiana anatumia hicho kama kigezo cha kukushusha. Vile vile huwa naona ni bora kujadili na watu nisiofahamiana nao kutatua matatizo yangu kuliko kupitia marafiki....
 
Ogopa kumweleza kila rafiki, but ukiwa na rafiki yako mwaminifu na mwenye busara ni vyema ukajaribu kumshirikisha katika matatizo yako ili akushauri.
Kwani ukikaa nayo sana moyoni waweza pata shinikizo la mawazo, amabalo la weza kuletea matatizo badae.
 
Back
Top Bottom