Je ni sahihi kwa viongozi wa serikali kupewa majina na ripoti za wahalifu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni sahihi kwa viongozi wa serikali kupewa majina na ripoti za wahalifu?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Kimbori, Aug 14, 2012.

 1. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,739
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Nimesikia katika gazeti moja la Kiswahili la kila siku ya kwamba, DC amepewa ripoti yenye majina ya wauzaji wa magogo na nguzo za umeme kinyume na sheria kutoka katika msitu..
  Nakumbuka miaka kadhaa iliyopita, Mh. Raisi alipewa ripoti yenye majina ya Watanzania 11 vinara wa uuza wa unga (madawa ya kulevya). Tangu wakati Mh. apewe ripoti na majina hayo kumekuwa na maswali yasiyo na majibu juu ya nini wahalifu hao walichofanyiwa kwani madawa ya kulevya yamezidi kuongezeka hata kutishia ustawi wa nguvu kazi ya Taifa.
  Samahanini kwa kukosa vyanzo halisi vya habari, ikiwa kama kuna mdau mwenye vyanzo halisi vya habari atoe. Nawaomba tujadili hoja JE NI SAHIHI KWA VIONGOZI WA SERIKALI KUPEWA MAJINA YA WAHALIFU BADALA YA MAJINA HAYO KUPELEKWA MAHAKAMANI? Kumbuka moja ya nguzo za demokrasia ni mgawanyo wa madaraka kati ya Mahakama, Bunge na Serikali. Karibuni wote!
   
 2. kupe

  kupe JF-Expert Member

  #2
  Aug 14, 2012
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 1,025
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  nao wanatafuta njia ya kula hela na hao wahalifu ndio maana wanaomba wapewe majina na washirikiane nao. nafikiri wakuu wa wilaya hawana shughuli ya kufanya ndio sababu. otherwise hiyo ni kazi ya polisi na mahakama. coz mkuu wa wilaya sio polisi wala hakimu
   
Loading...