Nahisi napenda nisipopendeka. Je, ni uamuzi sahihi nilioufanya?

habari zenu wadau! Nimefanya maamuzi magumu ambayo nilidhani yatanisaidia, lakini yanaishia kuniumiza. Ni kuhusu binti ambaye nimemfatilia kwa muda mrefu, nilijitahidi kwa kila hali kumuonesha kwa vitendo kwamba nampenda. Nilijitahidi kuwa karibu naye hasa kwa upande wa mawasiliano ya simu, muitikio wake ulikuwa mzuri japo alisema mapenzi na mimi no. Niliukubali urafiki japo kwa shingo upande, niliendelea kuwasiliana naye, lakin ilikuwa mpaka mimi nimtafute, nikikaa kimya naye anapotea, nikirudi anarudi. Kama mnavyojua kuwa kamba ikivutwa sana hukatika pabovu, ilifika muda nikachoka na nikaamua kukaa kimya. Sasa ni wiki ya 3 toka nimchunie, naye yuko kimya. Wadau hali hii inanitatiza, nataka nimpotezee mazima lakini naona naelekea kushindwa, moyo unaniuma kumuacha aende. Naomba ushauri wenu.

kumbe ushaumia tayari mi natoa msaada kwa aliekaribia kuumia kama ushaumia huku atukusaidii kitu mpwa endelea kuumia tu
 
mh viburudisho tena?
dawa ya hang over ni kushitua moja baridi tena....so tafuta super sub moja then jiweke sawa. Huyo kashasepa na hakupendi achana nae. Au kama vipi tafiti kama anamtu....atakuwa kajishika sehemu
 
mmh kwa kweli love haifundishwi,.,, pima mwenyewe uone ucje baadae ukajutia ushauri uliofuata, true love never end., kama moyo unauma try to re check,.. alikwambia anakupenda? ukute ni rafik 2 alaf unadhan ni mpenzi,.. mana weng 2napenda kuassume kwenye NO kuwe YES.
 
kaka toka nduki mkuu hapo hamna mahusiano anapasua kichwa hivyo je ukimmiliki aisee utajuta asubuh atakupenda jion atakuzngua c anajua huna hali kwake....me nakushauri mpotezee afu inaonekana ni kabinti kadogo umekapita ka miaka mitano na zaid...we poteza usinunue presha kwa bei rahisi mkuuu......kaushaaaaaaaaaaaaa
 
mkuu umejuaje? Ni kweli nimekazidi miaka 5, mpaka leo kakaa kimya. Hakika hakunipenda na wala hakukaa kufikiria kuwa na mimi hata siku moja, najutia muda nilioupoteza kwake.
 
mkuu umejuaje? Ni kweli nimekazidi miaka 5, mpaka leo kakaa kimya. Hakika hakunipenda na wala hakukaa kufikiria kuwa na mimi hata siku moja, najutia muda nilioupoteza kwake.
ha! Ha! ha! Haaaaa...! Aisee pole hako kana mtu wake tu, kupigiana sim na mambo mengine huonesha mtu anajal lkn kanauchuna! Au ndo kanajiandaa na UE? Kachunie zaidi mwishowe utakasahau tu.
 
ha! Ha! ha! Haaaaa...! Aisee pole hako kana mtu wake tu, kupigiana sim na mambo mengine huonesha mtu anajal lkn kanauchuna! Au ndo kanajiandaa na UE? Kachunie zaidi mwishowe utakasahau tu.

hakuna cha UE wala nini, ndo kwanza anaianza semista. Najitahidi kumdelete kwa kichwa japo anadai hana mtu.
 
Penda panapopendeka usije ukawa unapoteza muda wako kama ameshakuambia mapenzi no ..bado unaendelea kujiumiza kwa nn usitafute mwanamke ambaye utampenda naye atakupenda mkapendana kulikon kumpenda mtu asiyekuwa na time wewe kwa mtazamo wangu
 
yes ni uwamuzi sahihi, najua inakuuma sana lakini katika dunia kuna vitu hapa uvipende vipi utavikosa tu, pia fahamu wewe unampenda yeye ila yye hakupendi wew yupo anae mpenda yeye na huenda huko nae hapendwi vivyo ivo,the same case nawe kuna mtu anakupenda sana wew ila huenda wew humpendi au hujamjua bado,vuta subira kaka
 
fanya vitu vingine in short huyo dada ameshakuona kwamba wewe ni looser so tafuta manzi mwingine,,,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom