Je, ni sahihi kwa nchi moja moja za kiafrika kuota Maendeleo? Je, sio kujidanganya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, ni sahihi kwa nchi moja moja za kiafrika kuota Maendeleo? Je, sio kujidanganya?

Discussion in 'Great Thinkers' started by JingalaFalsafa, May 30, 2012.

 1. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Ni zaidi ya miaka 50 sasa, tangu nchi ya kwanza Afrika kupata uhuru, na miaka karibia 20 tangu nchi ya mwisho ipate uhuru.

  Katika kipindi hiki chote kila taifa limejitahidi kujitutumua kuimba wimbo wa maendeleo, wengine wakaungana, wakabadili mifumo, wakabadili uongozi, nk. Lakini bado hakuna hata nchi moja ya weusi iliyopata kujitoa katika vilio vya raia wake dhidi ya njaa, vita, maradhi, utumwa, wizi, matabaka, unyonge, unyonyaji, uduni, kashfa, umasikini, nk. Je, ni sahihi kuendeleza hizi "personal efforts" dhidi ya adui yetu ambaye ni mmoja? Kwani unyonge wetu Afrika una chanzo kingine zaidi ya huu wa RASILIMALI ZETU KUNUFAISHA MATAIFA YA NJE, HALI KWETU DUNI? Haijalishi nani anawezesha mirija hii inayofanikisha "flow of wealth from Africa to Western Countries", utajiri uliotakiwa kuboresha barabara, shule, hospitali, viwanda, teknolojia yetu, nk.

  Kwanini tunapita kwenye njia walizounda adui zetu, zenye vipingamizi vya makusudi? TUNAOTA NDOTO GANI SISI KAMA AFRIKA?
  Nyerere, licha ya kuiweka Tanganyika huru, kama Kwame na Ghana yake, hawakulidhika bali walipigana kuhakikisha mataifa mengine nayo yanakuwa huru, walichojali ni MAFUNGAMANO YETU, ni kama jeraha mguu kudhohofisha mwili mzima.

  Hili linajulikana, lakini measures zinazochukuliwa na nchi zetu ni kama mchezo wa kimama mama, mbaya zaidi tunamsikiliza mzungu juu ya aina gani nzuri za kupigana dhidi ya wizi wao wenyewe, kweli tutafika?

  HAKUNA AFRIKAMOJA, BASI NI UPUUZI KUOTA MAENDELEO, imani yangu!

  Mungu wetu anaita!
   
 2. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,568
  Likes Received: 1,933
  Trophy Points: 280
  Mkuu jingalafalsafa, nilishindwa kukujibu jana kwasababu ile thread ilikwishafungwa.

  However, kwa kifupi, sikudhani kama MMM alitumbukia kwenye mtego wa udini kama ulivyofikiri. Niliyapenda maoni yako except pale ulipofikiri hivyo.Topic hii hapa nayo ni nzuri sana.

  NI ukweli uliowazi kuwa Africa hakuna kinachotuunganisha zaidi ya umasikini,ujinga,maradhi nk. NI ukweli usiopingika kuwa Africa bila kuja pamoja, basi hatwendi mahali, ni matumaini yangu kwamba mjadala huu utapata wachangiaji, ni mjadala mzuri sana, tuko pamoja na ninaahidi kuchangia maoni yangu hapa.

  Tuwasubiri "other sons of Africa"
   
 3. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  AFRIKA!
  1. Ina mazingira yake binafsi yaani SURA YA NCHI pamoja na WATU wake, tofauti kabisa na mataifa mengineyo!
  2. Ina nyakati zake binafsi yaani MAHUSIANO yake binafsi na mahususi kwa watu wake katika kukidhi haja ya MAZINGIRA YAKE, ambayo ni sura ya nchi na watu wake(black people)! Ni MAZINGIRA NA NYAKATI, ndivyo viongozavyo maisha ya mwanadamu.

  *1. MAZINGIRA:
  (a) Sura ya Nchi; ni vile vituzungukavyo yaani aridhi na vilivyomo humo kama mito, maziwa, bahari, mabonde, milima, miinuko, misitu, wanyama, madini, nk. Pia ni anga na vilivyomo humo kama hali ya hewa, majira mbalimbali,nk.
  (b) WATU: Yaani ni nani wenye hiyo sura ya nchi, ambapo jibu ni wazi AFRICAN LAND IS FOR AFRICANS this means BLACK PEOPLE, ni sisi WATU WEUSI.

  2. NYAKATI:
  Ni mahusiano yaliyopo katika Mazingira, yaani baina yetu kama WATU, pia baina ya WATU na SURA YA NCHI YAO. Hapa ndipo panapoibuka itikadi, falsafa, desturi, imani, tamaduni, mila, nk. Nyakati huundwa na watu katika harakati zao za ku-"master" sura ya nchi yao, hivyo basi NYAKATI NI ZAO LA MAZINGIRA, hubadilikabadilika kulingana na Mahitaji ya mazingira! Hivyo basi, kama Nyakati ni zao la mazingira, basi nyakati ndizo zizaazo mifumo mahususi ya kiuchumi, kisiasa, kitamaduni, na kijamii pia!

