Je, ni Skills tu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, ni Skills tu?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Dec 21, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,606
  Likes Received: 5,781
  Trophy Points: 280
  Je, ni Skills tu?  [​IMG]Hata kama skills ni jambo la msingi sana katika sex, kuwa na moyo ulio wazi na hamu ya kujikabidhi kwa mume wako au mke wako husaidia kuwa na uzoefu wa sex inayokupa ridhiko zaidi.
  Hata hivyo njia bora ya kujifunza au kutojifunza ni actions; kumbuka mwili wako ni uhuru wako na upo responsible ni kitu cha lazima au hiari na unaweza kuupa uhuru mwili wako kwa kufanya Yafuatayo

  KWANZA
  Husika na mwili wako. Usikilize unakwambia kitu gani hasa jinsi unavyojisikia na nini unataka na unachohitaji ili kufanya kazi katika kiwango chake cha juu. Upe chakula kizuri, muda wa kupumzika, mazoezi kiasi cha kutosha na milango ya fahamu iliyo imara.

  PILI
  Uwe mwepesi kutambua message negative kuhusu mwili wako hasa zile ambazo wengine wanakwambia na zile wewe unawapa wengine.
  Hakikisha unafanya replacement na positive messages kwa mwili wako na wengine.

  TATU
  Ukiwa na mpenzi wako hakikisha unampa mguso wa mwili (touch) ulio mwororo na caring.

  NNE
  Badilisha mtazamo wako kuhusu sex kutoka kufanya na kufika kileleni (performance and orgasm) na kuwa kupeana raha na kuunganishwa (pleasure and union)
  Jifunze kufanya sex kuwa sanaa yenye raha.
   
Loading...