Je; Ni SMS Zipi Za Mapenzi Za Kukuacha Hoi Ulizokutana Nazo ?!

Kuna mmoja aliwahi kunitumia message ilikuwa inasema "Niko tayari kukupa mshahara wangu wa kila mwezi kuliko kukosa penzi lako"

Duh! Mkuu hebu tupe vionjo zaidi. Hii ni kali sana.

Mliishiaje?
 
Mhh kweli wewe ni mtaalam, unayejua kuitumia yako kalamu kila nikuonapo hupata hamu, hujihisi kupoteza fahamu, naomba ufahamu wewe ndio wangu mtaalam! Nakumiss

Kweli wewe ni mpishi! Umahiri wako unaanza kwenye ukunaji nazi hadi upakuaji. Upekechapo ndizi za mtori mimi huwa hoi. Nakupenda mpenzi.
 
Duh!

Hii kali sana:


Ama kweli Mungu aliumba mtoto huna kasoro kila ukipita nyuma midume hushikwa na kiholo, nakupenda.
 
Hapa Ngoma nzito!


Najua kama kweli wanipenda lakini moyini najiuliza itakuwaje, tofauti zetu za dini naona ni kikwazo, nafsini nazidiwa na mawazo, mchana mwema.
 
Mmh!

Nakumbuka siku ya kwanza maneno matamu uliyoniambia, ahadi kede ulinipatia, nakunifanya nijione malkia katika hii dunia, lakini leo umenibadilikia au kukupa penzi nimekosea?
 
Ooh My . . . .

Hivi ni kweli umebanwa na kazi au unaniwekea pozi? Mawasaliano yalikuwa hayaishi tulipolianza letu penzi, leo si simu wala sms nizipatazo toka kwako mpenzi, hakika hunipendi siku hizi, enewei sina jinsi, zaidi ya kumshukuru mwenyezi!
 
Honey hivi unakumbuka? Ahadi uliyonipa, mwisho wa mwezi ukifika pesa utanipa, nitatuwe matatizo yaliyonifika, la azizi nakukumbusha tarehe zimefika, na tatizo langu bila wewe haliwezi tatulika! Luv u mwaah.
 
Mpenzi hakika ningekupa ila tarehe mbaya zimefika hali ya hewa imechafuka, vumilia wikiendi ijayo nitakupa, usiwe na pupa, mbivu zako nitakupa hakuna mwingine wakumpa, luv u.
 
Kila siku mimi ni mtu wa kulia, ipo siku uvumilivu utaniishia, hivi ni kwa nini hutaki kutulia na kila kitu nimekupatia, wewe wehuka na hao wanaokupapatikia, lakini utaja jutia siku ikiwadia.
 
Hakika najutia nafsi yangu kukupatia mwanaume kiruka njia kila mwanamke wewe akuvutia, nguo shuruti wataka akuvuliye, katu penzi sitakaa nikupatiye.
 
weeh superman na hizo mbio unamkimbilia wa zamani?mbona unavuta sana memories?ngoja na mwenza wako nae aanze,utakoma!:spy:
 
weeh superman na hizo mbio unamkimbilia wa zamani?mbona unavuta sana memories?ngoja na mwenza wako nae aanze,utakoma!:spy:

Mkuu King;

Mimi niko Gado!

Ziko kwenye simu ya zamani (Unakumbuka Nokia Mche wa Sabuni?) wakati bado namfukuzia Mamaaa . . .

Hebu tupe vionjo vya SMS zako basi . . .
 
Mkuu King;

Mimi niko Gado!

Ziko kwenye simu ya zamani (Unakumbuka Nokia Mche wa Sabuni?) wakati bado namfukuzia Mamaaa . . .

Hebu tupe vionjo vya SMS zako basi . . .

u should pay rent for spending so much time in my head,lol!
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom