Lagrange
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 2,256
- 2,572
Wakuu habarini za wakti huu?
Nikiwa nasikiliza mahubiri redioni kama kawaida yangu ,nimeshutushwa na mahubiri ya leo ya Mchungaji Mpachi katika kituo cha redio cha Rock fm hapa Mbeya .
Mtumishi huyu wa Mungu anasema ni sharti unapo chukua mkopo uupeleke madhabahuni ukanenewe maneno ya baraka na kutolewa fungu la kumi:
Mtumishi akaendelea kutoa shuhuda za waumini wake kadhaa walio pata maanguko kutokana na kutopeleka mikopo yao madhabahuni.
Akaendelea kuhubiri kuwa kuna siku alienda kwa mkopeshaji mmoja ,akakuta ana matunguri kwenye droo ,katika hayo matunguri majina ya wakopaji yameandikwa na kiasi walicho kopa .
Mtumishi anadai akambananisha mkopeshaji, mkopeshaji akamwambia kuwa kabla ya kumkopesha mtu wanamchunguza kwanza kwenye ulimwengu wa roho kama anaweza kuwa mteja mzuri au la, Mkopeshaji akamwambia pia Mtumishi ili mtu aweze kurejesha mkopo ni lazima aupeleke madhabahuni ,na mtumishi akaongezea kuwa hupaswi kwenda mbele za Mungu mikono mitupu na ndicho kinacho wakimbiza watu ,akanukuu
" 15 Utaiweka sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu; utakula mikate isiyochachwa muda wa siku saba kama nilivyokuagiza, kwa wakati uliowekwa, mwezi wa Abibu (kwa maana ndio mwezi uliotoka Misri); wala hapana mtu atakayeonekana mbele yangu na mikono mitupu;
Kutoka 23:15"
Wakuu najua hapa jamvuni kuna watu wana uzoefu mkubwa sana kwenye maisha katika nyanja mbalimbali ,karibuni tubadilishane mawazo katika hili.
Karibuni sana tujadili hichi kitu maana nimebaki njia panda Wakuu