Uchaguzi 2020 Je, ni sahihi kwa Tume ya Uchaguzi kutoa onyo tarehe hizi kwa watendaji kutojishirikisha na masuala ya uchaguzi?

Brightg

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
373
660
Toka kampeni imeanza hawakuzungumzia wala kufuatilia wanayo yafanya Mawaziri, Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa, hawa watendaji wamefanya mengi sana wengine wamejihusisha nakuwaagiza wananchi kutowachagua wapinzani kama Mkuu wa Wilaya ya Hai, Ole Sabaya alifanya kampeni kata hadi kata, alizuia viwanja vyote vya kufanyia kampeni ili wapinzani wasifanye kampeni Hai mjini, kuna mwingine amewaandikia barua wagombea wote wamuone ana kikao nao.

Yote haya ndio yanakumbukwa leo, hivi tume kwanini hawafanyi kazi yao kama TCRA maana yake hawasubiri malalamiko bali wanayo yaona yakitendeka na kuyafanyia kazi kabla hata ya malalamiko kuwafikia. Je, hii haiwezi kudhihirisha weledi wa tume au udhaifu wao.

Je, TUME YA UCHAGUZI waendelee kusubiri malalamiko au hata wao wakiona matendo kama hayo hata kabla ya malalamiko kuwafikia wawe wamesha chukua hatua.
 
CHADEMA kila jambo nyie mnalalamika. Sasa ulitakaje yani?

Hawakusema mmelalamika

Wamefuatilia na kujiridhisha, wameonya mnalalamika, mna shida sana asee
 
CHADEMA kila jambo nyie mnalalamika. Sasa ulitakaje yani?
Hawakusema mmelalamika
Wamefuatilia na kujiridhisha, wameonya mnalalamika, mna shida sana asee
Inategemea na kilichofanyika kinaiathiri CCM au la.
 
Back
Top Bottom