  Sisi kama Afrika, tuna MAFUNGAMANO MAKUBWA KABISA YA KIMAZINGIRA NA KINYAKATI, AMBAYO NDIYO YATUPASAYO KUZINGATIA KATIKA KUBUNI MIFUMO YETU BINAFSI KUTUONGOZA! Mafungamano haya hayawezi kukwepeka milele, yalikuwepo, yapo na yataendelea kuwepo! Na ukweli ni kwamba, pasi kuyatumia mafungamano yetu vizuri basi kila jitihada tutakazozifanya ni bure na upuuzi mkubwa....
  (nitarudi)
  AfricannotTanzanian.
  Mungu wetu anaita sasa!
   
 4. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #4
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  AFRIKA:
  .....Mafungamano yetu ni makubwa sana, japo zipo tofauti ndogondogo ambazo haziwezi kutufanya tutengane ila kushikamana zaidi. Wapo wafugaji, wapo wakulima, na wawindaji wachache sana. Hawa hutegemeana, hivyo tofauti zao ni mtaji mwingine wa ushirikiano wao.

  Mkono hauwezi kukataa kupaka dawa kidonda mguuni, kwa sababu athari yake ni juu ya mkono pia.

  Nchi zote za kiafrika, kilio chetu kimoja "underdevelopment", chanzo tunakijua sote ni "RASILIMALI ZETU KUTOTUNUFAISHA WENYEWE, BADALA YAKE KUNUFAISHA MATAIFA YA NG'AMBO" suluisho ni kukata mirija hii. Lakini hatuwezi kuikata pasi kujua ilipo, na imesimikwaje.

  Mirija haipo mingi sana ni michache yenye kasi kubwa: WAPI IPO?
  1. Uwekezaji. Tunawaona wakoloni wetu wakipewa nafasi nyingine ya kusimamia njia zetu za uchumi. Migodini, mbuga, aridhi, majini, angani, biashara, nk. Huwa tunajidanganya, eti tumeingia mikataba mibovu. Ni utoto, kwani hata ukiingia mikataba nao mizuri kwako, wataiba tu, haijawai kuwepo equal exchange na bepari tangu dunia ianze.
  Ubinafsishaji. Wapo ndugu zetu wanaopatiwa mitaji mikubwa na hawa adui zetu, na kuwafanikishia wanachotaka.
  2. Kutumia nguvu. Tunaona vamizi mbalimbali mara NATO, US, France,nk. Wengine wanaingia kupitia civil wars, ndege zinaruka na madini kwenda ng'ambo. Ni UJAMBAZI.
  3. Soko huria. Hapa tunawapelekea wenyewe rasilimali zetu kwa amani kabisa. Wanapanga bei, wanatupangia ushuru, hata kiwango cha uzalishaji pia.

  Hizo ndizo njia tatu kuu. Zipo ndogondogo pia kama za kutoa aridhi, madini, kama asante. Hakuna nchi yoyote ya watu weusi inayoweza kukwepa hayo milele.

  IMESIMIKWAJE?
  Tuache habari za ukoloni, ila tuje moja kwa moja katika kipi kinachobeba maovu hayo hapo juu kwa sasa, japo misingi yake nayo ilisimikwa na ukoloni.

  Nilishasema mara nyingi kuwa: UOZO wowote katika taifa ni zao la mfumo mbovu wa siasa. Na mfumo wowote ule katika taifa ni lazima utokane na MAZINGIRA na NYAKATI za eneo husika. Demokrasia haina inachosadifu katika mazingira na nyakati zilizopo Afrika...ni mfumo mbovu. Na ndio chanzo kikuu cha uozo wote, na ndio usimikao mirija ya rasilimali zetu kunufaisha mataifa ya nje. Demokrasia.....!!!???

  KWA NAMNA GANI:
  Tatizo letu raia tuliowengi ni kufikiri kuwa demokrasia ni katika siasa na uongozi tu. Ni utoto. Demokrasia ni zaidi ya siasa, ni pamoja na tamaduni, na uchumi.

  Aje? (nitarudi)

  Mungu wetu anaita sasa!
   
 5. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  AFRIKA:
  1. Kisiasa, demokrasia imelenga kulubuni watu kuwa wao ndio wenye dhamana ya kujiamulia mambo yao wenyewe! Kupitia maoni ya wengi ama kura za walio wengi tufanye maamuzi yetu wenyewe!

  Fikiri viwango vya elimu vya tuliowengi, tunapewa haki kupigia kura kitu ambacho hatukijui, sio kuburuzwa huko! Mabunge yetu yana wawakilishi wetu, wao wanapitisha sera tofauti tofauti kwa niaba yetu, kweli shangazi, mjomba, bibi, babu, mama, baba, kaka, na dada zangu kijijini wamemtuma mbunge wetu kuunga mkono aridhi yetu kupewa muwekezaji? Kwanza hata maana ya uwekezaji wanaijua?

  Mbona hatuishi malumbano nao? Huwezi kutoka humo, kwani kanuni na taratibu za demokrasia zinatufunga! Nyamongo ndugu wanakufa, Mtibwa watu wanakufa kwa kukata muwa mmoja tu kupoza kiu, mbugan, majini, watekelezaji ni polisi wetu, wanalinda maslahi ya taifa katika uwekezaji, wewe mwenzangu inakuingia akilini hiyo? Demokrasia imesema, nasi hatuna budi! UBUNIFU HAUJAWAI KUFIKA MWISHO!

