Je, ni sawa kupiga stori za mapenzi na Shangazi yako?

IGADESA

JF-Expert Member
Jan 15, 2021
295
721
Habari wana jamvi!

Kwangu mimi binafsi hili swala la kuweza kufunguka mahusiano ya kiundani ya madem zangu naowagonga kwa shangazi au mama mdogo ni ngumu sana.

Siku za hivi karibuni nilienda kwa mshkaji wangu flani hivi tunamwitaga Mesi, anaishi nyumbani kwa shangazi yake ambae ameolewa na bosi flani hivi na ana watoto watatu, Mesi ana umri wa miaka 26 na shangazi yake ana umri wa miaka kwa kukadiria 40 .

Siku hiyo tupo sebleni tunachek muvi tukiwa pamoja na anti yake watoto walikuwa wanacheza nje basi Mesi akaanza kufunguka pale,

"Anti yule dem wangu anaekujaga kunifulia aliniletea mizinguo sasa hivi nimeachana nae, kwa hiyo hatokuja tena",

Anti yake akasema " wewe nishakuzoea unapenda kuwagonga watoto wa watu lakini kuoa hutaki" na Mesi akaendelea kusema" hapana shangazi wengine ni rafiki tu, ninaowagonga hawazidi hata watatu".

Dah, mi pale sebleni najifanya nakenua meno kumbe nawashangaa mtu na shangazi yake aina ya stori wanayopiga bila hata kupindisha maneno.

Hivi kweli ni sawa kufunguka kuhusu mahusiano yako kiundani kwa shangazi zetu ama hata mama wadogo kama ambavyo mshikaji wangu Mesi amefunguka kwa Shangazi yake ama ndo mambo ya kwenda na wakati?
 
Ni sawa lakin sio kuingia ndan kihivyo nnachojua naweza kuongelea mapenz na maant na maanko ila sio wazazi
 
Huo mda wa kukaa na shangazi/mama wadogo kuzungumza masuala yaan mapenzi unatoka wapi? lol
 
Hili ndio life la kizazi cha sasa. Malezi ya familia yashakwenda mrama hivyo tunapata jamii yenye kujiachia
 
Back
Top Bottom