Je, ni sahihi Msando kujibu masuala ya diplomasia?

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Na Thadei Ole Mushi.

Nimeisoma Barua ya Msando yote aliyowaandikia USA.

1. Achana na Makosa ya Address aliyoyafanya Brother Msando twende kwenye Hoja nyingine za barua ya Msando. Kwenye barua ile kuanzia mwanzo Hadi Mwisho Msando kaonyesha kuwa hata Marekani huwa wanavunja haki za binadamu. Msando anataka kutuaminisha kuwa Marekani leo wakiamua Kula Kinyesi na sisi ni sawa kukila. Hakuna mahali ambapo Msando kaweza kusema Kama ni kweli haki za Binadamu zinavunjwa ama lah!... Kwa kifupi Msando anatuambia kuwa ni Kweli tumekiuka haki za Binadamu simply kwa kuwa Marekani nao wanazivunja.

2. Issue za Kidiplomasia hujibiwa Kidiplomasia na hupitia Chanel ambazo ni sahihi. Kilichofanywa na Msando ni kutaka kufurahisha watawala lakini akumbuke kuwa barua yake inazidi kuzorotesha uhusiano wetu na Marekani. Mh Kabudi sio mjinga kutafakari, Serikali kwa ujumla sio wajinga kutokumjibu Pompeo, wanatafakari kwa namna gani wanaweza kusulihisha mgogoro huu wa Kidiplomasia. Fani hii ya Diplomasia watu huisomea huwezi kukurupuka tu from no where mtu individual ambaye Hana taaluma hiyo kuanza kutuhumu mataifa Mengine. Kwa bahati mbaya kabisa barua ile copy yake ameielekeza kwa Rais wetu. Msando Hana tofauti na vijana waliovamia ubalozi wa S.A kudai Bombadia.

3. Msando naye kaingia kwenye Makosa yale yale kuwa naye anatetea ukiukwaji wa haki za Binadamu. Kwa maana hiyo Msando Siku akiwa Kiongozi hawezi kutuwakilisha Tena Marekani pamoja na washirika wake.

4. Serikali na hasa Rais hahitaji utetezi Sana anachohitaji ni Solutions, tunatetea Sana badala ya kutoa solutions. Barua ya Msando haitoweza kuitisha Marekani na Wala Marekani haitobadili msimamo kwa sababu ya barua ya Msando. Kwa maana hiyo bado tatizo linabaki na linaweza kukuzwa kwa barua hii ya Msando. Tumepoteza uwezo wa kutoa Solutions kwa sababu ya kusaka madaraka na Vyeo.

5. Kuna kasumba imeibuka kuwa ili uwe mzalendo Kila Jambo la Serikali ni la kutetea, nchi hii haiwezi kujengwa kwa kutetea makosa, nchi hii itajengwa kwa kuyaondoa makosa, kuambiana ukweli kuwa hili hapana lile sawa.

Wahenga walisema "two wrongs don't make a right". Narudi Jalalani..

Ole Mushi
0712702602
 
Ukishakuwa Ccm sifa kuu ni kujitoa ufahamu. Ccm inaendeshwa kwa ujanja ujanja sana na ushaidi ni uchaguzi ukifika wanaweka sera pembeni na wanaanza kutumia mbinu chafu sasa wameingia kwenye rada za Marekani.

Unanua ndege, unajenga reli halafu unateka na kuua watu kwa sababu za madalaka, unajenga chuki unafunga watu.

Bora nikose vyote lakini niwe na uhuru wa kuishi sio mtu kukatisha uhai wangu kisa tunapishana mawazo

Hapana Ccm inatosha sasa tafuteni watu makini kuongoza nchi au achieni nchi yetu.
 
Mwanahabari Huru,
Msando hana hoja katika barua yake, lakini kama Mtanzania ana haki ya kikatiba ya kujieleza, kuandika barua ubalozi wa Marekani, State Department, White House, New York Times, Washington Post, Jamiiforums etc.

Wamarekani wenyewe tunapenda uhuru wa kujieleza na tunamuona anatumia uhuru wake huo, hata kama hoja zake zina mushkeli mwanzo mwisho.

Natetea haki yake ya kujieleza hata kama sikubaliani na anachoeleza.
 
Back
Top Bottom