Ngolinda
Senior Member
- Apr 12, 2010
- 125
- 25
Kuna habari kwamba waandishi wa habari hasa kutoka habari corporation wanatumika katika kampeni za kumnadi Rais Kikwete, na wale wote wanaokwenda kinjume na maslahi ya CCM wanafukuzwa katika msafara wa kampeni za Kikwete kama ilivyotokea kwa mwandishi wa gazeti la mwananchi. Na juzi wanahabari hao katika msafara wa Kikwete walionekana wamevalia vijikoti vyenye picha na maneno ya kumnadi mgombea huyo. Maswali ni: Je, ni sahihi kwa wanahabari kutumika kupiga kampeni na kuandika habari kwa maslahi ya kundi fulani linalosaka madaraka?. Je, haya ndio maadili ya wanahabari? Na kama media ikikubali kutumika kwa maslahi ya kundi fulani, hii si kuhatarisha maslahi na mustakabali wa nchi yetu?