Je ni sahihi kuwatoa watoto chumba wanacholala na kuwalaza sebuleni au chini kuwapisha wageni?

Kalpana

JF-Expert Member
Jun 16, 2017
26,046
47,578
Kama mada inavyosema hapo juu. Hili suala tumekua nalo katika familia nyingi. Je ni ustaarabu wa kumkirimu mgeni au ni unyanyasaji kwa watoto.
 
Dunia ya sasa imechafuka sana.

Bora hata watoto wawapishe wageni watandike godoro walale sebuleni kuliko kufikiria kuwalaza watoto pamoja na wageni.

Ila kama uwezo unao bora uwatafutie wageni hoteli ya jirani wakalale huko.
 
Ni kweli aisee ila mm nilikua natazama na kwa upande mwingine why wao ndo wasilale sebuleni au chini?
 
Mgeni ni vizuri kuwalaza wageni sebuleni ili wasikae sana kulinda utu wa mtoto.

Ila ni vizuri kujenga nyumba kubwa kwaajili ya kuwa na nafasi ya kutosha kwa ajili wageni.
 
Unamaanisha *Ni* au *Si* vizuri
 
Siyo sawa kabisa. Wageni walale sebuleni na watoto wabaki kwenye chumba chao. Huu ukarimu ndo umekomaa hadi kwenye mambo muhimu ya kitaifa, kama vile kuruhusu wageni kuchukua madini yetu bure halafu wanatuachia mashimo. Haina tofauti na kulala sebuleni na kumpisha mgeni chumbani.
 
ni vyema kuwakirimu wageni lakini sio kulala na watoto...Watoto watafutiwe sehemu nyingine
 
Hili ni janga la kitaifa.
Familia nyingi zinaathirika na hili jambo.
 
Siyo sawa kabisa. Wageni walale sebuleni na watoto wabaki kwenye chumba chao. Huu ukarimu ndo umekomaa hadi kwenye mambo muhimu ya kitaifa, kama vile kuruhusu wageni kuchukua madini yetu bure halafu wanatuachia mashimo. Haina tofauti na kulala sebuleni na kumpisha mgeni chumbani.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom