Magu
Senior Member
- Jun 13, 2011
- 156
- 56
Maadili ya kiafrika yanatuelekeza kutochangia chumba na watoto wetu wakati wa kulala hususani usiku ambapo mambo mengi na maongezi ya kifamilia kati ya baba na mama hufanyika.
Maongezi ya baba na mama ni mengi kuanzia maisha ya watoto na pia mijadala mingi ya maisha yanayoendelea mtaani, ambapo wanandoa hupashana habari na wakati mwingine kupeana umbea wa hapa na pale, lakini pia chumbani kwa wazazi ndo kiwanda cha kutafutia watoto wengine ili kutimiza andiko la kuijaza dunia kama tulivyoagizwa.
Sasa naomba kujua umri sahihi au ni wakati gani muafaka wa kumpa mtoto uhamisho wa kutoka chumbani kwa wazazi awape nafasi ya kufanya yote hayo niliyosema hapo juu, pia kutokubeba wanayofanya wazazi na kupeleka mtaani kwa watu wasiohusika na kuwaaibisha wazazi.
======
Baadhi ya Wachangiaji wamesema hivi;
Maongezi ya baba na mama ni mengi kuanzia maisha ya watoto na pia mijadala mingi ya maisha yanayoendelea mtaani, ambapo wanandoa hupashana habari na wakati mwingine kupeana umbea wa hapa na pale, lakini pia chumbani kwa wazazi ndo kiwanda cha kutafutia watoto wengine ili kutimiza andiko la kuijaza dunia kama tulivyoagizwa.
Sasa naomba kujua umri sahihi au ni wakati gani muafaka wa kumpa mtoto uhamisho wa kutoka chumbani kwa wazazi awape nafasi ya kufanya yote hayo niliyosema hapo juu, pia kutokubeba wanayofanya wazazi na kupeleka mtaani kwa watu wasiohusika na kuwaaibisha wazazi.
======
Baadhi ya Wachangiaji wamesema hivi;
jamani twendeni mbele turudi nyuma, watoto wa siku hizi wako na akili sana since day one anapozaliwa. zamani mtoto alikuwa akizaliwa hata macho hafungui mpaka baada ya siku saba lakin leo kana toka tumboni na macho kamefumbua kesho yake ukikaekea kalam au rangi rangi kanaanza kufuata kwa macho akiashiria kuwa macho yanaona.
ni busara sana mama na baba kulala na mtoto mchanga chumbani mwao. to me ningeshauri muwe na vitanda viwili chumbani ili mtoto alale na mama au baba hadi aishie usingizini kisha ndio nyie mkalale wenyewe kwenye kitanda chenu. hali hii iendelee hado mtoto afikishe miaka 3. hapa mtatakiwa kumuamisha chumba na kuampeleka kulala chumba chake ambapo pia mama na baba usiku mtalazimika kwenda kumuangalia amelalaje.
mtoto anapotengwa chumba kwa siku za kwanza msifanye ni routine ya kila siku ila mwelezeni kabisa mnamjengea utashi wa kuwa independent. siku moja moja mwaweza kumchukua mkalala naye au wakati ni mgonjwa but siku nyingine mnayotaka privacy basi mtoeni mkamlaze chumbani kwake.
kitanda cha huyu mtoto chumbani kwenu kiwepo kwani ni makosa sana kulala na mtoto mdogo kitanda kimoja ingawa sisi waafrika tumezoea. hata kama kazaliwa leo, basi alale na mama tu na akisha sinzia kabisa afunikwe aachwe peke yake. hali hii kisaikolojia humjengea mtt ujasiri, na pia humfanya asiwe tegemezi. vile vile humpunguzia risk za magonjwa jamani.manake mmetoka kufanya tendo la ndoa mara ukajikuta umemgusa mtoto binafsi sioni kama imekaa vizuri hii kwangu.
Mkuu
Katika kosa kubwa ambalo huwa linafanywa na wazazi kwenye malezi ya watoto wao ni katika step hii, wewe umezungumzia kulala, lakini mimi naomba nizungumzie swala la ni wakati gani muafaka kukaa uchi mbele ya mtoto wako.
Mtoto hadi anafikisha umri wa miaka mitatu nadhani ni poa tu kama unaweza kukaa nae akiwa uchi, hapa nakidiria kwamba huo ni umri ambao mtoto akiona maumbile ya mama anaweza akayatofautisha na ya baba. Ni vyema kuwa huru na mtoto, ili aweze kujitambua, lakini mambo ya kujificha ficha yanamsababishia viulizo kichwani, mtoto anaingia ndani ghafla wewe unakimbilia kuficha nyeti, unasababisha mtoto kujiuliza kuna nini pale na kuwa mwanzo wa kumchanganya.
Kumbuka ni hatari sana kwa mtoto wako kujifunza kitu chochote kutoka kwa watu baki badala ya wewe mzazi, wengi uabuse opportunity za kutrain. Kama kwa lulu & co,
Well said mkuu, mtoto ukitaka upende malezi yake akiwa na kama miezi sita hivi (anakula chakula chochote na keshajua usiku ni kulala tu) unafanya kumzoesha kulala vyumba tofauti tofauti na watu tofauti ili kuzea hiyo hali. Kikubwa uwe makini na usalama wa mtoto, awe na kitanda kinachohama kwa usalama zaidi ili alale kitanda chake chumba chochote.
Tatizo Waafrika wengi huwa tuna desturi kuwa ukifanya maandalizi ya ujauzito na maandalizi ya mtoto anayekuja wanachukulia kuwa ni uchuro!! Ukinunua vitu vya maandalizi wanaishia "kukuuliza akifa je?" na hali hii inafanya tusiwe na tabia ya kufanya planning ya ujauzito wa mtoto/watoto wanaotarajiwa kutafutwa na kuzaliwa!! Hatimae utakuta hali inafika kuwa mbaya kwa familia, watoto watatu hadi wanne tena wa jinsia tofauti wanashea chumba kimoja na wazazi.
Lakini mambo huwa ni rahisi pale mnapoanza kuishi pamoja mkajadili kwanza kabla ya kubeba mimba juu ya huduma za huo ujauzito na hata mtoto ajae kuwa atakula nini, atalala wapi, atavaa nini na atacheza mazingira yepi!!