Je ni sawa baba kumuomba msamaha mwanae | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni sawa baba kumuomba msamaha mwanae

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Feb 18, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Katika mazingira ambayo tunakulia sisi watanzania mara nyingi mama ndio anakuwa karibu na watoto zaidi kuliko baba. Ofcourse hii inaweza kubadilika kutegemea na familia husika. Ila kwa mtazamo wa ujumla naweza kusema hivi ndivo ilivyozoeleka. Sasa mara nyingi baba anakuwa mkali kwa watoto inafikia hatua mtoto akimuona baba amerudi kutoka kazini badala ya kufurahia ndio anasikitika. Anamsalimia then anatafuta sehemu ya kujificha. Well, hili si tatizo sana maana sometime inakuwa ni nature ya mtu kwamba anakuwa yupo hard kwa kila mtu hata kwa familia yake.

  Sasa tatizo linakuja pale huyu baba ambaye hana ukaribu na wanae pale anapojikuta amemchapa mwanae kimakosa au kampiga kimakosa then kwa sababu yupo too superior anaona kuomba msamaha kwa mwanae ni udhaifu. Akijiangalia kwa jinsi anavyo behave then aseme samahani....anaona duh hii nitakuwa nimejishusha hadhi yangu. Anaamua kunyamaza tu na kuendelea na maisha kama kawaida.

  Sasa ubaya wake ni kwamba mtoto nae anakulia katika mazingira kama hayo. Hajafundishwa kuomba msamaha na hajawahi kuombwa msamaha. Hali hii inakuwa inaendelea kutoka kizazi hadi kizazi. Mimi sidhani kama ni aibu au kujidhalilisha kama ukiamua kuomba msamaha pale unapofanya makosa hata ka wale waliokuzidi umri. Ndio inakuongezea heshima maana binadamu mara nyingi tunakumbukana kwa mabaya so watu wanapokuzungumzia pale ulipochemsha basi watasema pia kuwa uliomba msamaha. Mimi kwa mtazamo wangu nadhani ndio inaongeza utu wako mbele za watu.

  Anyway point ya muhimu niliyotaka kuisema ni kwamba mara nyingi kuomba msamaha kwa mwanao inakauwa ni vigumu zaidi kama utatengeneza umbali kati yako na watoto wako. Ikishakuwa hivyo kama ukimfanyia makosa mwanao kuomba msamaha inakuwa ni kazi ngumu sana. Kuna familia moja naifahamu ambayo baba na mama huwa wanashindana kutengeneza ukaribu na watoto wao hali ilinivutia sana sio siri. Hope kwamba we can adopt some ways of living from other families. Hii haimaanishi kuwa upo dhaifu. Kwa sababu be sure kwamba zipo pia familia ambazo pia zina adopt some ways of life from you
   
 2. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Yeah, umenikumbusha story fulani ya udogoni. Kuna rafiki yangu mmoja baba yake alikua mkali sana. Siku moja jioni nami nikiwa hapo kwao tukicheza yule rafiki yangu (Stan) alivunja glass ya maji. Kwa kweli ilikua ni bahati mbaya maana alitereza. Dingi alimcharaza ilhali mtoto aliomba sana msamaha na dingi aliona tukio zima la kuteleza. Baada ya kama nusu saa dingi nae alivunja glass maana aliiweka kwenye meza na akasahau wakati anaamka, akagonga kile kimeza na glass kuanguka na kuvunjika. Alijichekesha kiunafiki na kuonyesha kwamba bahati mbaya ni kwa mkubwa na si kwa mtoto/watoto. Ni tukio nisilolisahau hadi sasa ni mtu mzima.

  Matukio kama hayo na elimu tuliyoipata na ulimwengu huu wa utandawazi naamini umekua chachu ya mm na wengine kubadilika, hususani katika suala zima la makuzi ya watoto. Ukishajua tu binadamu, na binadamu hutokea akakosea, na hivyo busara ni kuomba msamaha, application ya hiyo ni kwa kila mtu regardless of rika, mila, social status (mwisho wa siku social status inabidi iishie getini/mlangoni, ukishafika nyumbani kwenye familia yako) etc.

  Kizazi hiki cha bongofleva, mambo yamebadilika, yanabadilika na yataendelea kubadilika....... Naamini zimebaki familia chache tena watoto ni wa utandawazi, wababa ndio bado wahafidhina wa hizo masculinity hegememony na ambao wanashindwa cope mwishowe.... wanaishiwa haribu watoto katika makuzi..... mtoto anaona hili ndo linafaa dingi analazimisha afate vile alivyokulia yeye, anasahau hakukua na computer, TV, AC, etc, leo mwanae anakua navyo ndani.......
   
Loading...