  2. Kiuchumi: Hapa ndio target yao kuu ya ulaghai wa hapo juu! Wanaita wenyewe "free economy" -marufuku protectionism ya aina yoyote, na wale tuliowachagua hapo juu ndio wapewao nafasi ya kutusainia yote haya! Watasema tanzania imeridhia, kweli tanzania ni mawaziri tu na raisi wao?

  Nina hakika kama demokrasia mnayodai ni maamuzi ya wengi basi tusingeona upuuzi huu, nina hakika kuwa zaidi ya 90% ya wakulima hawapendi kuona mbogamboga za majani ama nafaka zikiruhusiwa kuingia nchini, wafugaji nao kuona maziwa na nyama zenye chapa za ng'ambo, wenye viwanda nao kuona mitumba, mabati, saruji, nk. hawapendi kuona vitu hvyo kutoka nje, wafanyakazi nao zaidi ya 90% wasingependa kuona ngozi nyeupe maofisi, wataalamu wetu nao hawapend kuona wakandarasi, madaktari, wahadhiri, nk wakipata kazi kwenye nchi zetu, kwani zinawanyima fursa wao wazawa! Sasa hayo maamuzi ya wengi, "demokrasia" yanapatikana wap? Mbona kila kundi linalaumu, lini watanzania tulipitisha hayo?

  Uwekezaji, Ubinafsishaji, soko huria, ni lini waafrika wengi tulipigia kura hayo? UBUNIFU HAUJAWAHI KUFIKA MWISHO, TUKIAMUA TUNAWEZA, nguvuu yetu ni UMOJA na KUTHUBUTU!

  3. Kitamaduni: Hapa ndipo Demokrasia inapohimiza na kutumia akili nguvu nyingi sana kutuzika usingizini! Watu wanapandikizwa usingizi akilini, masikioni na machoni mwao! Chochote utakachoona hakiendi sawa, demokrasia itakwambia UHURU-HAKI, utakaa chini utanung'unika lakin ni bure!

  Watu wanajengewa utamaduni wa kutofanya kazi, kuzoea na kuona ni kawaida unyonyaji-matabaka, wizi, uchafu (usagaji-ushoga), yote hayo demokrasia inasema UHURU! Serikali haina cha kuhoji juu ya mtu anayelala na kuamka baa wala hana mda wa kazi kwake ni starehe tu, serikali haina nguvu ya kuhoji mtu anayemlisha mbwa wake mlo mmoja sawa na bajeti ya familia yenye watu watano jirani yake, eti mali yake HALALI, ni uhalali gani huo, zaidi ya unyama na upunguani? Demokrasia imesema haki! Watu wanaiba tunaaminishwa haki yao, eti ni wajasiriamali-kumbe ni vibaraka vya wazungu, sisi tunakenua meno viwanjani, baa, sinema, bichi, nk. Hivyo ndio dini zetu zinavyotuongoza, ndio mahubiri yetu tunayoyaona kwenye sanaa zetu redioni, jukwaani ama kwenye TV, creating mental slavery, demokrasia inasema haki! Nani anaendelea kuturoga kama si sisi wenyewe?

  Yote hayo yameundiwa katiba yenye maneno mazuri sana "HAKI ZA BINADAMU"

  Mungu wetu anaita!
   
 6. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Nilishakuuliza sehemu na haukunijibu, nauliza tena, Kila ukimaliza post zako mwishoni unasema "Mungu wetu anaita" naomba unijibu katika muktadha wa post hii.
   
 7. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #7
  Jun 22, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Tupa kule hisia zako, imani zako, mitazamo yako, mazoea yako, ujuzi wako, uzoefu wako, hulka zako, mapenzi yako, falsafa na itikadi zako. Simika misingi mipya, au pima ili uliyoitupa katika mizani ya MANTIKI YA UTU.

  Utakuwa umeisikia tayari Sauti ya Mungu aliye hai, ikikuita kuipigania MANTIKI HIYO, kwani MANTIKI ya UTU i nafsini mwa kila mtu, kutoiishi ni sawa na kujisaliti na kujinafiki mwenyewe, ni KUJIKATAA kabla hujakataliwa!

  Sijaiona kwenye dini zetu, siasa zetu, tamaduni zetu, wala uchumi wetu wa sasa, lakini ilipaswa kuwemo humo. Ndio maana unaitwa kuipigania. Pindi itakaposimikwa humo, tutasema "MAISHA NI FURAHA", lakini kwa vile kwa sasa haimo humo, basi "MAISHA NI UPUUZI NA USHENZI MKUBWA, NA KILA KITU CHAKE"

  Mimi na wewe tukiamua tunaweza, nguvu yetu ni UMOJA na KUTHUBUTU.
  Mungu wetu anaita sasa!
   
 8. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  JingalaFalsafa

  Mkuu, ukiishayatupa hayo yote alafu unabakia kama nani?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #9
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Duh! Mbona post inajieleza vya kutosha mkuu? Uwe nani aje?

  Namaanisha kwamba kila unachofikiri ama kutenda, kiwe katika misingi ya UTU. Yaani usifungwe na chochote ila UTU katika maisha yako! Baada ya kuwa hivyo utakuwa unajijua mwenyewe umekuwa nani, ukitaka utajiita padri, shehe, mchungaji, mwanasiasa, mwanaharakati, mwanafalsafa, kiongozi, mtawala, whatever!

  Ni lazima tuumize vichwa, mambo sio rahisi hata kidogo vile tunavyofikiri! Ni lazima tupigane na adui katika ulimwengu wa kiroho na kimwili! Ndio maana nasema "Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani kiroho na kimwili, anaita sasa"
   
 10. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #10
  Jun 23, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Namaanisha kwamba, mtu akiishatupa hisia zake, imani yake, mitazamo yake, mazoea yake, ujuzi wake, uzoefu wake, hulka zake, mapenzi yake, falsafa na itikadi zake alafu anabikia kuwa kama nani?

  Sababu hivi ndio vitu vinavyomtofautisha mtu mmoja na mtu mwingine, na ndio UTU wenye, akiwa hana hivi si atakuwa kama hayawani? Au wewe UTU unamaanisha ni nini?
   
 11. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #11
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Sangarara

  Simika misingi mipya au pima ile uliyoitupa katika mizani ya UTU! Yaani akili na matendo yako yaongozwe na mantiki hiyo ya UTU! Ni kusema kuwa hulka, mapenzi, hisia, uzoefu, ujuzi, falsafa zako, kama zimekosa mizani ya UTU, isikufunge itupe, usiseme nimezoea au nimesomea au ninapenda! TUPA-BWAGA! Simika MANTIKI YA UTU katika falsafa zako, imani zako, itikadi zao, mazoea yako, falsafa zako, hulka zako, mapenzi yako, ujuzi na maarifa yako...hapo ndipo utakuwa umeisikia sauti ya Mungu!

  Nisome upya ndugu tangu tangu mwanzo, utanielewa! Ukishanielewa, usiache tu ukadhani kuna mtu wa kufanya, wewe ndio MUHUSIKA MKUU, sio huyu wala yule!

  Mungu wetu anaita sasa!
  UTU sio tofauti yangu na yako, UTU sio personalties za watu, japo UTU ndio upasao kujenga personality ya mtu! UTU ndio msingi mkuu kabisa maisha ya binadamu, utu ndio alama iwakilishayo uwepo Mungu, utu ni kiwakilishi cha Mungu nafsini mwetu!

  UTU unaweza pimwa kwa utashi wako, lipi jema lipi baya! Hakuna mtu anayeua pasi kujenga hofu nafsini mwake ama kujishuku kwa afanyacho, hata kama sheria imeruhusu "you must feel guilty", ndio UTU huo!

  Mungu wetu anaita!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #12
  Jun 23, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  JingalaFalsafa

  Naomba utumie lugha nyepesi kuelezea hii kitu. Naamini kwamba bado sijaelewa unamaanisha nini. nimesoma post yako yote na nina maswali mengi ya kuuliza na kuna mambo mengi sana najihisi kukubaliana nayo mpaka sasa, hivi vimaswali vyangu vidogo vidogo vikipata majibu vinaweza kuwa ufunguo mkubwa sana wa kuelewa dhana unayotaka kuijenga na itakuwa msaada na kwa wengine wengi watakaopita hapa baadae.

  Kumbuka swali langu la kwanza haujalijibu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #13
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Mkuu sangara:
  Nimeshajibu maswali yote mkuu, ila tu labda ni lugha, japo si kivile sana! Ya kawaida tu!

  1.Naamini uwepo wa Mungu, kama chanzo cha maisha yetu, naamini tuliumbwa nae na kuletwa hapa duniani, yaani chanzo cha mwanadamu ni Mungu!

  2. Naamini pia kuwa, lengo la Mungu kutuwekea maisha(kuishi) ni "FURAHA-KUFURAHIA" tafsiri ya mwanzo kabisa ya maisha, ni FURAHA.

  3. Naamini pia uwepo kwa msingi mkuu wa kusimamia hiyo furaha au maisha. Kwangu hakuna nyingine zaid ya UTU. Hauonekani, ila kwa fikra zenye matendo.

  4. Naamini pia kuwa UTU ni "UWIANO SAWA", yaani MANTIKI. Ndio maana huwa nahoji uhalali wa kupiga hatua ya 2 ya maisha, hali jirani yako hana hata hiyo moja. UTU.

  5. Naamini pia kuwa UTU ndio msingi mkuu wa MANTIKI yoyote ile chini ya jua. Yaani hakuna UTU hakuna MANTIKI, ni upuuzi!

  6. Naamini uwepo wa nyanja kuu tatu (3) za maisha...yaani...
  (a) Siasa. Vile binadumu wanavyoweza kuratibu mambo yao, kwa maendeleo yao!
  (b) Uchumi. Kwangu ni physical and biological factors for human development!
  (c) Tamaduni. Ni mahusiano na fikra zake binadamu juu ya uchumi na siasa!
  Hayo yote matatu yanategemeana, na ni lazima yasimamiwe na kuongozwa na UTU!

  Nitakupa mfano:
  Binadamu alaye chakula mezani! Kitendo cha kuchota chakula kuleta kinywani ni SIASA (anaweza tumia kijiko, mkono, mdomo, mti, upawa,nk), chakula chenyewe ni UCHUMI, aina ya chakula, muda alao, eneo alalo, nk ni UTAMADUNI!

  Kwangu, kama unaamini kwa dhati kabisa thamani ya msingi mkuu wa maisha ni UTU, basi utakuwa umeisikia sauti ya Mungu tayari, kwani humo ndimo anamopatikana tu, hakuna kwingine!

