Je, Ni sawa mwanzo wa mahusiano mwanaume akahamia nyumbani kwa mwanamke?

rasta got soul

JF-Expert Member
Dec 16, 2015
234
114
Habari gani wadau,

Natumaini weekend iko poa na inaishia vizuri na tunajiandaa kwa mchaka mchaka wa wiki nzima.

Hebu tupeane mawazo zaidi. Kwenye hili jambo. Maana limekuwa gumzo kwa maisha ya sasa. Lets say umekutana na bi shosti ukamuelewa ukatupiamo mistari akaingia king.

Mkaanza mahusiano wewe una kazi yako na kipato chako ni cha wastani na bi dada nae hivyo hivyo.Later on penzi lika noga mkaamua muishi pamoja kwa sababu tusizozifahamu ukahamia kwa bibie na maisha yakawa yanaenda fresh.

Je hapo kuna tatizo? Nimeanzisha uzi huu coz nimesha ona nyuzi kadhaa humu ndani zenye mahadhi haya na watu wengi wamekuwa wakiponda sana.Kwangu mimi sioni tatizo as log as wahusika wanaelewana na wanaishi kwa amani.

Nawakilisha
 
Hakukuwa na haja ya wewe kuanzisha Uzi, kwasababu ulishapata majibu kutoka kwenye hizo Nyuzi zingine.

Afu kwanini mwanaume uhamie kwa Mwanamke badala ya yeye kuhamia kwako??

Wakati mwingine mnasababisha wenyewe mdharaurike.
 
Siyo lazima iwe hivyo sometimes mwanamke ana uwezo kuliko mwanaume kwahiyo anaona bora amsaifie mwenzie
 
Kwa nini unataka kuhamia kwa mwanamke ukihamia ni moja kwa moja wewe mwanaume unakwepa majukumu mara nyingi nimeona mwanaume akihamia kwa mwanamke huwa anakwepa majukumu kama ya kulipa kodi ya nyumba maana hata nyumba hamtabui pia maswala ya msosi wengi wao hawajishughulishi wanajua utafanya tu maana ni kwako.
 
Ni kwa sababu imeandikwa kuwa mwanamke ataachana na wazazi wake naye ataambatana na mumewe,nao watakuwa mwili mmoja. Labda wewe utupe swaga tofauti...wanaita"Experience the difference"
 
We hamia tu siku mkimwagana akutupie nguo nje ndio utatia akili
 
Hakukuwa na haja ya wewe kuanzisha Uzi, kwasababu ulishapata majibu kutoka kwenye hizo Nyuzi zingine.

Afu kwanini mwanaume uhamie kwa Mwanamke badala ya yeye kuhamia kwako??

Wakati mwingine mnasababisha wenyewe mdharaurike.
Umeongea yote.
 
Back
Top Bottom