Je ni vizuri kuonyesha waziwazi picha za watu waliokufa?

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,557
19,435
Imekuwa ni tabia ya Kawaida sana kwa magazeti ya Tanzania, hasa yale ya global Publishers kuonyesha waziwazi picha za watu waliokufa ama kwa ajali au kwa kupigwa risasi. Hiyo ni tabia ambayo nimeiona kwa muda mrefu sana sasa tangia zile za wakenya waliouwawa na polisi huko Arusha miaka kadhaa iliyopita. Je ni ustaarabu kweli kuonyesha picha za namna hiyo? Ninadhani kufanya hivyo kunasababisha watu wengine hasa vijana wale ambao akili zao hazijakomaa vya kutosha kushindwa kuona thamani ya uhai, na kuona kuwa kuuana ni jambo la kawaida.
 
Mi si mwandishi wa habari, lakini nadhani ethics za journalism haziruhusu kuonesha picha za kutisha au kuadhiri /kumkosea heshima na adabu muhanga wa ajali, majambazi, nk. Kwa kawaida kunatakiwa kuwepo aina fulani ya moderation au staha katika picha hizo. Lakini unakuta magazeti yetu yanaonesha waziwazi tena kwa karibu kila kitu: mf. majeruhi akiwa uchi, au kichwa kimekatika kiko pembeni, au mguu umeachana na mwili. Hii si namna nzuri na ya staha kwa wahanga na wanajamii. Mfano maiti au majeruhi wanaweza kupigwa picha baada ya kuvikwa au kufunikwa na nguo/kitambaa, nk. Hiyo haiondoi ukweli kwamba wahanga husika walipata ajali - na majeruhi au tayari ni marehemu. Staha ni ya lazima. Waandishi wetu lazima wajifunze kwa hilo.
 
Inasikitisha sana, kuna moja wameposti kwenye website yao, mtoto aliyeteketea kwa moto
 
Mkuu kitaaluma wanakiuka taratibu za kazi zao,lakini katika uhalisia wake wanasaidia kuwaelimisha wananchi hali halisi ya mauaji ya kutisha.Kuna siku nilikwenda pale Mwananyamala kuuga mwili wa ndugu yangu,tulkiwa katika harakati za kuuandaa mwili wa ndugu yetu ilikuja maiti fulani ikiwa imeharibika vibaya sana hivyo baba mzazi wa yule kijana na ndugu zake(baadhi)walikataa kwenda hata kuiona.Niambie kama upo peke yako utafanya nini?Mimi nadhani wapo baadhi yetu hatutatoa hata msaada kwa watu waliopata ajali hata kama bado wapo hai kwa kuogopa hali waliyo kuwa nayo.Kwa upande wangu waandishi wa habari kwa kufanya hivyo wamenifanya nichukulie kama ni kitu cha kawaida.Kwa sasa naweza kuogesha maiti,kumhudumia mtu aliye katika point of no return.watanzania wengi tunampenda mtu akiwa katika hali zuri ila akiwa ktk hali tofauti tunajitebga kwa kudai wapo watu fulani wa kuwahudumia watu hao.Hakuna watu wengine ila ni wewe na mimi tunahusika hivyo tuchukue hatua.Ukiona picha ya kutisha ujue inakukomaza,mbona picha za akina Anold na Rambo tunaangalia iweje hizo ambazo unatakiwa kutoa ushirikiano.ni hayo tu wakuu.
 
Inasikitisha serikali wako bize kupiga kelele magazeti yakionyesha wadada wakiwa nusu uchi lakini wanakaa kimya maiti wanaonyeshwa tena front page...
 
Back
Top Bottom