  Ili tafsiri ya maisha ibaki kuwa FURAHA, basi hatuna budi kuulinda msingi huu mkuu-UTU. Ndio maana hatuna budi kuisimika MANTIKI HII YA UTU kwenye nyanja zote 3, uchumi, siasa, na utamaduni. Ni kwa kutumia mantiki hii kuunda mifumo iongozayo nyanja hizo.

  HAPA TUNAWEZA KUHOJI JUU YA MIFUMO IONGOZAYO SIASA, UCHUMI NA TAMADUNI ZETU KWA SASA. Je, UTU humo ndaniye? Kama laa, basi tafsiri ya maisha imebadilika kutoka kuwa FURAHA kwenda HUDHUNI-ni UPUUZI. Hilo sio lengo la Mungu, ndio maana anaita tulipiganie lengo lake!

  (labda kwakuwa sijamaliza kuelezea thread yangu, ndio maana unapata maswali mengi, nashukuru pia kwa kufuatilia)

  Mungu wetu anaita!
   
 14. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  AFRIKA:
  Siasa ndio ya kuratibu namna gani uchumi na utamaduni wetu uwe, kulingana na NYAKATI na MAZINGIRA yetu!

  Demokrasia haina inachofanya katika hili, ndio maana nasema HAIFAI-NI MFUMO MBOVU WA SIASA, na ndio chanzo cha MAOVU!
  1. Haisadifu mazingira yetu, yaani "watu"-Afrika na "sura ya nchi"-Afrika. Demokrasia ni kama imani, haitaki kupokelewa kwenye fikra zetu, haituingii akilini-imekosa MANTIKI kwetu! Poor Political Consciousness on Democracy, sasa kwanini tujilazimishe kuiishi? Ndio maana leo wapo wanaong'ang'ania madaraka, wapo wasioona umuhimu wa kupiga kura hawaendi, wapo wanaoenda tu kwa vile wameambiwa waende, wapo wanaotanguliza ushabiki kama wa usimba na uyanga, mwingine hajala tangu jana amekosa nguvu ya kusimama mstarini hivyo haendi, eti tunachagua kiongozi, hivi tuko makini kiasi gani sisi? Kweli tunakubali kuleta mzaha kwenye masuala nyeti kama haya? Eti tumeambiwa hiyo ndio World Realistic... For how long then? Na ni nani amesema hivyo? Mungu, au shetani? Pumbavu!

  Embu chunguza hata makazi yetu hasi vijijini, yametawanyika mno, mengi hayafikiki kwa urahisi, watu wanabeba kura vichwan mwao (dhamana ya Maendeleo ya watu), hii tunaipa thamani gani dhamana hii? Kwanini tunaichukulia rahisi rahisi tu? Watu wanakufa kwa dhamana hiyo, wanalala njaa, wanaugua, wanateseka,nk. Thamani ipi tunayoipa dhamana yao? HAKUNA! Jibu, Sura ya nchi hairuhusu, aidha milima sana barabara imeshndwa kufika, au mvua nyingi gari imenasa matope haiendi, kutumia ndege ni gharama mno! Hiyo ni dhamana ya watu kwa maendeleo yao, inaletewa mzaha!

  Mfano:
  Ni watanzania wangapi wanaoweza kuhoji chochote juu ya kura yake aliyoipiga? Kwa vigezo vipi anaweza kuhoji? Ni lazima aogope! Kwanza hata utofauti mkubwa kati yake na kiongozi wake! Ye hana hata baiskeli wakati kiongozi amekuja na Vx ama Range! Ataongea nin? "Intimidition" hata mkoloni aliitumimia! Na hiyo ndio Demokrasia, alaaniwe yule apotoshae na kuwajaza watu Usingizi! UBUNIFU HAUJAWAI KUFIKA MWISHO, TUNAWEZA!

  2. NYAKATI: Ni mahusiano yaliopo katika mazingira, yaani baina ya mtu na sura yao ya nchi, pia baina mtu na mtu!
  Demokrasia haina inachosadifu humu!

  Waafrika tumezoea kuona sura yetu ya nchi kama rafiki wa karibu sana, lakini kwa sasa ni adui mkubwa, Demokrasia ndio chanzo! Waafrika wanajuta kuzaliwa kando ya bahari maana kaburu amelubuni anataka ajenge hoteli, yule wa mbugani hatakiwi kuokota hata kuni eti ni kitaru cha mzungu, masikini yule wa aridhi bora mzungu amepewa awekeze kilimo cha umwagiliaji, ole wale juu ya madini "ondokeni ukionesha pua yako tena, ni risasi", wale wa misituni-muwekezaji anavuna mbao hata kuharibu sehemu za kuabudia.

  Tunashurutishwa kuishi choyo na ubinafsi, hakikuwepo mwanzoni! Eti kila mtu ana nafasi yake binafsi ya kufikia hatua ya juu, chuki baina ya mtu na mtu inapandikizwa-upendo unazama, watu wanawindana, hofu na vitisho vinarindima, ni Demokrasia hiyo imesema HAKI. Pumbavu! Mahusiano yetu hayakuwa hivyo, hekima iliyaongoza! Demokrasia haina inachosadifu katika hilo!

