Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,769
- 10,645
Wakuu, leo nimeona nilete mada hii kwa mtindo wa swali ili kupata michango mbalimbali. Kwa tamaduni za kiafrika imekuwa desturi kwa mwanamume ama mwanamke kumficha ukweli mwenza wake pale inapotokea amegawa uroda nje ya ndoa.
Je, jambo hili linapaswa kuwa vipi kwa kutazama maadili ya kijamii na ya kidini pia? Ni sahihi, kwa mfano, kufanya toba kwa Mwenyezi Mungu huku ukikataa katakata kumwambia ukweli mwenza wako? Je, kuficha ukweli kuna maana gani linapokuja suala la mtu kujutia kosa hilo na dhamira kumshitaki?
Baadhi ya Michango
==============
=============
============
===========
Je, jambo hili linapaswa kuwa vipi kwa kutazama maadili ya kijamii na ya kidini pia? Ni sahihi, kwa mfano, kufanya toba kwa Mwenyezi Mungu huku ukikataa katakata kumwambia ukweli mwenza wako? Je, kuficha ukweli kuna maana gani linapokuja suala la mtu kujutia kosa hilo na dhamira kumshitaki?
Baadhi ya Michango
Wako wanaoamini katika kuficha ukweli. Hii ni dhambi itakayowaweka wengi motoni. Repentence is not real until you are ready to pay the price. Yaani ile inner conviction izidi hofu ya nje, uwee kusema kweli yote ndipo toba itakuwa sahihi mbele za Mungu.
Mungu hajawahi kuwa msiri wa wanadamu.
Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
==============
Hapo sasa kuna mawili uchague kupoteza kwa Mungu au kwa binadamu.
Kama mtu unahofu ya Mungu na dhamira inakusuta ni wazi kuna siku utajiropokesha tu maana itakutafuna ndani kwa ndani mpaka ukisema,ndo utaskia ka roho kametulia, ila ndo ujiandae kupoteza kwa mwenzako.
=============
Watu wengi hawawezi kusema hasa wabongo ila kwangu nipo tofauti sana, nina uwezo wa kumwambia ukweli na kujutia upande wake. Mama Zakaria sijui kama anaweza kuniambia ngoja nimuulize
============
Hivi nyie dhambi mnayoijua ni kuchepuka tuu? Mbona sijawahi kuwaona mkijipeleka polisi kwenda ku confess mnavyopokea rushwa maofisini, mnavyopiga madili, mnavyodhulumu watu, mnavyoibia wateja/waajiri, mpaka mmetajirika mmejenga majumba, magari makali nk?
Mtu mwenye akili timamu huwez kuconfess maana huyo mke hajakuuliza wala hajahisi chochote we unaenda ku confess ili iweje? Hata akikufuma red hendedi bado unatakiwa ubishe kwamba sio wewe na utafute wa kumsingizia hata shetani au nani sio una confess..!! Kama una roho ndogo ndugu stick to your wife usijiingize kwenye shughuli za michepuko.
===========
Kama unataka ndoa iote magurudumu nenda kaconfess kwa mkeo umecheat, ndio utajua madhara ya corona yapo vipi..
ukicheat nenda katubu piga kimya maisha yaendelee, unaenda kumwambia ujifunze nini?