Je, ni sahihi kutumia vyombo vya habari kupotosha umma?

Aug 19, 2015
27
7
Nachukua nafasi hii kutoa malalamiko yangu kwa wana jamii,
Siku ya leo kampuni ya TanzaniteIne Mining LTD iliyoko Mirerani Mkoani Manyara imeleta wahariri na waandishi wa habari takribani 20 kwa ajili ya kuja kuandika habari zao kuwa hawana matatizo yoyote na wafanyakazi na wanakijiji wanaozunguka mgodi huo.

Ajabu yake ni kwamba ukiwauliza wai wanasema kuwa wahariri hao wameletwa na serikali kuja kuwahoji,ajabu yake hivi serikali inaweza kuwaleta waandishi wa habari na kuhoji upande mmoja na kuacha upande aa pili wenye matatizo na uongozi?

Uzuri ni kwamba wafanyakazi wanajua mwanzo wa hiyo story na mratibu wa hayo mambo yote.Jambo hili limebuniwa na hawa wawekezaji wa kizawa kuwa waite waandishi wa habari waje kuandika huo upuuzi wao ambao ni kwa ajili ya kuzima uovu wote unaoripotiwa na vyombo vya habari kila siku,uzuri wake si kwamba kila mwandishi ana tamaa za hela ndogo ndogo na kudhalilisha utaalamu wake wapo waliokataa kufanya hiyo kazi,

Kizuri ni kwamba wanayo majina ya watu hao na vyombo wanavyotokea ili kuja kuangamiza watanzania wanaodai haki yao.itakapobidi tutaweka hadharani majina ya waandishi jao na vyombo wanavyotoka na kiasi cha pesa walichopewa.kwa hakika nchi hii inaharibiwa na sisi watanzania wenyewe.
Ni juzi tu watu wamefukiwa mgodini wakifanya uchimbaji haramu lakini ajabu yake taarifa zinatolewa na uongozi kuwa wale ni wachimbaji haramu maarufu kama apollo,ukweli ni kwamba wale ni wachimbaji wao wanaoingizwa kinyemela bila serikali kujua ili kupata mali isiyopitia mikononi mwa serikali.Daima njia ya mwongo ni fupi tu.

Leo jumatatu ya tarehe14 marc 2016 wameenda kupewa jinsi ya kudanganya na kesho Jumanne wamepewa offer ya kwenda kutembelea Ngorongoro.kweli mwenye pesa si mwenzako lakini sisi tunasema haki itapatikana tu hata kwa ncha ya upanga.Na hili wanalifanya makusudi ili kuihadaa serkali ya awamu ya tano kuwapa mkataba mpya maana mkataba wao unaishia mwezi wa nne mwaka huu.

Ombi letu tunaomba kama kweli kuna ukweli wa hawa waandishi wa habari kutumwa na serikali tujue na pia iwe wazi kwanini wamekuja kuwahoji wawekezaji tu bila kuwahoji pia waathirika wa kuwepo kwa mgogoro na hiyo kampuni?

Mwisho kabisa nataka kuwapa somo waandishi kuwa jamani chonde chonde "TUMIENI KALAMU YENU VIZURI KWA KAZI YENU"

Aksanteni na kwaherini.
 
ok.habari yako ni mchanganyiko {mixing} wa hoja.

Uzuri umeuliza wewe mwenyewe na kujijibu mwenyewe.... safi sana umetupunguzia tabu ya kukuna vichwa vyetu kutoa majibu ya heading yako.
 
Back
Top Bottom