  3. UTU:
  Hii ndio nguzo mama. Haijawai kuwepo kwenye neno HAKI-Demokrasia. Demokrasia imekuja kuhalalisha uovu kwa kutumia neno zuri "HAKI-UHALALI"

  Ona utofauti mkubwa uliopo kati ya tajiri na masikini, watu wachache wameshikilia bajeti ya nchi nzima hali tuliowengi tunapiga miayo isiyokwisha, eti UTAJIRI WA HALALI. Kuna uhalali gani wa kumgharamia mbwa hali binadamu anakufa? Unapanga bajeti ya kutanua club za usiku, jirani yako hana pa kulaa........
   
 15. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #15
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  ......kuna uhalali gani wa kumiliki gari kumi hali mwingine hana mavazi? Demokrasia inasema HAKI, UTU je?

  Mtanzania gani aliyepewa haki ya kumiliki hisa kubwa ya rasilimali zetu? Mmakonde na mhaya wanatofauti gani katika utanzaini? Kwanini tunakubali kuburuzwa? Wasomi wetu mnatupeleka wapi? Kwanini tupokee vitu tu bila kuhoji? Pumbavu!

  Ipi ni mantiki nafsini mwetu? Je, ni HAKI ama UTU?

  UTU KWANZA! Maisha ni FURAHA, nayo Furaha ni UPENDO, upendo ni UKWELI, ukweli ni MANTIKI, mantiki ni UTU, utu ni UWIANO SAWA (kufikiriana), uwiano sawa ni FURAHA, ambayo ndio MAISHA yenyewe! Mimi na wewe tumeshindwa kuyashuhudia haya, aidha kwa uzembe wa baba au babu, hata mwanetu hawezi kuishi haya, lakini tukiamua, kizazi chetu kijacho Kinaweza Kuishi tafsiri ya Furaha ya Maisha! Nguvu yetu ni UMOJA na KUTHUBUTU. Na tuanze kuisimika misingi hiyo sasa!

  UBUNIFU HAUJAWAI KUFIKA MWISHO, tujenge nia sasa, kwani uwezo na sababu tunazo! Hakuna kinachoshindikana chini ya jua, hata kwa gharama ya damu, ila mantiki ipiganiwe-UTU! Ni upumbavu kujisumbua kutungua embe bovu, hali ungeweza kutafuta zima!

  MUNGU wetu anaita sasa!
   
 16. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #16
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wakati ukuta, na kila jambo lina muda wake.

  Kwa mtazamo wangu kipindi cha Uhuru barani Afrika hadi mwisho wa muongo uliopita ulimwengu wa kwanza hasa nchi za magharibi zilikuwa zingali na mfumo na itikadi za uchumi wa waati wa kikoloni kutoka katika makoloni yao kuwa ndio source ya raw material. Mazingira ya leo hali imebadilika ghafla kutokana na nchi maskini kufunguka akili na kuona wana haki ya raw material kutosafirishwa nje, bali products. Jambo hilo limezinufaisha sana nchi za Asia, zikifuatiwa South America (Latin America) na sasa bara la Afrika linakuja juu ila kwa kasi ambayo si rahisi kuiona isipokuwa kwa mwenye uzoefu wa kutembea duniani kwa kusoma hali hilivyo na ulinganifu stahiki.

  Nchi za magharibi zimekuwa forced bila kutaka kutokana na nchi wazalishaji katika ulimwengu wa tatu kudai malipo bora na uanzishwaji wa viwanda kwa ajili ya raw material. Kutokana na hali hiyo raw material ni ghali zaidi kusafirisha kwenda huko Ulaya na Marekani, na hivyo kufanya bidhaa zao kuwa ni ghali zaidi kuliko bidhaa zinazozalishwa katika nchi ambazo ni chimbuko la raw material. Mazingira hayo yamefanya wenye nafasi kutoka mataifa ya nchi za magharibi kuelekeza nguvu upande wa nchi maskini kujenga viwanda na vitega uchumi vingine kwa vile uvunaji ni bora zaidi kuliko kuvusha malighafi.

  Pamoja na nchi hizo kuvuna kutoka nchi maskini kwa kuwekeza, ni hatua mojawapo kwa nchi maskini kujijengea uchumi wa uzalishaji kwani kwa njia hiyo wazawa wanapata nafasi ya kufunguka akili nao kufanya kila kinachowezekana na papo wazawa kupata ajira katika nchi zao wenyewe.
   
 17. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #17
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Mkuu Candid Scope:
  Nakupata vizuri, lakini hii ndio hofu yangu.
  . Kuzuia tu malighafi kutosafirishwa nje kutamsaidiaje mwanawaafrika?
  >wanavuna wenyewe malighafi zetu-mashambani, migodini, majini, mbugani, misituni, nk.
  >wanapeleka malighafi hizo kwenye viwanda vyao wenyewe walivyojenga kwenye aridhi yetu sisi.
  >bidhaa kutoka humo zinauzwa kwetu wenyewe tena zile duni kwa bei ghali, hali kuwa zile bora zinasafilishwa ng'ambo.
  *wamekamata njia zetu zote za uzalishaji mali, tunajivunia nini sasa? Tunawaita wawekezaji, ni kweli wamewekeza tangu hatua ya kwanza had ya mwisho!

  ¤Hawa wako radhi kujenga viwanja vikubwa vya ndege tena vya kisasa, sisi tutapongezwa kwa hilo, kumbe lengo lao ni kusafirisha rasilimali zetu "smoothly", aidha kwa kutufunga macho au kuwezesha mandege makubwa kutua na kuondoka!

