Je, ni Uzalendo mashabiki wa Yanga kwenda kuwapokea washindani wa Simba kutoka Nigeria pale JNIA?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,597
141,410
Kupitia runinga ya ITV wameonekana mashabiki wa Yanga wakiwapokea timu pinzani na Simba kutoka Nigeria katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.

Nauliza tu kwenu wanasiasa kitendo hiki kilichofanywa na mashabiki wa Yanga kina chembe ya uzalendo?

Maendeleo hayana vyama!
 
Kwani katika Nchi hii kuna uzalendo?

Kama walioapa kuilinda Katiba ya Jamhur wanaivunja hadharan bila hofu wala AIBU yoyote na twaendelea kuwaamini.

Wacha Wana Yanga wafanye wapendavyo viongoz wanafanya makubwa kuliko hayo na tumeufyata kimyaa
 
Kwani katika Nchi hii kuna uzalendo?
Kama walioapa kuilinda Katiba ya Jamhur wanaivunja hadharan bila hofu wala AIBU yoyote na twaendelea kuwaamini
Wacha Wana Yanga wafanye wapendavyo viongoz wanafanya makubwa kuliko hayo na tumeufyata kimyaa
Wewe ni Yanga!
 
Kwa sasa Nchi hii ina uzalendo wa bandia, ila katika hali halisi uzalendo ulikufa siku nyingi! Hata hawa kina Pole pole, Madilu ..... uzalendo wao ni kwa ajili ya tumbo! Acha Yanga wawapokee Plateau ....

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
 
Ni uzalendo tosha kabisa. Uzalendo ni pamoja na kujali wageni. Yanga oyeeeeeeee. Kesho tukutane kwa mkapa tuwasapoti wanaijeria ili washinde kwa kishindo.
 
Kupitia runinga ya ITV wameonekana mashabiki wa Yanga wakiwapokea timu pinzani na Simba kutoka Nigeria katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.
Lakini cha ajabu Plateau wenyewe waliwapuuza hao mashabiki wa Yanga. Nadhani Plateau hawakuwa wazalendo kwa hilo
 
Kupitia runinga ya ITV wameonekana mashabiki wa Yanga wakiwapokea timu pinzani na Simba kutoka Nigeria katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.

Nauliza tu kwenu wanasiasa kitendo hiki kilichofanywa na mashabiki wa Yanga kina chembe ya uzalendo?

Maendeleo hayana vyama!
Huo ni uzalendo... Wao wameenda kama watanzania, si kama wana'yanga
 
Yanga wameonesha ukarimu tulionao watanzania hasa kwa kuwapokea wageni na kuwakirimu , kwa hiyo mlitaka wasikaribishwe kwa kuwa eti ni wapinzani wa Simba kwani Simba ni Yanga ? Acheni mambo yenu ya kizamani Simba chezeni mpira au ndo mmewaogopa mnataka kusingizia mashabiki wa Yanga kwa kuwapokea?
 
Simba 5 Plateau 0
 
Haya mambo haya?
Unawauliza wanasiasa lakini hata kwenye siasa ikitokea mpinzani yeyote anatoka nje ya nchi kwa hali ilivyo atapata watanzania wengi wanaoweza kumpokea kwa mbwembwe
 
Vitu vya kawaida hivi kwenye mpira hata ulaya mashabiki wa timu pinzani wanashabikiaga timu za wageni
Kupitia runinga ya ITV wameonekana mashabiki wa Yanga wakiwapokea timu pinzani na Simba kutoka Nigeria katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.

Nauliza tu kwenu wanasiasa kitendo hiki kilichofanywa na mashabiki wa Yanga kina chembe ya uzalendo?

Maendeleo hayana vyama!
 
Kupitia runinga ya ITV wameonekana mashabiki wa Yanga wakiwapokea timu pinzani na Simba kutoka Nigeria katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.

Nauliza tu kwenu wanasiasa kitendo hiki kilichofanywa na mashabiki wa Yanga kina chembe ya uzalendo?

Maendeleo hayana vyama!
Mimi sio mwanasiasa jibu langu ni moja tu kwamba wote walikwenda kuwapokea ni washamba
 
Lakini cha ajabu Plateau wenyewe waliwapuuza hao mashabiki wa Yanga. Nadhani Plateau hawakuwa wazalendo kwa hilo
Hapana mkuu hizi timu zetu za Africa labda kwingine sijui Ila zetu tuna zile Imani za ushirikina hasa hiyo timu ilipotoka, sasa watu wake wakupokee huna taarifa nao wala hawakuhusu hata kama wewe utamfurahia na kwake upo vitani? Hiki ndicho ambacho mashabiki wa Yanga hawakukiwaza kabisa, huruma
 
Nchi hii ina uzalendo? Tangu lini?
Kupitia runinga ya ITV wameonekana mashabiki wa Yanga wakiwapokea timu pinzani na Simba kutoka Nigeria katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.

Nauliza tu kwenu wanasiasa kitendo hiki kilichofanywa na mashabiki wa Yanga kina chembe ya uzalendo?

Maendeleo hayana vyama!
 
Uzalendo ni simba kupokea pyramid basi maana chochote kikifanywa na simba ni halali ni sawa ila kikifanywa na wapinzani wao si sawa.
 
Back
Top Bottom