Je, ni sahihi kumtafuta mtu unayehisi ana mahusiano na mtu wako na kumkanya ?

Spartacus boy

JF-Expert Member
Sep 22, 2020
1,574
3,133
Habari wakuu.

Je, itokee mtu awe na mahusiano unayoyatilia shaka na wako mke/mpenzi na wewe ukamtafuta kumkanya na kumtisha either peaceful or whatever ni sahihi?

Na kabla ya kufanya hayo yote ukamuuliza mpenzi wako akakataa na usiridhike je ukichukua hatua hii ni busara?
 
He he he kwani Nani katoa namba hapo. Mambo mengine jiongeze . Mwanamke kama hamtaki mtu awekagi mazoea hata kidogo , eiza Kuna pesa anakula, kapenda muonekano au anapata furaha Ila hawezi kukuacha na muda mwingine anaweza kua anakula mzigo na wewe au vyote Kwa pamoja. He he he nacheka Ila inauma polee mkuu.
 
Kwanza utampa kiburi mwenza wako maana ataisi umekufa kwake na huna unaweza mfanya ongea na mwenza wako onesha msimamo wako siyo vitisho Ila mwambie vile unaweza kushusha mzigo na kuubeba mwingine najua mapenzi yanauma Ila kumfata mtu anayekuchapia na kumtishia uwoo ni udhaifu mkubwa sana na itakuumiza siku zote na itakuwa fimbo ya kukuchapia Kwa mwenza wako
 
Kama ni mke wa NDOA

Sitamkanya huyo Mtu.. BALI ni kukusanya Ushahidi wa Kutosha.. kwanza

Na kufanya Upembuzi yakinifu.. nikishamaliza kazi hiyo.

Namwita mke.. namuuliza Kulikoni?.. JIBU lake ndio litaamua ADHABU gani ifwate
Mkuu akikataa je na wewe ukawa na ushahidi??
 
Huyo nae alimtongoza kama wewe, sasa kama alikubaliwa kosa liko kwa mpenzi wako huyo ndio wa ku deal nae jamaa hana kosa lolote pengine alimuambia hajaolewa au hana hata mchumba
 
Inategemea na muhusika mkuu mwenyewe.

Ujue kuna maamuzi unayafanya kutokana na tukio husika, na kwa wakati ule husika.

Labda itokee tu mtu akuelezee jinsi tukio lake alivyoweza kucheza nalo.

Kifupi hapo hamna kanuni hata kidogo
 
Back
Top Bottom