Je, ni sahihi kuingia maliwatoni na kapero (kofia au barakashe)?

Dr hyperkid

JF-Expert Member
Jun 7, 2019
10,125
19,715
Nawasalimu kwa Jina la Jamuhuri wakuu,

Nisipoteze muda kuna hili swala limetokea pahali kidogo limenishangaza bada ya mzee mmoja kuchachama kwa ukali juu ya tabia ambayo binafsi sijaona kama ni tatizo japo si mumini wa hiyo tabia hapana.

Mzee alikuwa mbogo na kudai kijana hayaheshimu maliwato nikabaki na shangaa. Kumbuka nilikua katika pilikapilika zangu na hapo ilikua katika choo cha public.

Na pengine kuwaza wenda ni umri unamsumbua, lakini nikasema hapana lazima nitake kulifahamu hili kiundani je ni sahihi kuingia chooni na kofia au BARAKASHE iwe kwa haja kubwa au ndogo.

Na kama hapana yapi mavazi ya maliwatoni? Na kwa nini hapana?

Je Kunaushirika wowote wa choo na nguvu za giza?

Au choo kina mihadi yoyote na mapepo? Au choo kina utakatifu gani hadi kuvuliwa kofia?
 
Wazee walituambia tukikojoa kwenye maji ya chemchem yanayo churuzika mama zetu watakatika titi.

Kumbe walisema vile ili watoto waogope na wasiweze kuchafua maji kwakua wanawapenda mama zao.

Kwahiyo fatilia hata hiyo inaweza kuwa ni mbinu tu au siyo ustaarabu wa tamaduni husika.
 
Mkuu hakuna mafindisho yoyote juu ya balaghashia ndani ya uislam ni urembo tu

Liliigwa kutoka kwa Wayahudi kipa
 
Miiko ya wazee wetu ilikuwa na faida na hasara zake, mfano kwetu sisi huwezi msalimia mtu aliyekuzidi umri ukiwa umevalia kofia...Binafsi naona hii ipo sawa
 
Ila watu wanakompliketisha sana maisha.
Hapana, kuna watu wamezidi, kuna jamaa angu huwa anatembea kwa kudunda(usela) na huvaa kofia kila siku . sasa yule jamaa hata umkute anatoka chooni anatembea kwa kudunda na amevaa kofia😂
 
Back
Top Bottom