Je, ni sahihi mpwa kuwa paymaster general wa Serikali?

Mkuu Huyu dogo Dotto james bora atafute mapema pa kukimbilia maana mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka na uhujumu uchumi Dec 2025 yanamsubiri na hakwepi mfueni za kumtosha, mjomba yeye ana kinga ila dogo namuonea huruma.
Utamfanya nn acheni mdomo wenyeviti wa mtaa tu wanakula michango yenu mmewashindwa sembuse huyu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I due respect your idea!!! Naomba uwe too academic!! Kwenye utumishi wa umma ama kivyovyote vile kwanini unahisi siyo sawa??? Naomba usiseme tu siyo sawa njoo na supportive evidence!!!! Jiondoe kwenye lile kundi la fallacy of generalization!!! Ukitoa evidence kwamba hafai kwa mujibu aidha wa sharia zetu ama maadili ya utumishi wa umma wengi tutajifunza ila ukijibu kwa kushabikia hakuna cha kujifunza

Sent using Jamii Forums mobile app
Kanuni za utumishi wa umma zinaelekeza kwamba ili mtu ateuliwe kwenye nafasi ya kiuongozi au kimadaraka serikalini pamoja na utendaji bora na tabia njema ni lazima mtu huyo awe ameshafanya kazi serikalini kwa zaidi ya miaka 12 na ni lazima awe na cheo cha afisa Mkuu yaani principal officer kwenye cheo chake cha utendaji kabla ya kuteuliwa kwenye cheo hicho cha kimadaraka.
Sasa kwenye ishu ya huyo doto james hakidhi vigezo vyote tajwa hapo juu.
Hii ni nepotism at its highest level
 
Watanzania tunatatzo kwenye kufikiri

Msomi wa jf huwezi ukatetea hoja mgando kama hii!!! Hapa ndo nagundua watu wanachuki na mtu mmoja!!!

Hivi tatizo liko wapi hasa??? Kabila? CCM au Magufuli???

Hoja hizi ni za kipumbavu kabisa kwa karne hii huwezi jadili ukabila msomi mzima huko ni kukosa hekima na kujitambua naomba kama tunashindwa kujadili sera tuache mambo haya ya enzi za ujima

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee kwa akili yako hii,acha Makonda aonekane ndio genius wenu kwny chama chenu.
 
Jadili issue sio kukandia Uafrika wako ili ujihisi wewe labda ni tofauti.
Trump kaweka mwanawe Ivanka na mkwewe Jared Krusher Ikulu, wale nao ni Waafrika?
Usichokijua Jared&Ivanka hawalipwi hata senti 1 na serikali/white house kwa kazi hio ya kumshauri Trump.

Je hapa kwetu huyo bwana anayeongelewa hapa halipwi mshahara,marurupu,posho na serikali?
 
Hazina ya nchi siyo kitu cha kuvhezea inatakiwa kuongozwa na mtu mzoefu na asiyeyumbishwa na wanasiasa. Uchumi wa nchi utakapo kufa ndiyo mtajiandaa kuilinda hazina kama mboni ya jicho. Upwa siyo tatizo hata kidogo tatizo ni linakuja hivi je ana uzoefu wa kutosha?
Mbona naskia ni mchumi aliyebobea kutoka Tanroads aliyesomea Harvard.
 
Wacheni ulisu. Mtu ana haki zake kama raia wa tz. Haki hizo hazipotei eti kwa kua ni mpwa wa rais. Huyo kichaa lissu ni mwanasheria gani kazi yake kushutumu bila ushahidi. Kama ameona jinai si akafungue kesi dhidi ya rais na mpwa wake. Kinachooneka ni chuki tu. Hawa maliberali wamezibiwa mianya ya kuiba hela ya umma kila kona ndio maana wanahorojoka kama wendawazimu
Yaleyale ya awamu ya nne ya Jakaya kikwete ,Chadema walidai Sheli zote Tanzania kutoka Zanzibar mpaka Buloba Ni za Ridhiwani kikwete ,waliropoka wakasema Kila Sheli mikoa yote Tanzania zilikuwa za Ridhiwani ,safari hii Chadema wamekuja na jipya la mpwa wa Rais,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Share

Sijafahamu bado kwa nini umeona imefaa sana kwa wewe kuuliza swali hilo. Kwa maan napata shaka juu ya ufahamu mdogi wa namna ambavyo katiba yetu ya Jamhuri inavyoelekeza.

Hata hivyo si mbaya sana kwani kuelezana kwa kuelemisha si jambo baya hata kidogo. Mara nyingi serikali inaweka mikakati dhabiti katika sekta mbalimbali lakini lengo hasa ni kumuhudumia mwananchi, ili naye mwananchi huyu aweze kuleta tija kwa ustawi wa taifa.

Na kwa jinsi hiyo, sekta ya elimu pia imeweka kusudi hilo. Kwamba, vijana wa Tanzania watasoma na kisha watalitumikia taifa lao wao wenyewe. Watatumia taaluma zao kwa ajili ya ustawi wa taifa lao. Kwa hiyo, kumbe wajibu wa kulitumikia taifa kwa watu wa taaluma ni la kila mtanzania mwenye sifa.

Hatuwezi kuwa wepesi wa kutazama sana hali ya undugu ama hali ya ukabila ambao haupo hapa nchini mwetu; kwa kudhani kuwa ndio tunatengeneza hoja ya kukosoa, badala yake ndio tunaumba ubaguzi wa namna hiyo taratibu ambao athari zake zitajidhihirisha baadaye.

Kuwa mpwa wa Rais ama mtoto wa Rais ama mjukuu wa Rais ama hata mke wa Rais, haikuondoleia haki zako za kikatiba kama watanzania wengine. Unayk haki ya kutumika kwenye majeshi, unayo haki ya kutumika kwenye biashara kubwa na ndogindogo, unayo haki ya kuwa katibu wa wizara yo yote ile ndani ya nchi, ipo haki pia ya kuwa hata waziri au balozi pia. Ili mradi tu utaratibu umezingatiwa.

Kwa mtanzania hawezi abadani kupoteza stahiki zake eti kwa kuwa ni mpwa wa Rais. Jambo la msingi hapa ni vegezo na sifa, na kama anazo basi amestahili kuwa kwenye nafasi hiyo. Tusianze kuumba ubaguzi wa kikabila au wa kindugu pasipo kuwa na sababu za msingi.
Hayati baba wa taifa angekua hai.huyo kijana asingekaa kwenye hio nafasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivyo kumbe sasa hivi ni zamu ya Wasukuma...??
Ndiyo zamu yao acha watese kwa zamu,zamu iliyopita mlisema ya wakwere ,mkadai Ridhiwani kikwete anamiliki Sheli zote za Tanzania Toka Zanzibar mpaka bukoba,Sasa swala la Sheli za Ridhiwani limepotea limekuja la mpwa wa Rais msukuma kumiliki hazina ,poleni chadema Sera zimewakimbia mnatafuta ukabila,hata akiongea kichina bado mtatukana tu,subirini 2020 Lissu ataingia ikulu mtaongea lugha yoyote mtakayopenda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom