Je ni umri gani wa mtoto anatakiwa kutolewa chumbani kwa baba na mama wakati w kulala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni umri gani wa mtoto anatakiwa kutolewa chumbani kwa baba na mama wakati w kulala

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Magu, Jun 22, 2012.

 1. Magu

  Magu Senior Member

  #1
  Jun 22, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Maadili ya kiafrika yanatuelekeza kutochangia chumba na watoto wetu wakati wa kulala hususani usiku ambapo mambo mengi na maongezi ya kifamilia kati ya baba na mama hufanyika.

  Maongezi ya baba na mama ni mengi kuanzia maisha ya watoto na pia mijadala mingi ya maisha yanayoendelea mtaani, ambapo wanandoa hupashana habari na wakati mwingine kupeana umbea wa hapa na pale, lakini pia chumbani kwa wazazi ndo kiwanda cha kutafutia watoto wengine ili kutimiza andiko la kuijaza dunia kama tulivyoagizwa.

  Sasa naomba kujua umri sahihi au ni wakati gani muafaka wa kumpa mtoto uhamisho wa kutoka chumbani kwa wazazi awape nafasi ya kufanya yote hayo niliyosema hapo juu, pia kutokubeba wanayofanya wazazi na kupeleka mtaani kwa watu wasiohusika na kuwaaibisha wazazi.
   
 2. Magu

  Magu Senior Member

  #2
  Jun 22, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sijui kama imeeleweka ndg zangu
   
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Jun 22, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Miezi sita tu inatosha........................LOL
   
 4. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  wazungu hua hawalali na watoto hata wakiwa wadogo maana si unajua wale ngono ni daily so watoto wanakua wanawawekea kauzibe
   
 5. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #5
  Jun 22, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Inategemea na nyumba unayoishi....kama ni chumba kimoja utamuhamishia wapi mkuu???
   
 6. stephot

  stephot JF-Expert Member

  #6
  Jun 22, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 5,024
  Likes Received: 2,646
  Trophy Points: 280
  Tokea siku alyozaliwa muangalie matakoni tu,ukishaona yanaanza kuwa meusi mhamishe chumba.
   
 7. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #7
  Jun 22, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,341
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Muda muafaka hapa sio umri bali check yafuatayo;
  1.kakianza kukodoa macho na kuona aibu wakati mmekula pozi la kingono na mamsup kafanyie transfer
  2.Kakianza kutoa comments kwenye topic za kikubwa hata kama hakawezi kuongea vizuri kape transfer
  3.Ukiona hakapati usingizi pale mech imeanza kape transfer
  4.kachunguze kenyewe kama kanatambua mambo mnayofanya na mkeo kanayaelewa kwa upana upi kama kanaonesha uelewa kape transfer
  CONCLUSION
  Nimeshindwa kutaja umri ili nipate swali zima kutokana na ukweli ni kwamba watoto wa siku hizi hawaeleweki hawafwati growth phase tulizozizoea.e.g mtoto ana miezi minne eti analilia ugali anaokula mama yake na hadi umpe ndo ananyamaza.
  Pia desturi wanayoitumia wazungu kuwatenga watoto wao chumba tangu uchanga unaepusha kuaribika kwa maadili kwa mtoto na pia inasaidia kumjengea hali ya kujiamini mtoto tangia utotoni ndiyo maana hawa jamaa sio waoga kabisa recall "building of church in Evil forest in things fall apart by Chinua achebe"
   
 8. s

  sawabho JF-Expert Member

  #8
  Jun 22, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Kwa umri huo hata raha sitakuwa nayo chumbani, maana nitakuwa naenda kumchungulia kila baada ya saa moja, hasa akiwa kifungua mimba. Lakini ni vizuri mlale naye chumba kimoja hata afikie umri wa kuongea ili mtakapomhamishia kwa Mdada wa kazi kubaini kama akifanyiwa mabaya. Vinginevyo, huko kwa Mdada wa kazi ndiko anawezjifunza makubwa kuliko ambayo angejifunza kwenu wazazi.
   
