Je, ni sahihi Baba kuzaa mtoto au watoto na kuondoka na kutelekeza hao watoto asiwatafute tena?

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
8,123
16,423
Wadau nimewaza sana nikajiuliza mno sikupata jibu!!Kuna huu msemo wa kipumbavu sana eti! Baba huwa hatafuti mtoto bali mtoto ndio hutafuta Baba!

Huu msemo ni sahihi?kuna ndugu zangu wamefanya haya na huwa najiuliza wanapataje amani ya nafsi kwa ujinga kama huu?

Baba yangu mdogo alizaa binti mzuri sana anaitwa Halima kule Bunda na mama mmoja wa kiisenye !Badae aliondoka na kurudi kwao dodoma na kumuacha mama na mtoto hadi leo ilikuwa miaka ya 1995!!Hakumfuatilia wala hajui huyo binti alipo!!Binafsi namdharau na kumuona mjinga unawezaje kuiacha damu yako kizembe vile?Leo ameoa na ana watoto karibu watano

Baba yangu mzazi kabla ya mimi kuzaliwa alizaa mtoto kule Iringa mtaa wa uhindini kwa ustaadhi tena shehe tena alizaa na binti wa huyo ustaadhi tena mtoto wa kiume !!!Lakini hadi leo hajui alipo wala hakufuatilia sasa huwa namwangalia namdharau sana

Kuna dada yangu wa mama mwingine kwa sasa ni marehem alizaa watoto wawili huko tanga badae alikuja nao nyumbani baada ya miaka miwili alifariki mi nikiwa masomoni !Badae ndugu wa mume wa marehemu walikuja kuchukua hao watoto kizembe sana! Kumbuka hawakuja hata kwenye mazishi ya mama ya wale watoto wala walikuwa hawatoi matumizi yeyote sasa najiuliza waliwachukuaje watoto wakiwa wadogo vile?

Eti kwanini baba alikubali kwanini wasingelelewa wakawa wakubwa kwanza ndio wakachukuliwa???Hadi leo hawajulikani walipo wakina Shafi Abeid na Omari Abeid nachukia sana!Kumbe inawezekana hata wanangu wanaweza telekezwa kabisa mi nisipokuwepo

Je wadau nauliza ni sahihi ujinga huu??Mbona mimi nilienda hadi kusini kuifuata ile mimba yangu niliompa tukiwa chuoni hadi leo nalea mtoto tena na wadogo zake. Hawa wanaume wenzangu walishindwa nini?

Kuna watu wanatia Hasira sana wakuu
 
Mkuu binadamu tupo tofauti,inamaana hatufanani.kwako unaona ni ujinga kwa mwenzako anaona sawa tu.
Wewe fanya unachoona kipo sawa usimuangalie mwenzako amefanya nini.
 
Kuna mdogo wangu mmoja mtoto wa mama mdogo baba yake alimkataa tangu akiwa mimba hadi anazaliwa hakuwahi kuwa na habari naye. Alivyomaliza form four alienda kufanya kazi mkoa mwingine kawatafuta ndugu zake mapenzi yakawa motomoto sijui hata waliishia wapi maana amerudi tena
 
  • Thanks
Reactions: amu
Aisee Ulimwengu una mambo ya ajabu!Utakuta mzee anatishia laana kwa mtoto ambae hata hajamlea kabisa wamejuana ukubwani tu!!!
 
Ni mambo ya kawaida sana binadamu hatufanani na hatutakaa tuwe sawa hata viongozi mfano Trump, Kinyata, Museveni, Xhi Jiping, JPM hawafanani kuanzia Mtazamo, utu na kila kitu. Ndio maana kuna Malaika na malaika mkuu na kuna malaika mtoa roho....... Dunia inahitaji vichaa, magaidi, wachungaji, majangili, wauaji, masikini wa kila kitu na matajiri wasio na huruma ata punje pia wenye nguvu na ubabe na werevu wasio na mamlaka bila ya kuwasahau masikini jeuri nao wanahitajika kuwepo duniani kusidi maisha yaendelee.
 
Wadau nimewaza sana nikajiuliza mno sikupata jibu!!Kuna huu msemo wa kipumbavu sana eti! Baba huwa hatafuti mtoto bali mtoto ndio hutafuta Baba!

Huu msemo ni sahihi?kuna ndugu zangu wamefanya haya na huwa najiuliza wanapataje amani ya nafsi kwa ujinga kama huu?

Baba yangu mdogo alizaa binti mzuri sana anaitwa Halima kule Bunda na mama mmoja wa kiisenye !Badae aliondoka na kurudi kwao dodoma na kumuacha mama na mtoto hadi leo ilikuwa miaka ya 1995!!Hakumfuatilia wala hajui huyo binti alipo!!Binafsi namdharau na kumuona mjinga unawezaje kuiacha damu yako kizembe vile?Leo ameoa na ana watoto karibu watano

Baba yangu mzazi kabla ya mimi kuzaliwa alizaa mtoto kule Iringa mtaa wa uhindini kwa ustaadhi tena shehe tena alizaa na binti wa huyo ustaadhi tena mtoto wa kiume !!!Lakini hadi leo hajui alipo wala hakufuatilia sasa huwa namwangalia namdharau sana

Kuna dada yangu wa mama mwingine kwa sasa ni marehem alizaa watoto wawili huko tanga badae alikuja nao nyumbani baada ya miaka miwili alifariki mi nikiwa masomoni !Badae ndugu wa mume wa marehemu walikuja kuchukua hao watoto kizembe sana! Kumbuka hawakuja hata kwenye mazishi ya mama ya wale watoto wala walikuwa hawatoi matumizi yeyote sasa najiuliza waliwachukuaje watoto wakiwa wadogo vile?

Eti kwanini baba alikubali kwanini wasingelelewa wakawa wakubwa kwanza ndio wakachukuliwa???Hadi leo hawajulikani walipo wakina Shafi Abeid na Omari Abeid nachukia sana!Kumbe inawezekana hata wanangu wanaweza telekezwa kabisa mi nisipokuwepo

Je wadau nauliza ni sahihi ujinga huu??Mbona mimi nilienda hadi kusini kuifuata ile mimba yangu niliompa tukiwa chuoni hadi leo nalea mtoto tena na wadogo zake. Hawa wanaume wenzangu walishindwa nini?

Kuna watu wanatia Hasira sana wakuu
Baba tafsiri ya kwanza ni aliyemtia mimba mama.

Hayo mambo mengine mbwembwe tu na ziada.lakini tafsiri halisi ya baba yetu ni yule aliyeempa mimba mama yetu.

Kuhusu malezi hata asiyekuwa baba yako akulee vipi hawezi kuwa baba yako kwa sababu hajatia mimba.

Kuhusu baba eti aweze kukuhudumia basi hata mtu asiyekuwa baba yako akuhudumie vipi hawezi kuwa baba yako kwa sababu hajatia mimba.

Hivyo tafsiri halisi ya baba ni yule aliyempa mimba mama.

Kuhusu malezi ni majukumu yake kwa sababu yeye ndo kasababisha uje hapa duniani na mama yako,hivyo anapaswa akuhudumiie.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom