Je ni sheria ya nchi mfanyakzi kukatwa BIMA ya afya bila kuwa mwanachama?

Mong'oo

Member
Oct 13, 2008
56
0
Je ni sheria ya nchi mfanyakzi kukatwa BIMA ya afya bila kuwa mwanachama wa BIMA hiyo?
Kuna jambo ambalo linanisumbua kichwani kuhusu kujiunga na matibabu ya BIMA ya afya.
Nauliza jamani ni lazima kujiunga nayo? Je nikiamua kutibiwa
kwa hela yangu hospitali nayotaka mimi na familia yangu itakuwaje?
Je ni halali kukatwa BIMA ya afya bila kuwa mwanachama? Kwa nini wanakata kila mwisho wa mwezi bila ridhaa ya mtu?
Mimi silielewi hili jambo.
Mwenye maelekezo atuelemishe tafadhali.
 
Si halali kuchangia kitu ambacho si mwanachama.

Ila kama upo serikalini kwa ujumla wake wameamua kila mfanyakazi kukatwa bima ya afya. Kwa maoni yangu inaelekea watu wa accounts wanakuwa ni wavivu na kufanyakazi kwa mazoea bila kuwa analytical katika majamboz.
 
Serikalini Bima ya Afya ni lazima na ndio uanachama wenyewe,kujiondoa uanachama ni kujitoa Serikalini.Upo hapo?
 
Serikalini Bima ya Afya ni lazima na ndio uanachama wenyewe,kujiondoa uanachama ni kujitoa Serikalini.Upo hapo?
Ni kweli, lakini mpaka sasa sio makundi yote ya watumishi wa serikali ni wanachama wa Bima ya Afya. Kwa mfano wanajeshi wote kwa maana JWTZ, Polisi, Magereza n.k. sio wanachama wa Bima ya Afya japo kuna mpango wa kuifanyia marekebisho Sheria iliyoanzisha mfuko huo ili kumwezesha waziri mwenye dhamana kuendelea kuongeza wanachama kadiri atakavyoona inafaa.
 
Back
Top Bottom