 9. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #9
  Jun 22, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,341
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Nilijua tu kuwa hii sread itapokea majibu ya ajabu si mnaona huyu ameshaanzisha.
   
 10. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #10
  Jun 22, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kiafya mtoto haruhusiwi kulala na wazazi
   
 11. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #11
  Jun 22, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,966
  Likes Received: 1,858
  Trophy Points: 280
  jamani twendeni mbele turudi nyuma, watoto wa siku hizi wako na akili sana since day one anapozaliwa. zamani mtoto alikuwa akizaliwa hata macho hafungui mpaka baada ya siku saba lakin leo kana toka tumboni na macho kamefumbua kesho yake ukikaekea kalam au rangi rangi kanaanza kufuata kwa macho akiashiria kuwa macho yanaona.

  ni busara sana mama na baba kulala na mtoto mchanga chumbani mwao. to me ningeshauri muwe na vitanda viwili chumbani ili mtoto alale na mama au baba hadi aishie usingizini kisha ndio nyie mkalale wenyewe kwenye kitanda chenu. hali hii iendelee hado mtoto afikishe miaka 3. hapa mtatakiwa kumuamisha chumba na kuampeleka kulala chumba chake ambapo pia mama na baba usiku mtalazimika kwenda kumuangalia amelalaje.

  mtoto anapotengwa chumba kwa siku za kwanza msifanye ni routine ya kila siku ila mwelezeni kabisa mnamjengea utashi wa kuwa independent. siku moja moja mwaweza kumchukua mkalala naye au wakati ni mgonjwa but siku nyingine mnayotaka privacy basi mtoeni mkamlaze chumbani kwake.

  kitanda cha huyu mtoto chumbani kwenu kiwepo kwani ni makosa sana kulala na mtoto mdogo kitanda kimoja ingawa sisi waafrika tumezoea. hata kama kazaliwa leo, basi alale na mama tu na akisha sinzia kabisa afunikwe aachwe peke yake. hali hii kisaikolojia humjengea mtt ujasiri, na pia humfanya asiwe tegemezi. vile vile humpunguzia risk za magonjwa jamani.manake mmetoka kufanya tendo la ndoa mara ukajikuta umemgusa mtoto binafsi sioni kama imekaa vizuri hii kwangu.
   
 12. UKI

  UKI JF-Expert Member

  #12
  Jun 22, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 699
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mkuu chumba kimoja??? mlikuwa serious kuanzisha familia kweli kwa maandalizi ya chumba kimoja??
   
 13. UKI

  UKI JF-Expert Member

  #13
  Jun 22, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 699
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  jamani mambo gani haya sasa?? ndio ushauri huo kweli? huyu mtu yupo serious sasa hayo meusi ni manini?? dah!!!!
   
 14. regam

  regam JF-Expert Member

  #14
  Jun 22, 2012
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 268
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mie yalinitokea ya ajabu. Baada tu ya kumaliza tunda an mamsapu wangu mwanangu akaanza kumpa pole mama yake. Yeye alidhani tulikuwa tunapigana. Mie tangu siku hiyo nikakapa transfer. Kalikuwa nod kanaanza kuongea tuu
   
 15. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #15
  Jun 22, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Mkuu
  Katika kosa kubwa ambalo huwa linafanywa na wazazi kwenye malezi ya watoto wao ni katika step hii, wewe umezungumzia kulala, lakini mimi naomba nizungumzie swala la ni wakati gani muafaka kukaa uchi mbele ya mtoto wako.

  Mtoto hadi anafikisha umri wa miaka mitatu nadhani ni poa tu kama unaweza kukaa nae akiwa uchi, hapa nakidiria kwamba huo ni umri ambao mtoto akiona maumbile ya mama anaweza akayatofautisha na ya baba. Ni vyema kuwa huru na mtoto, ili aweze kujitambua, lakini mambo ya kujificha ficha yanamsababishia viulizo kichwani, mtoto anaingia ndani ghafla wewe unakimbilia kuficha nyeti, unasababisha mtoto kujiuliza kuna nini pale na kuwa mwanzo wa kumchanganya.

