Je, ni sehemu/mahali gani naweza kupata exposure ya kimaisha?

ugalila

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
652
599
Leo hii vijana wengi ni watafutaji wa maisha na mwenyezi mungu anakubariki kadri ya jitihada zako zenye tija , leo nimejaribu kucheki na jamaa zangu wawili watatu wote wapo ugaibuni, nilivyowadadisi kidogo wote wamejiweka kwenye mazingira ya kupata exposure zenyewe , mmoja alipata kazi UN kapangiwa branch ya ugaibuni, wengne wawili walikuwa na karibu na mchungaji wakapata chance wakadandia flight na baba mchungaji wakabaki kwa ajili ya kujiendeleza vikozi vya hapa na pale.

Msingi wa maelezo hayo yote ni kutoa picha ya jinsi baadhi ya watu wanapata exposure ya kimaisha kama kukutana na watu wenye exposure kubwa ndani ya nchi na kufanya nao mazungumzo ili uweze kufanana nao kwa mafanikio kupitia exposure na uzoefu walioupata, au ni njia zipi unaweza kupitia ukapata exposure kubwa ya kimaisha tofauti na exposure uliyonayo sasa,

Note: Haya maisha pasipokutafuta fursa ,fursa haziwezi kuja wakati umejifungia ndani, yahitaji kujichanganya uweze kukutana na fursa mbali mbali maana kwa stahili za maisha ya kibongo Unaweza ukafika 50yrs ujatembea popote na level yako ya maisha ni ya watu wenye mitaji chini ya laki tano .
 
Nchi za kuanzia kupata mitaji kwa vijana ambayo ukienda ukakaa hata mwaka mmoja tuu zimekua ngumu sana kuingia na ukiwa huko wanafatilia sana makaratasi tofauti na kabla ya Ma terrorist hawajaingia zilikua ni Hong kong..Singapore kwa wajasiliamari kwa vijana wa shule ni stellenbosch university au Unisa ukisoma hivyo vyuo huko huko unapata kazi nzuri tuu sasa tatizo fees kwa sasa ipo juu sana tofauti na miaka ya nyuma.
 
Nenda Hong kong camteen uwe unarudi bongo kila visa ya miez mitatu inapoisha Camteen ndio magarivya bei chee yanapouzwa na vitu vingi vya electronics hata ukiwa na nauli tuu ukakaa huko utapata hela ya kutuma mizigo tofauti na Bongo..
 
Gharama zake za kwenda na kurudi zipoje?? Vipi gharama za kuishi kwa siku ukijumuisha chakula malazi??
 
Je gharama ya kwenda kurudi n sh ngapi? Je living cost zipoje?
 
mkuu ntaelekeza sehemu ambayo sijakwenda hatupo kujisifia kwa mmi nilieenda Nchi nyingi nikiwa natafuta maisha naelekeza wenzangu wanaotaka kutoka pia mkuu..
Yani hapo ndio umemuelekeza, acha masihara, nenda jukwaa la ujasiriamali kule kuna mdau msome vizuri uone anavyotowa data useful kwa wanaotaka kufanya biashara China, tofauti na huu uhuni ulioandika wewe.
 
matola huyo sio mfanyabiashara kwa jinsi nolivyomuelewa snataka aende sehemu akachange ili afanye biashara akiwa na mtaji hong kong pako vizuri ndio maana nikamuelekeza akitaka kwrnda atapewa mbinu za kwenda pale maana ni wasumbufu sana ila akifika kuna sehemu rahisivya kuishi Camteen na vitu vinapatikana huko..China ataenda mtaji hana au nimekosea wapi
 
Mkuu hebu changanua zaidi habari za Camteen,inaonekana una point hapa.
Gharama zake za kwenda na kurudi zipoje?? Vipi gharama za kuishi kwa siku ukijumuisha chakula malazi??
 
Nenda Hong kong camteen uwe unarudi bongo kila visa ya miez mitatu inapoisha Camteen ndio magarivya bei chee yanapouzwa na vitu vingi vya electronics hata ukiwa na nauli tuu ukakaa huko utapata hela ya kutuma mizigo tofauti na Bongo..
hilo bichi halifai tena kaka.hong kong ya sasaiv njaa tupu sio camteen,sham shui po wala pale chunking,asilimia kubwa ya waliokuwa kule wamerudi bongo na baadhi wako Guangzhou,Sasaivi kupata ile viza tu ni mtihani mie nmeenda mwishoni mwa mwaka jana almanusura wanirudishe,nmespend zaidi ya masaa matatu pale migration na custom.halaf hata kutuma vitu kutoka kule hailipi kama zamani
 
titimunda huo utaratibu wa kusumbua wageni upo na kila Nchi wanafanya ivyo sisi ndio wenye shida inatakiwa kukubali wao wanachokitaka maana wabongo wameharibu sana..na siwezi amini kwamba bora kuchanga bongo kuriko kule kwa wanaoanza kumbuka unapokua beginner ndio nalozungumzia bongo watu wanataabika sana fulsa kule zipo mkuu hata kuwe kugumu vp huwezi fananisha na Dar bwana..
 
Ila unachozungumza upo sahihi kwamba kwa kuwa wasafiri wamepungua kupata hela haiwezi kuwa kama zamani ila bidhaa still zipo ukiweza kutuma unapata chochote mkuu..mimi mwaka huu nilikua kule kuna vitu natoa pale napeleka South Africa naona sio mbaya kivile bei zao still zipo chini na vitu vyao vipo bora mkuu na sasa ivi supply ipo juu demand ipo chini kuriko zamani
 
Vietnam wana electronics ipo bei chini kuriko china ila ni kwa mtu mwenye mtaji wa kutosha maana hakuna kupakia loose cargo pale Cambodia wana saa zile Original nzuri unaweza ukafata pale pia bei yao ipo chini sana viwanda vingi vya makampuni ya ulaya vipo hapo
 
Ila unachozungumza upo sahihi kwamba kwa kuwa wasafiri wamepungua kupata hela haiwezi kuwa kama zamani ila bidhaa still zipo ukiweza kutuma unapata chochote mkuu..mimi mwaka huu nilikua kule kuna vitu natoa pale napeleka South Africa naona sio mbaya kivile bei zao still zipo chini na vitu vyao vipo bora mkuu na sasa ivi supply ipo juu demand ipo chini kuriko zamani
yeah skuiz wasafiri wamepungua.wengi wanaenda mainland kwahyo kunakuwepo ugumu hata kwenye utumaji wa mizigo na zile dili zetu za udalali.ila kaka Hong kong ya sasaiv haifai kwenda kama beach tena.angalau uwe mzoefu nako
 
Vipi vietnam kukoje nako.wanatoa viza za muda mrefu .nataka nikijaaliwa mwaka huu niende nkasafishe macho
 
yeah skuiz wasafiri wamepungua.wengi wanaenda mainland kwahyo kunakuwepo ugumu hata kwenye utumaji wa mizigo na zile dili zetu za udalali.ila kaka Hong kong ya sasaiv haifai kwenda kama beach tena.angalau uwe mzoefu nako
yaa sema mainland ndio sio ila kwa mtu akiamua kufata vitu pale na akaja kuuza Tz akiwa na hela kidogo sio mbaya maana bongo hakuna ishu kabisa kwa vijana bidhaa hakuna zilizopo zipo bei juu sana mtu akibeba mzigo wake kilo 100 zinamtoa vizuri tuu au
 
kweli kaka nachopendea hong kong vitu vyao asilimia kubwa ni original vile vya kuuzwa ulaya.naonaga wachina wanatoka mainland wanaenda kufanya shopping HK.na vitu vya mtumba bei ni sawa na bure hasa mafriji,pasi,rice cookers na electronics nyengine.ishu kisafirisha tu.natamani enzi zile Silent ocean wangekuwa wanaopareti HK
 
yaa vietnam kuna bidhaa nyingi sana wakenya wanachukulia pale mizigo yao ukiweza chukua visa ya thailand shuka na Ethiopian unapita na bus cambodia then vietnam hawasumbui na vtu vingi nenda mkuu
 
Back
Top Bottom