Je, ni sahihi kwa Mwanamke kupiga picha na rafiki wa mume na kuzitunza katika simu yake?

chawa wa mama

JF-Expert Member
Jun 8, 2020
292
1,083
Naomba msaada wa mawazo wakuu,

Mama Ngina wangu nikiwa niko safari, kukawa na hafla huku nyuma ya jirani yetu. Nimekuta wife kapiga picha akiwa pamoja na rafiki yangu na mwanangu mdogo.

Ni picha zaidi ya kumi, ila ajabu hana hata picha yangu kwenye simu yake. Hapa niko chumbani nazikagua na kawivu kwa mbaaaaali kananitembelea.

Nimuulize, nikae kimya au hata sijui tu
 
Pole kwa mawazo..
Hilo ni kosa kubwa kwa wana ndoa.
Ongea nae kama ana adabu ataomba msamaha na kuwa makini ktk maisha ya ndoa
Ila akipiga chenge kujitetea... basi siyo "MuAminifu kwako"
Tunawatakia amani
 
Mapenzi ni gunia la misumari!Nikiwa mkubwa siyataki
1098765.jpg
 
Kwanini kimya kimya Mkuu? Amuite tu amuulize hizi picha ni aje kupiga picha zote hizi? Nini kinachoendelea kati yenu?
atamjibu ilikuwa sherehe tu alafu anaanza kuishi kwa tahadhari kama kweli ana mahusiano
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Rafiki wa mume wangu ni rafiki yake yeye, na rafiki yangu mimi ni wa kwangu

Mkuu mpaka hapo umeshafeli eti unakuja jf kuuliza eti nimuulize

Subiri usimuulize mpaka ukute wamepiga picha za uchi pamoja sawa
 
Kwanini kimya kimya Mkuu? Amuite tu amuulize hizi picha ni aje kupiga picha zote hizi? Nini kinachoendelea kati yenu?
Sijui kwann ila kama hafanyi ndo atafanya baada ya kumwambia hivyo. Yaani ni kama kuna picha anaitengeneza kichwani kwa mwanamke anaanza kuassume. Nadhani atulie tu, afanye uchunguzi kimya kimya itakuwa rahisi sana kuufahamu ukweli kama anautaka.
 
Rafiki wa mume wangu ni rafiki yake yeye, na rafiki yangu mimi ni wa kwangu

Mkuu mpaka hapo umeshafeli eti unakuja jf kuuliza eti nimuulize

Subiri usimuulize mpaka ukute wamepiga picha za uchi pamoja sawa
Hata asipomuuliza kama mkewe mzinzi ni mzinzi tu, na hakuna mzinzi atakubali kuwa kazini kirahisi rahisi.
 
Back
Top Bottom