Je, ni salama kwa kiongozi mkuu wa nchi kufanyiwa dhihaka?

Kudhihaki mtu yoyote ni kumdharau hata mtoto akidhihaki mzazi ujue anamapungufu na hana adabu hivyo anastahili kufunzwa na kushikishwa adabu kwa adhabu..
Vipi mzazi akimdhihaki na kumdharau mtoto? Respect must be reciprocal!
 
Tatizo Matusi na dhihaka ni sehemu ya utamaduni wetu wa Kitanzania.

Kwenye majukwaa ya kisiasa huko matusi na dhihaka ni kama kawaida. Wakati wa kampeni 2015 matusi ma dhihaka zilitawala uchaguzi .... Kuna watu walidiriki kusema mbele ya jukwaa kuwa hawatapeleka MAITI Ikulu sasa unategemea leo matusi na dhihaka zitajifutikia tu kwa vile uchaguzi umeisha............!!?

Humu jukwaani watu wanatembeza matusi ......... kila second comment kuna tusi au dhihaka!!
Jukwaani walisema mamvi kajinyea bd unataka ww usidhihakiwe kuna wakati tunatakiwa tukubali tuende sawa bhana
 
Kwanza ujue yule tunamlipa sisi... kuwa rais haimaanishi uheshimiwe tu bila kuheshimu.
Pili.. Unaposema anajenga reli n.k sio pesa yake ni kodi zetu wananchi... Wala hakwenda na pesa ikulu zaidi ya nguo tu.
Mwambie aache kutukana wenzie majukwaani nao hawatamtukana.
 
Busara ya kawaida kabisa inakutaka kunyamaza.mimi nimemwelewa sana Mh Rais pale alipoomba aombewe kwa Mwenyezi Mungu.anajua yeye ni mwanadamu anamapungufu anaomba tumwombee ili Mwenyezi Mungu amsaidie aongoze vyema.
Nahisi maombi bd hayajibiwi mjitahidi kumwombea basi
 
Ombi langu kwenu wote tunapaswa kumheshimu na kumsaidia ili atuongoze mpaka muda wake utakapokwisha.Kumbukeni anaweza akawa amekosea kwa mtizamo wako lakini kwa maslahi mapana ya nchi anapaswa kuungwa mkono.
SAWA ILA NAE LAZIMA AWE NA HESHIMA SIYO ANAKUWA KIBURI!!!!!!!
 
Mungu na watawala nani wakuheshimiwa? Mungu anadhihakiwa na watawala wanaoamua fulani anyongwe, fulani afunguliwe hata kama alibaka, fulani aliiba pesa za umma ingawa hakukamatwa na aliowagawia hawakushtakiwa lakini asote ndani. Huyu Mungu kwa nini tunamtesa? Rais ni cheo cha miaka 10 kwa Tz ingawa marais wa nchi jirani wanaona wadumu mpaka vifo viwatenganishe. Je, baada ya uRais kuna maisha au hakuna?

Wale wanaoitwa wapumbavu baada ya urais watakuwa sane au bado watakuwa wapumbavu vile vile? Rais kawekewa mafuta kwani yeye ni mfalme kusema ametoka ukoo wa wafalme au yeye askofu au Papa?

Ni mtumishi wa watu ndo maana marais wa nchi zilizoendelea na demokrasia ilipokua wanachorwa vikatuni, wanatukanwa, wanatangazwa kwenye vyombo vya habari na wanakosolewa adharani bila woga wala aibu. Na hakuna mtu anaweza kuwafanya chochote. Mtoa uzi labda unafikiri tuna mfalme. Tunaelekea huko any way sababu mtu kaongea kuwa nanii ni nani kwani? sasa hivi anasota jela. Tutaona mengi ila time will tell. Labda mtu aamue kufia madarakani kama Kamuzu Banda otherwise........
 
Magufuli anajenga Reli ambayo itakuwepo kwa miaka mingi ijayo,si kwa manufaa yake bali kwa manufaa ya nchi,Magufuli anajenga miundombinu mikubwa ya kuzalisha umeme ambayo itakuwepo miaka mingi hata baada ya yeye kuondoka lakini kwa ajili ya nchi.Pale ambapo tunahisi Mh amekosea ni vyema kutumia lugha ya staha na heshima.tuepuke matusi.N
HAYO YOTE BILA KUWA NA DEMOKRASIA NI KAZI BURE KABISA!!!!!!!
 
Mkuu hapo umeandika vitisho vitisho tu. Mara eti "ni mpakwa mafuta kwa Mungu"

Huyo Mungu alishawahi kumwona? Alimpaka mafuta lini? Nani alihudhuria hilo tukio? Tunaomba ushahidi angalau wa kapicha kamoja.
 
Crap
Magufuli hakuchaguliwa na Mungu,bali alipita kwa kura za maccm na wizi wa kura uliosimamiwa kwa ustadi na Kikwete,Mkapa na Lubuva
Usimsingizie Mungu,hawezi kufanya ujinga huo.
 
HAYO YOTE BILA KUWA NA DEMOKRASIA NI KAZI BURE KABISA!!!!!!!
Mimi najizuia sana kutokutoka kwenye Mada. Demokrasia ni Pana sana.inategemea una mtizamo upi.Ikumbukwe katika nchi zetu hizi.kiongozi wa nchi ndio anatoa mwelekeo wa demokrasia au Aina ya utawala anaotaka.Na hakuna anaeweza kumshitaki kwa hiyo turudi tu kwenye Mada ambayo inaomba tuwe na heshima na staha kwa kiongozi wetu
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom