Je ni utatanishi upi uliojitokeza kwenye Katiba ya sasa?

Emmanuel Kasomi

Verified Member
Sep 3, 2014
4,776
2,000
Katiba ndio muongozo na uhai wa taifa lolote duniani. Inapotokea Katiba haisemi au kuzungumzia jambo kinagauba au kuonesha upungufu wa aina yoyote ni ishara kuwa ni utatanishi hivyo kuhitajika marekebisho ikizingatiwa Tanzania huongozwa na binadamu ambao wanaweza kupatwa na matatizo yoyote.

Duru za kisheria zinabainisha kuwa maeneo yafuatayo yanaleta utatanishi kwa kuzingatia mchakato wa kukabidhiwa madaraka wa Rais Samia:

Mosi, Rais hakumteua waziri mkuu ndani ya siku 14 kama Katiba inavyoeleza Ibara ya 57(2) mara baada ya kuapishwa kulingana na agizo la muundo wa Baraza la Mawaziri na Serikali.
Pili,kwa mujibu wa Ibara ya 54 wajumbe wa Baraza la Mawaziri ni Makamu wa rais,Waziri Mkuu,Rais wa Zanzibar na mawaziri wote. Hata hivyo Rais Samia alikaa kikao na baraza la mawaziri pasipo kuwepo Makamu wa Rais kama takwa la katiba lilivyo.
Tatu, Katiba ya sasa inasema Rais atashauriana na waziri mkuu kuunda Baraza la Mawaziri, lakini waliopo sasa kwa asilimia kubwa 'wamerithiwa' kutoka kwa hayati Magufuli.
Nne, Katiba ya sasa haisemi lolote kuhusu muda ambao anatakiwa aunde baraza la mawaziri baada ya kuingia madarakani hata baada ya uchaguzi mkuu.
Tano, Katiba ya sasa inasema rais mteule anapoingia mdarakani na uteuzi wa Mwanasheria mkuu wa serikali unakoma Ibara 59(5b), ikiwa na maana anatakiwa kuapishwa tena kama rais mpya atataka kuendelea naye.
Sita, baadhi ya mawaziri wa Rais Samia walikula kiapo chini ya utawala wa hayati John Magufuli si Rais Samia.
Saba, Katiba haielezi Rais mteule atachukua muda gani kuunda Baraza la Mawaziri. Ikumbukwe hayati Magufuli alitumia takribani siku 30 kuunda Baraza la Mawaziri baada ya uchaguzi wa mwaka 2020 ambapo aliawaapisha Mwanasheria mkuu,Waziri wa mambo ya nje na Waziri wa Fedha na Mipango pekee. Pia mwaka 2015 ilimchukua siku nyingi hadi kutangaza baraza la mawaziri, kwa vile hakubanwa na muda ambao kimsingi ilibidi utajwe kwenye katiba.
Nane, Rais amepewa mamlaka ya kuvunja Baraza la Mawaziri, lakini hajavunja.
Tisa, Ibara ya 37(5) ya Katiba ya sasa haisemi ni muda gani wa Makamu wa Rais ataapishwa kushika wadhifa wa Rais mara baada ya kutokea kifo mfano cha hayati Magufuli.
 
SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
28,502
2,000
Mimi najionea raha tupu maccm mnavyotifuana. Ashukuriwe Mungu muumba wa mbingu na nchi kwa kutuondolea dhalim.
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
14,533

... vifungu vyote ulivyo-quote vinamhusu Rais Mteule; case ya Samia ni tofauti na, bahati mbaya, Katiba haisemi chochote kuhusiana na case hiyo! Case ya Mh. Samia inaangukia kwenye kundi la Rais Mrithi na sio Rais Mteule. Of course, nakubaliana na wewe ni high time Katiba izungumzie kinagaubaga Rais Mrithi anapaswa kufanya nini immediately kabla na baada ya kuapishwa!
 
Emmanuel Kasomi

Verified Member
Sep 3, 2014
4,776
2,000
... vifungu vyote ulivyo-quote vinamhusu Rais Mteule; case ya Samia ni tofauti na, bahati mbaya, Katiba haisemi chochote kuhusiana na case hiyo! Case ya Mh. Samia inaangukia kwenye kundi la Rais Mrithi na sio Rais Mteule. Of course, nakubaliana na wewe ni high time Katiba izungumzie kinagaubaga Rais Mrithi anapaswa kufanya nini immediately kabla na baada ya kuapishwa!
🙏🙏🙏 Shukurani mkuu kwa nyongeza hiyo
 
Kinyayo

Member
Aug 17, 2016
76
125
Wisely fact,ni kwamba katiba yetu iseme akifa Rais, uchaguzi urudiwe kama ambavyo hufanyika kwa wabunge,short and cleare.
.
.
.
Inakuwaje kwa wabunge tunatangaziwa jimbo lipo wazi lakini kwa Rais ni kinyume.
.
.
.
Tume ile....ile.

Why?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom