Je, ni sawa kwa wanafunzi wa O-level kuruhusiwa kutumia vikokotozi (Calculators)?

Emery Paper

JF-Expert Member
Jun 1, 2019
1,429
2,713
Ni matumaini yangu basi wadau wenzangu wa Elimu mko salama kabisa!.

Kama kichwa cha uzi kinavyouliza, nimeshangazwa sana na haya mabadiliko ya kiteknlojia katika elimu, kitu ambacho kimepelekea wanafunzi wa kidato cha nne kuruhusiwa kutumia vikokotozi katika mitihani yao. Nakumbuka miaka ya nyuma vikokotozi viliruhusiwa tu kutumika kwa wanafunzi kuanzia kidato cha tano.

Hali hiyo, ilitufanya watu wengi akili zetu kuwa active, kwani hesabu ndogo ndogo tulizipiga kwa kutumia vichwa vyetu. Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi sana juu ya sababu za kuwaruhusu wanafunzi wa kidato cha nne watumie calculators pasipo majibu.

Je, ni sawa kwa wadogo zetu kuruhusiwa kutumia calculators ? Na je kuna faida zipi kwa wao kuruhusiwa ?
 
Baada ya darasa la saba kuwekewa hesabu za multiple choice naona wameamua kuwaruhusu O'level watumie vikokotozi, kwa maoni yangu naona hii haijakaa sawa wanawadumaza vijana ubongo mwisho wa siku tunapata vijana ambao wanashindwa kupambanua mambo, UNAKUTA F4 GRADUATE ANASHINDWA HATA TABLE YA 12. hii hapa chini ni mtihani wa f4 pre national.
Masiya @upepowapesa Deadbody
IMG_3741.JPG
 
View attachment 1216646
This is too sad. Sijui waliokuja na haya maamuzi waliwaza nini au wana maono gani juu ya kizazi hicho kijacho cha vikokotozi?. Kwa hiyo ni kumaanisha four figures zinaenda kosa matumizi, hesabu za logarithms zinaenda kusahaulika. Na bado mwanafunzi anapewa masaa 3 ya kuufanya mtihani ambao anatumia kikokotozi.
 
Kama ni mbumbumbu atabaki kuwa mbumbumbu tu na vipanga watabaki kuwa vipanga tu....unaweza mpa mtoto kila kitu na akashindwa kuvitumia na mwingine ukamnyima kila kitu na akavitafuta mwenyewe na kuvipata plus ujuzi wa kuvitumia juu.
 
Waacheni watumie, sisi tusiyotumia hatujafaidika na kitu chochote, na ulimwengu wa sasa unavyokwenda mbio lazima twende nao, huko ulimwengu wa kwanza wanatumia nyenzo za kuwasaidia katika shughuli zao ndiyo maana wanapiga hatua, bora wanafunzi wajifunze angalau jinsi ya kutumia calculator.
 
Ni kweli kabisa mkuu ulimwengu unavyokwenda mbio tunatakiwa tuende nao mbio kwa kuzalisha watu ambao wapo smart kichwani ambao wanaweza kufikiria,, sasa kama mtu hesabu rahisi kama za f4 anasolve kwa kikokotoo atakuwa vipi katika kupambanua mambo?
 
Me sioni ubaya wowote mtu kama anaelewa kitu ni anaelewa..ukipewa calculator leo kama hujui swali lina sovika vipi utaishia kushangaa

Watu bado wanaamini mtu kusoma kwenye mazingira magumu ndio anakuwa smart kichwani ambayo si kweli

Kusolve hesabu za F4 bila kikokotoo sio kusoma katika mazingira magumu mkuu
 
calculator omeruhusiwa kutumika katika somo moja tu la physics na itakua applicable zaidi kwenye practicals.

ni kweli pamoja na yote ilikua inatesa sana mwanafunzi kupoteza muda mwingi kufanya hesabu ambazo actually physics siyo hesabu.

binafsi sioni tatizo....naona wamechelewa sana
 
Elimu inazidi kurahisishwa, watoto washindwe kufaulu tu ila kuna hatari kubwa ya kuwadumaza kiakili na kuwafanya wawe na upeo mdogo wa kufikiri.
Na bado wataendelea kutuimbia tujiajiri na kusahau aina ya wahitimu wanaowatengeneza.
 
Waacheni watumie, sisi tusiyotumia hatujafaidika na kitu chochote, na ulimwengu wa sasa unavyokwenda mbio lazima twende nao, huko ulimwengu wa kwanza wanatumia nyenzo za kuwasaidia katika shughuli zao ndiyo maana wanapiga hatua, bora wanafunzi wajifunze angalau jinsi ya kutumia calculator.
Kuna kitu kitakosekana nacho ni mind sharpness. Jaribu kukumbuka enzi unafundishwa table, hauoni kuwa zilikufanya akili yako ikawa sharp na kurespond timely ? Leo hii unategemea huyu anayeruhusiwa kutumia calculator atakuwa mtu wa aina gani ?
 
This is too sad. Sijui waliokuja na haya maamuzi waliwaza nini au wana maono gani juu ya kizazi hicho kijacho cha vikokotozi?. Kwa hiyo ni kumaanisha four figures zinaenda kosa matumizi, hesabu za logarithms zinaenda kusahaulika. Na bado mwanafunzi anapewa masaa 3 ya kuufanya mtihani ambao anatumia kikokotozi.
Labda idadi ya maswali itaongezeka
 
Imechelewa sana. Kikokotozi hakimfanyi mtu ajue kitu. Kama mtu hajui, hajui tu. Kama anajua, anajua tu.

Hapa naweka bold prediction: Mashule mengi Tanzania yanapiga marufuku simu za viganjani. Itafika siku yataruhusu kutumia simu (rununu, vishikwambi au tekenolojia yoyote itakayokuwa inatamba wakati huo), na hata kuzitumia darasani kwa mafunzo.
 
Back
Top Bottom