Je, ni sahihi kwa mzazi wa kiume/kike kuingia kwenye chumba cha wanawe wa jinsia tofauti bila kugonga hodi?

Luqman mohamedy

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
892
1,226
Kwenye familia za kizungu mzazi kugonga kwenye room ya wanawe wa jinsia tofauti imekuwa ni utamaduni tofauti na kwenye familia zetu za kiafrika mzazi huingia bila hodi.
Baadhi ya watu wameona ni sahihi na wengine wanapinga swala hili.
Je mzazi ana mamlaka ya kuingia chumbani kwa mwanae bila hodi?
Ni ipi experience yako kama mzazi au kijana uliyepita kwa wazazi??
 
Inategemea na mtoto ana umri gani.
Kama ni mdogo naona haina tatizo , ila akishafikia 10+ hapo mzazi inabidi awe makini anapotaka kwenda chumbani kwa mtoto hasa wa kike.

Japo kila familia Ina taratibu zake.
 
No problem hata binto akiwa na miaka 17 mzazi wa kiume azame tu,kwani tatizo nini! Hata akimkuta binti yuko kama alivyozaliwa,
tatizo wabongo mmeweka uzinzi mbele,wazazi wa kike mnadhani waume zenu wakiingia vyumba vya mabinti zao watawakula.
 
Mh !!

Usigune ndo ukweli.
Wazazi wengi wa kike wamekaa kufikiria uzinzi uzinzi tu kwa waume zao
 
Mi Mzee alikua anagonga chumbani kwangu toka nipo chalii nami nimejengeka hivyo vyumba vya watoto wote wawe wa kiume au wakike lazima nigonge siwezi kuingia bila kugonga...
 
Mimi sina familia lakini siku nikiwa nayo nitakuwa nagonga mlango siwezi ingia kama chooni

Kuna watu wana akili za kuwa wamejenga nyumba wao na hawewezi kugonga ni kuingia tu hiyo sio sawa kabisa . Hata kama ni jinsia moja ni vizuri kugonga hodi sio kuingia tu hovyo hovyo.
 
Exactly kugonga mlango hakuondoi umiliki wa nyumba yako!
 
Back
Top Bottom