  ¤Watajenga barabara nzuri za juu na chini, kumbe ni kutupofua ama kurahisisha purukushani zao za kupora rasilimali zetu.
  (si tunaiona Afrika Kusini, mweusi ana nafasi gani kule zaidi ya unyonge?)

  ¤Watajenga majengo marefu na mazuri, ni ya kufanyia mikutano yao ya kuratibu wizi wa rasilimali zetu, pia ni yao kwa ajili ya kuhamia pindi hali ya hewa kwao inapokuwa mbaya, sisi tunawakenulia meno tu, eti "uhuru wa kutembea"
  HIZI HESABU WANANDUGU, ukikwepa kisu unakutana na mshale. Mambo sio rahisi, ni ubunifu na kuumiza akili vile kufikia kupasuka kichwa!

  Tutaendelea kulaumu tawala zetu kila siku, kumbe kwa uvivu wetu wa kutotaka kuumiza vichwa!

  ¤Mbaya zaidi, hata wenzetu wanatusaliti, wanachukua rasilimali zetu kwenda kulimbikiza nje, "dada yangu anakufa juu ya kitanda njiani kwenda hospitali" Pumbavu kila wakihema!

  Yaani hata ikitokea hawataki kutunyonya tutawalazimisha, ni sawa na mwanamke akatizae jela na "kichupi". TUFANYIE NAFSI NA AKILI ZETU MAPINDUZI KWANZA, na hiyo ndio silaha pekee ya kulinda rasilimali zetu, si upuuzi wa kulilia mikataba, ama demokrasia-kitokeacho sasa ndio demokrasia-ukikubali kuolewa............! Tanzania pekee yake, haiwezi.

  NI LAZIMA TUIWEKE WAZI THAMANI YA MTU MWEUSI NA KUISIMAMIA KWA GHARAMA YOYOTE ILE!

  Mungu wetu anaita!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #18
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  AFRIKA:
  Hiyo ni mirija ya namna inavyofanya kazi kuendeza UNYONGE wetu Afrika!

  Naomba kutoa mfano huu:
  "Nimelaza gogo refu la duara kubwa vile mtu anaweza kupita juu lisipotingshwa kutoka sehemu A (ni sehemu duni) hadi sehemu B (ni sehemu yenye ustawi-fanaka). Pembeni ya gogo kuna miba mikali na kila aina ya hatari, msitu mnene, nyoka wakali, simba, nk. Wewe upo sehemu A, mimi nipo sehemu B, lengo lako ufike sehemu B, uwepo wangu mimi sehemu B, unategemea sana kubaki kwako sehemu A.

  Kwa vile wewe unataka kutoka sehemu yenye unyonge A, uje niliko mimi B, hali najua wazi ujio wako nilipo ni unyonge wangu...nakushauri ndugu upite juu ya gogo unifikie nilipo! Nawe unakubali, basi kila ukipiga hatua kadhaa juu ya gogo, nachofanya ni kulitingisha japo kidogo tu, nawe unaanguka kwenye miiba. Nakufariji kidogo, nakupa moyo ukaanze tena mwanzoni kwani ndiko kwenye ngazi za kupandia juu ya gogo. Utarudia na kurudia huku ukiendelea kuchomwa na miiba!

  Lakini mchezo ni ule ule, na hutonifikia ng'oo! Maneno yangu ya faraja kwako eti yanakufanya ujione ulipita kwa pupa ndio maana ukaanguka, au upepo ulitingisha gogo...kumbe nimekufumba macho. HUTANIFIKIA MILELE SEHEMU B, UTABAKI SEHEMU A KIZAZI NA KIZAZI"

  Kwangu, wewe ni "punguani", vile kuaminishwa kuwa huwezi fika sehemu B, ila kwa njia ya gogo tu. Mwerevu hatopita tena juu ya gogo, ila atatafuta njia nyingine pembeni kwenye miiba, labda anaweza kufyka miiba hiyo na kuizoa, ili kupata njia ya kufika sehemu B, hata kama atazidiwa na miiba njiani akafa, mwbnaye ataendelezea msingi wake, na hata mjukuu na kijukuu. Mwishoni kitukuu kinaweza kuona nuru ya sehemu B, lakini fahari itakuwa kwako wewe aridhini, gharama ya upendo wako kwa kizazi chako kijacho!

  UBUNIFU HAUJAWAI KUFIKA MWISHO.

  Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani, Anaita sasa.
   
 19. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #19
  Jul 21, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  AFRIKA:
  Tafsiri yangu kuhusu mfano wa gogo;
  Sehemu A ni Afrika na Unyonge wetu! Na sehemu B ni mabepari na ukuu wao huko Magharibi!

  >Tamanio letu Afrika, ni kuondokana na unyonge wetu unaotokana na njaa, vita, magonjwa, umasikini, utumwa, n.k. Hali kwa mabepari tamanio lao ni sisi kubaki hapa tulipo ili waendelee kujineemesha na rasilimali zetu! USTAWI WA MUAFRIKA NI KIFO CHA MZUNGU.

  >Gogo: Limelazwa na mabepari, wanadai ni njia ya kuondokana na unyonge wetu, wanatushauri, kutuamuru na kutushinikiza kupita, nayo ni Demokrasia!

  >Gogo linatingishwa, tunaanguka njiani, tunaanza na tena:
  Wakikukosa kwenye dini kama Nigeria watakunasa kwenye ukabila kama Burundi na Rwanda, ama ukanda kama Sudan, ama kwenye matokeo ya uchaguzi kama Kenya na Zimbabwe, ama kwenye huduma za jamii kama Tanzania, ama wakupandikizie mamluki kama Kongo, ama wakuvamie kijeshi kama Libya na Ivory Cost, ama wakushike sharubu kama Malawi. Ni kasehemu kadogo tu kanakoleta yote hayo, eti wanadai HAKI, mzungu kawaambia piganieni, ni haki yenu, wanashikiana mapanga! Gogo limetingishwa lazima uanguke, utaangukia kwenye vita, vitakavyosababisha njaa, magonjwa, ukimbizi, n.k sawa na UMASIKINI, watakushauri ujipange upya, utaanza tena Zimbabwe tunaiona! Bado tutabaki kuwa tegemezi, na hakuna asiyejua umuhimu wa utegemezi wetu kwao! Gogo limetingishwa ndugu, lazima uangukie kwenye miiba!

  Kauli ya "vitendo visivyo vya kidemokrasia" hazihishi midomoni, yote ni kuhalalisha mbinu zao chafu, eti wanatetea demokrasia.
  >Namna nyingine ya kutingsha gogo ni hii ya kuwataka watu kuchagua viongozi wao, eti uhuru wa kuchagua. Ndugu zangu waliowengi hawajui hata maana ya neno sera, wala hajui vigezo vya kupima ubora wa sera, lakini demokrasia imewaambia ,wana Haki ya kupiga kura. Unategemea atamchagua nani kama sio yule aliyempa kitenge na kofia? Je bado tuliamini gogo? Kwanini tusitengeneze njia tupite pembeni?

  Ubunifu Haujawai Kufika Mwisho.

  Mungu wetu anaita sasa!
   
 20. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #20
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  AFRIKA:
  Na Haki za Binadamu-hii ndio mbeleko ya Unyonge wetu Afrika, taka tusitake HAKI ni mama wa Ukoloni Mamboleo, ni msingi mkuu wa Utumwa wetu wa Fikra, haki ni silaha ya kukiuka UTU-MANTIKI, HAKI ndio sumu ya Ustawi wetu Afrika! Haki ndio chanzo cha maovu mengi Afrika, Haki ni baba na mama wa UNYONYAJI, Haki ni UPUMBAVU ni UPUUZI MKUBWA! Kama ilivyo kwa maji na moto, ndivyo ilivyo kwa Haki na Mantiki-Utu!

  Tafsiri iliyopo juu ya Haki, ni UHALALI wa ama kufanya au kufanyiwa jambo fulani! Uhalali huu ukazaa neno Uhuru-Huria, ukaingizwa kwenye mifumo ya siasa, ikazaliwa Demokrasia, kwenye Uchumi ikazaliwa private ownership, kwenye Utamaduni ikazaliwa neno "vile nijisikiavyo-nitakavyo" pasi kujali Mantiki ya mambo, yaani UTU, kama msingi mkuu wa maisha! Haki zikaongozwa na HILA, kutokana na asili ya binadamu kuzaliwa na Tamaa ya kujikweza-kutafuta Ukuu "kuabudiwa", ni baada ya kupewa uhuru-uhalali, na neno Haki, HILA - ubinafsi na choyo zikashika hatamu, ikaanza mtu na mtu hadi taifa na taifa!

  KIMANTIKI (ki-UTU), kila kilicho juu kinasehemu kinashikizwa, yaani kuna kitu kinatoa nguvu yake kulinda uwepo wa kile kitu juu! Kama B ipo juu, basi inashikizwa na A au C au yoyote ili isianguke kwa kupenda ama kulazimika! Huo ndio uitwao UNYONYAJI!
  (Hatujadili nani kasema nini juu ya nini, ila vile MANTIKI inavyoweza kutafutwa)

  HAKI ikamuweka binadamu Huru, binadamu huyu huyu anaewaka tamaa, matokeo yake-hisia za watu zinatumika kufanya maamuzi na kuongoza maisha, MANTIKI ya mambo ikatupiliwa mbali, watu wakajifikiria binafsi (HILA ZA HAKI), mtu akawa juu ya mtu, taifa juu ya taifa, vita, mauaji, uhasama, fujo, mateso, unyonge, nk vikashika hatamu! Bado Haki, inasadikishwa kuwa suluisho, hatutafiki milele!

  MANTI-UTU kama msingi mkuu wa Maisha ya binadamu, inapokiukwa kinachobaki Unyama! Nataka niwe juu yako, ni wazi nitakufanyia hila uwe duni! Tanzania inataka kuwa juu lazima tumfanye Kenya au Uganda awe duni, ili sisi tujikweze (tamaa za binadamu), kama walivyofanya Ulaya, wenyewe kwa wenyewe kwanza, mwisho wakawa wamoja dhidi yetu! Wao wameshafika, lakini sisi hatutofika milele, tutapigana kila siku, kupigania ukuu, tutafitiana kila siku kutafuta ukuu-kumbuka ilianza baina yangu na wewe tu sasa ni taifa na taifa, baada ya kupewa uhuru wa tamaa zetu, nasi tukatumia hisia zetu na mioyo yenye hila, tukabariki upumbavu HAKI, tukakiuka Mantiki UTU !

  Mungu wetu yuko hai! Anaita sasa!
   
Loading...