  Kumbuka ni hatari sana kwa mtoto wako kujifunza kitu chochote kutoka kwa watu baki badala ya wewe mzazi, wengi uabuse opportunity za kutrain. Kama kwa lulu & co,
   
 16. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #16
  Jun 22, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,279
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Mara nyingi watoto wa kwanza wanachelewa kuamishwa chumba sababu wazazi hawana experience. Mwanangu wa kwanza na wa pili ilibidi wahame siku moja; baada ya kuona chumba kimekuwa kidogo. Ila nilijifunza kuwa inawezekana mtoto wa mwaka mmoja na nusu kuamishwa chumbani kwa wazazi, kwani mwanangu wa pili alihama akiwa na mwaka mmoja na nusu. Na uzuri wake mdogo analala mpaka kunakucha alikuwa ahamki kuomba chakula na analala na pampus. Mkubwa shughuli tulikuwa nayo ya kumwamsha kwenda ku pee. Mbona tumeweka zamu na mume wangu maana tuliona siyo fair kumwambia house girl awe anampeleka mtoto ku pee wakati ameshinda anafanya kazi siku nzima.

  Kama nyumba ni kubwa na mimi nashauri watoto wasilale na house girl; sijuhi kwa nini lakini mimi roho yangu hainipi mwanangu kulala na mtu baki.

  Asikwambie mtu kutokulala na watoto kuna raha yake; mnarudi kwenye ujana.
   
 17. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #17
  Jun 22, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,279
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Mbona mi nasikia wako tofauti na ulichosema hapo kwenye bold? Nikimaanisha hawana hizo nguvu za sex daily. Lol.

  Yes hawalali na watoto kwa sababu nyingi pamoja na usalama hasa kama mtoto analala kitanda kimoja na mzazi, anaweza kulaliwa. Wana sheria nyingi za kumlinda mtoto, ila sidhani kama wanajali kama watoto wao wanawaona wanapo do. Wangekuwa wanajali basi watoto wao wasingejua mambo ya sex wakiwa wadogo.


   
 18. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #18
  Jun 22, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  my first born nilimuhamisha akiwa na miezi 3, imediateky nilipoanza kazi tu, akahamia kwa dada, nilikuwa naamka usiku kunyonyesha tu! nategesha alarm, so kila baada ya muda fulani nakwenda kunyonyesha, na nilipopata twins, nilihama nao mimi, ili daddy apate kupumzika bila manepi ya watoto, pampers au vilio visivyokwisha! so he was ol alone, akirudi job nakwenda kwake kuongea habari za famili, wakati watoto wapo na hausgalz, akitaka kulala narudi kwa twins. na akihitaji maongezi ya usiku ananipigia naruka fasta, tunaongea then narudi kwangu, so ilipofika miezi mi3 ya mimi kurudi job, twins walikuwa wameshazoea kulala kuleeee kwa dada, na mpaka kesho hawajui kama kuna kulala na dad na mum!
   
 19. R

  Rubesha Kipesha Member

  #19
  Jun 22, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimeipenda thread hii, manake itasaidia wengi, wazazi wakati mwingine huchukulia kuwa watoto
  hawaelewi mambo yanayofanywa na wazazi. Imeshatokea watoto kusimuliana mambo yanayotendwa
  na wazazi wao usiku! Kimaadili ina impact kubwa tu kwani mtoto aweza kujaribu baadae mambo aliyoyaona.
  Kuanzia mwaka 1 na nusu mtoto asilale na wazazi. Awe na kitanda chake kidogo katika chumba kingine , ili alale mwenye na siyo kulala na dada au mtu mwingine yeyote.
   
 20. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #20
  Jun 22, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  pamoja na maelezo mazuri ya wachangiaji, uwezo wa familia kumudu accomodation yenye nafasi ya kutosha pia ina-matter
   
Loading...