Je, ni sahihi kwa CHADEMA kumzika Josephat Isango kwa taratibu za chama?

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,375
Wadau, amani iwe kwenu

Nimeona picha ya Red Brigade wamebeba jeneza lenye mwili wa Mwandishi nguli marehemu Josephat Isango. Binafsi nilikuwa namtambua Isango kama mwandishi na si kamanda wa CHADEMA.

Kutokana na picha hizi zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, najiuliza, je ni sahihi kwa CHADEMA kumzika Mwandishi nguli kama huyo kwa taratibu za kichama? Kama jibu ni ndio, je waandishi wa aina hiyo wataheshimika kwa kazi zao ama ufuasi ndani ya vyama vya siasa? Je kazi yake kama mwandishi wa habari inaaminika kwa kiwango gani?

IMG-20170418-WA0025.jpg
 
Kwani ukiwa kamanda unakatazwa kuwa mwandishi? Mbona Charles Charles yule wa TAZAMA anajulikana kuwa ni gamba kongwe na anawadhifa chamani?
Acha maswali ya kiduanzi
Ulimwengu ni kamanda pia?
 
Kwani ukiwa kamanda unakatazwa kuwa mwandishi? Mbona Charles Charles yule wa TAZAMA anajulikana kuwa ni gamba kongwe na anawadhifa chamani?
Acha maswali ya kiduanzi
Kwa hiyo siku ile alivyopigwa pale Central Police alikuwa kama mwandishi wa habari ama kamanda? Kama ni kamanda, sasa mbona mlikuwa mnasambaza propaganda kuwa Waandishi wa habari wamepigwa?
 
Wadau, amani iwe kwenu

Nimeona picha ya Red Brigade wamebeba jeneza lenye mwili wa Mwandishi nguli marehemu Josephat Isango. Binafsi nilikuwa namtambua Isango kama mwandishi na si kamanda wa CHADEMA.

Kutokana na picha hizi zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, najiuliza, je ni sahihi kwa CHADEMA kumzika Mwandishi nguli kama huyo kwa taratibu za kichama? Kama jibu ni ndio, je waandishi wa aina hiyo wataheshimika kwa kazi zao ama ufuasi ndani ya vyama vya siasa? Je kazi yake kama mwandishi wa habari inaaminika kwa kiwango gani?

View attachment 497931
imeuma
 
Nimekuelewa, ila ndio wanavizia mwanya hata kwenye misiba kupaisha bendera yao. Na labda alikuwa mmoja wa waliokuwa wanapokea bahasha kuwasaidia kuwepo.

Natumaini wataiangalia familia ya Marehemu bila kuwasahau mbeleni.
 
Mkuu Hivi huna Istoria ya Ndg Isango?

Huyu ni Mwanachadema kindaki ndaki na Mwaka 2010 Aligombea Ubunge kwenye Jimbo la Singida Mjini kwa Tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema akishindana na Mo Dewji wa ccm.

Hivyo Usishangae Maziko yake leo Kubebwa na Chama cha Chadema Ndugu Lizabon.
 
Hawa wandishi wa habari ndiyo maana wanaacha kuwajibika kwa mujibu wa taaluma zao na kuanza kuvitumikia vyma ili baadaye viwazike aibu sana. Huyu Isango alijuweka taaluma. Pembeni kabusa na akawa kada wa Chadema
 
Mkuu Hivi huna Istoria ya Ndg Isango?

Huyu ni Mwanachadema kindaki ndaki na Mwaka 2010 Aligombea Ubunge kwenye Jimbo la Singida Mjini kwa Tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema akishindana na Mo Dewji wa ccm.

Hivyo Usishangae Maziko yake leo Kubebwa na Chama cha Chadema Ndugu Lizabon.
Tatizo siyo kugombea, tatizo ni wakati wa kazi mbona huwa hawaweki mambo hadharani kuwa ni wanachadema na kujificha kwenye kivuli cha wandishi wa habari? Waige mfano wa Kubenea kuliko kuwa vuguvugu
 
Wadau, amani iwe kwenu

Nimeona picha ya Red Brigade wamebeba jeneza lenye mwili wa Mwandishi nguli marehemu Josephat Isango. Binafsi nilikuwa namtambua Isango kama mwandishi na si kamanda wa CHADEMA.

Kutokana na picha hizi zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, najiuliza, je ni sahihi kwa CHADEMA kumzika Mwandishi nguli kama huyo kwa taratibu za kichama? Kama jibu ni ndio, je waandishi wa aina hiyo wataheshimika kwa kazi zao ama ufuasi ndani ya vyama vya siasa? Je kazi yake kama mwandishi wa habari inaaminika kwa kiwango gani?

View attachment 497931

Kwa hiyo wewe ulitaka aagwe kwa bendera ya chama chako?!
 
Back
Top Bottom