Je, ni sahihi kuita uchaguzi huu kuwa ni wa Awamu ya Tano?

Utotole

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,604
4,259
Lipo jambo ambalo linanitatiza hapa na kwa fikra zangu naona haliko sawa. Linaweza kuwa dogo, lisilokuwa na 'impact' yoyote, lakini kama ninavyofikiria ni sahihi ipo haja ya kuweka rekodi hizi sawasawa.

Tunaambiwa, na sisi tunasema uchaguzi huu ni wa kuweka serikali ya awamu ya tano. Swali langu, je, ni kweli serikali ijayo itakuwa ya awamu ya tano? Tukiongelea Rais ni kweli tunatafuta Rais wa Tano!
1. Mwalimu Julius K. Nyerere
2. Alhaji Ali Hassan Mwinyi
3. Mh. Benjamin W. Mkapa
4. Prof.Dr. Jakaya Mrisho Kikwete
5. (huyo ajaye)

Lakini inapokuja kwenye awamu, naamini kila unapofanyika uchaguzi hiyo ni awamu kwa maana ipo nafasi ya kubadlil Rais au hata Serikali kabisa. Hata enzi zile za kura ya Ndiyo/Hapana au picha ya mtu na kivuli, kama tukiuita uchaguzi ilibidi, at least theoretically tuchukulie kwamba ulikuwepo uwezekano wa wapiga kura kumkataa rais aliyependekezwa (japo hakuwa na mpinzani) hivyo kupelekea kupendekezwa mwingine.

Mfano sioni mantiki ya kuchukulia kwamba uongozi wa mkapa kuanzia 1995 hadi 2005 kuwa awamu moja, na wa JK. Kikwete kuanzia 2005 hadi 2015 kuwa awamu moja pia wakati taifa limefanya UCHAGUZI MKUU mara nne (4), yaani 1995, 2000, 2005 na 2010. Ni sahihi zaidi kusema walikuwa marais wawili waliokuwa madarakani kwa awamu nne (kila mmoja akiongoza awamu mbili).

Topic hii nina hakika hairuhusu mtu kujifungamanisha na chama chochote cha siasa wakati wa kuchangia. ni namna ya kupata mawazo yanayoweza kusaidia kuweka rekodi sawa.

Natambua kwamba humu ndani wapo wenye kujua hadi 'chaguzi' zilizofanyika wakati wa miaka zaidi ya 20 ya Mwalimu Nyerere (kama zilifanyika).

Kwa kuzingatia yote hayo, je, awamu hii ya uchaguzi ni ya ngapi?
 
Naona kwa sasa wadau wame-activate 'campaign closure and polling day mode'. Nina imani hayo yakiisha mtarudi hapa tulijadili na hili maana naona ni muhimu kuliweka sawa. At least tupewe maelezo toka kwa wanaofahamu, kwa nini imechukuliwa hivyo.
 
Back
Top Bottom