mambomengi
JF-Expert Member
- May 16, 2009
- 829
- 242
Nimetatizwa na Serikali kutokuwachagua vijana 29 kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita eti kwasababu wanaumri unazidi miaka 25!
Je serikali inakumbatia ujinga? Nafikiri ingekuwa bora wale waliochelewa kusoma wasaidiwe (wasipendelewe) ili walau waweze kuelimika--sasa hawa 29 wamefaulu kwanini wasiendelee na masomo. Au Kauli mbiu ya serikali ni "Elimu ina mwisho"

Dk Kawambwa alisema mwaka 2010 wanafunzi waliochaguliwa walikuwa asilimia 83.52 ya wenye sifa, hivyo mwaka huu kuna ongezeko la asilimia 12.63, kwa awamu ya kwanza.Alisema wavulana 624 sawa na asilimia 2.42, hawakuchaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano na vyuo vya ufundi kutokana na sababu mbalimbali.
Alizitaja sababu hizo kuwa ni kutokuwa na uwiano wa alama za masomo (credits), alama kutotimia na baadhi kuwa na umri wa zaidi ya miaka 25.
Alisema wanafunzi 29 walikuwa na umri uliozidi miaka 25 ambao kisheria hauwaruhusu kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa shule za Serikali
Source: Mwananchi.co.tz