Je ni sahihi kwa watoto kuingilia ugomvi wa wazazi wao?

Random

JF-Expert Member
Jan 8, 2017
791
740
Mada tajwa hapo juu ihusike;

Kwa familia zilizo na wazazi wawili na zikabarikiwa watoto, nyingi miongoni mwazo zina ugomvi. Hii ni kwa sababu chache au nyingi znazotofautiana kutoka familia moja hadi nyingine.

Kibaya zaidi unakuta watoto kwakuwa wameshabalehe na wao wanajiingiza katika ugomvi huo kwa kuelemea upande mmoja hasa wa mama wakidai kuwa mama anaonewa na baba n.k

Chuki, fitna, na hila za hapa na pale hudhihirika kwa baba yao. Mara chache sana watoto kua upande wa baba. Pamoja na yote je watoto kuingilia vita ya wazazi ni sawa?

Tupe experience hata ya jirani yako
 
Yamekukuta mkuu? Pole
Kimsingi sio sawa, nadhani duniani kote ugomvi wa mke na mme ni ugomvi mgumu sana kuamua maana utawaamua baada ya muda mfupi wakiingia chumbani wakitoka nje wanacheka tayari ushaonekana mbaya
 
Mkuu kama hukukulia maisha hayo huwezi elewa,lkn mm binafsi ninekulia katika familia ambayo siku mbili hazipiti bila bila timbwili kunukishwa,mkiwa wadogo mnaaminishwa kua flan ndo mbaya lkn mkikua mnakuja kugundua nn hasa tatizo
 
Ndiyo maana inashauriwa wazazi waepuke sana kugombana mbele ya watoto, Imagine mtu umekuwa mtu mzima then unaona Mzee anamkwida Maza ama Maza anamkwida Mzee...Utaacha yatokee yakutokea kisa tu si vizuri watoto kuingilia ugomvi wa wazazi? Unaweza ukawaachanisha bila kuwa na upande wowote na ukipata fursa ya kuongea kitu unawaeleza wewe kama mtoto unavyoathirika na tabia yao ya ugomvi....Ila mambo yao ya ndani ya ugomvi hayakuhusu na usiegemee upande..
 
Ni kweli mkuu ni changamoto sana kuishi kwenye familia ya namna hiyo,binafsi nmekulia mazingira ya hivyo,mzee alikua anapiga sana tungi akirudi nyumbani anaanza kumzingua Mother,ugomvi unaanza.

Kuna kipindi nilitokea kumchukia sana mzee kwa mambo aliyokua akiyafanya na kiukweli ni vigumu kutokuegemea upande wowote .

Lakini nashukuru Mungu mzee kaacha pombe na tunaelewana vizuri
 
Ndiyo maana inashauriwa wazazi waepuke sana kugombana mbele ya watoto, Imagine mtu umekuwa mtu mzima then unaona Mzee anamkwida Maza ama Maza anamkwida Mzee...Utaacha yatokee yakutokea kisa tu si vizuri watoto kuingilia ugomvi wa wazazi? Unaweza ukawaachanisha bila kuwa na upande wowote na ukipata fursa ya kuongea kitu unawaeleza wewe kama mtoto unavyoathirika na tabia yao ya ugomvi....Ila mambo yao ya ndani ya ugomvi hayakuhusu na usiegemee upande..
Well said mkuu huwezi kukaa na kuangalia tu hivihivi
 
Kuwahusisha watoto katika ugomvi wa nyie wazazi. Ni mbaya sana. Kwani mnawaletea chuki. Natamani wazazi wangekuwa na Mawazo kama yangu. Ya kwamba hata mkigombana. Wanapotokea watoto. Inabidi mjishushe. Muanze na kucheza na kucheka. Hii itawajenga vizuri watoto.
Sio ngumi mateke. Mbele za watoto
 
Huu uzi, unanifanya nimuombe Mungu amlaze mahala pema peponi mama yangu!
Tokea nilivyozaliwa hadi mama alivyofariki sikuwahi kushuhudia ugomvi wa wazazi wangu.
Raha ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umuangazie apumzike kwa amani. Amina
 
Mkishakuwa na watoto mnagombania chumbani. Kuna jamaa akitaka kumpiga mkewe anamtoa out, mdada anapendeza akirudi macho yanevilia damu
 
Kuna siku nilipokea kesi toka kwa mother anaongea huku analia. Nilimbembeleza na kumfariji, nilijua mshua ana makosa lakini nikimtuhumu nikaona nitaendelea kuleta mpasuko. Nilichofanya ni kumpigia simu na kumwambia malalamiko niliyopata, hapa sikumruhusu ajitetee. Nilimwambia "wewe si ndio kichwa cha familia sasa huo ugomvi wenu sitaki kusikia baadae nitakupigia simu ukiwa umeyamaliza". Muda si mrefu nikapigiwa simu na wote wawili wameyamaliza.
Lakini haya mambo huwa ni kero sana kwa watoto.
 
Baba na mama yawapasa kutambua kuwa namna wanavoishi huwaathiri watoto wao. Hivyo yawapasa kufanya kila liwezekanalo kumaliza tofauti zao pasipo kusababisha amani kutoweka kwenye familia.
 
siku zote kama hujapitia katika familia ya namna hiyo unaweza sema simply tu kuwa watoto hawaruhusu kuingilia ugomvi Wa wazazi..ila Mimi nimeexperience matatizo hayo almost my whole life mpaka mwaka Jana baba alipoondoka kimya kimya home...siwezi kukaa wakati naona mama anapigwa mpaka nguo zinamvuka au kesho anaamka amevimba uso halafu ukifuatilia sababu ni baba kuwa na wanawake nje.....siku zote za maisha ya mama angu ilikuwa vipigo na matusi daah haya mambo yasikie kwa jirani tu....still ni baba angu ila alitujengea attitude mbaya sana towards yeye..kimsingi kukwaruzana katika ndoa kupo ila si kudhalilishana mpk kwa watoto...!!
 
Back
Top Bottom