Je, ni sahihi kwa mzazi kumlipisha kodi ya nyumba mtoto wake (mtu mzima) anayeishi naye?

alubati

JF-Expert Member
May 29, 2016
2,858
2,000
Waungwana Salaam!

Niende moja kwa moja kwenye hoja, je ni sahihi na halali kwa mzazi anayeishi na watoto wake watu wazima nyumbani na hawasomi kuwalipisha kodi ya nyumba na gharama zingine kama umeme, maji nk?

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu wazima halafu wapo nyumbani kwa wazazi?kabila gani hao?,sasa kama wanalipa kodi wakiwa hapo nyumbani kwanini wasiende kupanga mbali ili vyumba vya nyumbani mzee apangiishe watu wengine ale kodi kwa raha?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
13,502
2,000
Waungwana Salaam!

Niende moja kwa moja kwenye hoja, je ni sahihi na halali kwa mzazi anayeishi na watoto wake watu wazima nyumbani na hawasomi kuwalipisha kodi ya nyumba na gharama zingine kama umeme, maji nk?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni halali.....

Kwa kuwa hao ni watu wazima waliozidi umri wa miaka 18, kwa hiyo mzazi wake hapaswi kuwafanya vijana wa kula na kulala
 

Hamdan

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
350
500
Ni sahihi kwa mzazi anayeishi na watoto wake watu wazima nyumbani na hawasomi kuwalipisha kodi ya nyumba na gharama zingine kama umeme, maji nk.

Kwa sababu si sahihi kwa watoto hao kuwepo hapo, ilhali wanauwezo wa kujitegemea.

Na wala sio uadui.
 

Tukundane

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
10,575
2,000
Ni sahihi kabisa kwa mzazi kumtoza mtoto wake kodi kwa kuwa ni njia ya kumfundisha kuwa amekua na anatakiwa ajitegemee.
 

black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
16,202
2,000
Tena mzee aandike na urithi kuwa ameficha hela nyingi kwenye moja ya kuta za nyumba
Na siku atakapofariki wakiona hiyo Will waanze kuzitafuta hizo hela kwa kuangusha ukuta mmoja mmoja ila wakose wote


Sent from my iPhone using Tapatalk
 

Mokaze

JF-Expert Member
Aug 3, 2018
5,855
2,000
Waungwana Salaam!

Niende moja kwa moja kwenye hoja, je ni sahihi na halali kwa mzazi anayeishi na watoto wake watu wazima nyumbani na hawasomi kuwalipisha kodi ya nyumba na gharama zingine kama umeme, maji nk?

Sent using Jamii Forums mobile app

Hayo ni mambo binafsi ya kifamilia ambayo hayana hukumu maalumu ya kijamii kwani mtu mwingine anaweza kuuliza kinyume cha swali hilo kwamba; je ni sawa kwa mzazi kutomtoza kodi ya chumba mwanaye mtu mzima anayejitegemea???.
 

mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,409
2,000
Nikuulize swali kidogo tu, Je, wanamlipa kwa fedha gani. Za nje au shilingi yetu? ? Kama hawataki kumlipa baba yao anayemlisha mama yao anaye wapikia, basi hayo ni majangili sio watoto. Wampishe baba yao awapangishe wenye uswezo wa kulipa kodi mzee ale na mama yao
 

lordchimkwese

JF-Expert Member
Nov 16, 2015
962
1,000
Hivi mbona wazee wengine hawataki watoto wao wahame nyumbani afu wengine wanakua kama wafukuzwa hivi...

Nahisi ukiona unafukuzwa ujue unazingua kinamna flani..
Mana hapa mshua ananambia nisiende kupanga badala yake hela ya kupanga ninunue tofali nikitoka niende kwangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

jacana

JF-Expert Member
May 24, 2020
204
250
Hii inatokeaga tu kwa wazazi wasio jielewa, umeniza unanitemea Nyumba nitatoa wapi bila kuniwezesha wewe
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom