Je, ni Sababu ya Msingi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, ni Sababu ya Msingi?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Dec 8, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,770
  Trophy Points: 280
  Je, ni Sababu ya Msingi?

  [​IMG] Swali:
  Mimi ni mwanaume mwenye miaka 29 nilioa ndoa takatifu kanisani miaka miwili iliyopita na tumekuwa na wakati mgumu sana (migogoro) na mke wangu.
  Ni miezi sita sasa hatujakutana kimwili (tendo la ndoa).

  Naamini tendo la ndoa ni moja ya haki ambayo mume na mke ni muhimu haki kwani ni moja ya sababu zinazofanya tuoe.
  Sioni dalili ya kupata suluhisho kwa migogoro yetu je, naweza kuachana naye (talaka) kwani naamini ninayo sababu ya msingi.

  MAJIBU
  Asante sana kwa swali lako ambalo naamini si wewe peke yako ambaye umejikuta unanyimwa tendo la ndoa kutoka na migogoro kati ya wanandoa.

  Ukweli kujibu swali linalohusu talaka au kuachana ni sawa na kukata kitunguu ganda kwa ganda huku unaugulia kwa machozi hata hivyo nitajitahidi kujibu kama ifuatavyo.

  Jambo la msingi ni kwamba sababu uliyonayo haina msingi na haiwezi kukufanya kutoa talaka kama ndoa yako ni takatifu kama unavyosema.
  Sababu ya msingi ambayo inaweza kukufanya uoe mwanamke mwingine ni pale tu kifo kikitokea na sivinginevyo.

  Pia kukosa tendo la ndoa haina maana ndoa haipo au ndoa inaweza kuvunjika kwani ndoa ni muungano (union) na agano (covenant) wa watu wawili mbele za Mungu waliokubaliana kuishi pamoja hadi kifo kitakapowatenganisha.

  Msingi mkubwa wa ndoa ni kuondoa upweke (loneliness).
  Mungu mwenyewe anatoa jibu kwamba
  ‘‘Si vema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa”.
  (Mwanzo 2:18)

  Ndoa ilianzishwa kwa sababu Adam alikuwa mpweke siyo kwa sababu alikosa tendo la ndoa na hivyo Mungu akaona kwamba “Haikuwa vema”.

  Hivyo companionship ndio msingi wa ndoa na ndoa ni agano la companionship kwa wawili wanaooana.
  Na huu ushirika wa ndoa ni kuwa pamoja katika mawazo, malengo, mipango, jitihada na miili.
  Na msingi wa ndoa ni upendo wa kila mmoja kumpenda mwenzake ili kuondoa upweke.

  (Soma Malaki 2:14, Mithali 2:17)

  Tendo la ndoa halifanyi ndoa bali katika ndoa kuna tendo la ndoa na kutokuwepo kwa tendo la ndoa hakuwezi kusababisha ndoa isiitwe ndoa.

  Ndoa huwepo kabla ya tendo la ndoa.
  Je, wakati unafungua ndoa baada ya kula kiapo mchungaji aliwaruhusu mwende kwanza honeymoon na baada ya kurudi honeymoon ndipo atangaze kwamba ninyi sasa ni mke na mume?
  HAPANA!

  Ninachofahamu ni kwamba baada ya kula kiapo tu, mchungaji alitangaza mbele za mashahidi (KANISA) ninyi ni mume na mke.

  Naungeenda honeymoon kabla ya kwenda kanisani na kutoa kiapo (vow) mbele za Mungu na kanisa (mashahidi) wewe na mchumba wako mngeitwa waasherati maana mmefanya mapenzi (sex) kabla ya kuoana kwa desturi za kiyayudi ungetoa talaka hata hivyo wewe unalalamika kukosa tendo la ndoa ndani ya ndoa kitu ambacho talaka ni impossible.

  Hivyo kukosa tendo la ndoa hakukupi sababu ya msingi ya kuachana au talaka.
  Tendo la ndoa halifanyi ndoa na haliwezi kutenganisha walioana kwani tendo la ndoa ni matokeo ya wanandoa kuishi pamoja na wana wajibu wa kufanya tendo la ndoa ili kuzaa na kuongezekana na hata wasipozaa haina maana ndoa inaweza kutenganishwa.

  Ukiwa honeymoon una enjoy tendo la ndoa kwa kuwa unakuwa umeoa tayari, ni tendo takatifu.
  Hii ina maana hata ukizini baada ya kuoa au kuolewa haiwezi kusababisha ndoa kuwa dissolved isipokuwa kifo.

  Jambo la msingi ni kwamba kwa Mungu hakuna lisilowezekana na ukimwamini Mungu ametoa ahadi kwamba hakuna tatizo katika ndoa lisilo na solution kwani kwake hakuna lisilowezekana au kwa Mungu yote yanawezekana.
  Mathayo 19:26
   
 2. e

  ezekielboaz Member

  #2
  Jan 18, 2010
  Joined: Jan 16, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole sana kaka yangu nimeguswa na tatizo la kunyimwa tendo la ndoa na mkeo.miongoni mwa sababu kuu ya kuoa is to conrol sexual desire,pia miongoni mwa mahitaji ya binadam sex is among.now do the following,1.waeleze wazi wazazi wako na wakike wafanye ufumbuzi 2.onesha mapenzi ya hali ya juu sana (apandaye haba atavuna haba na apandaye kwa wingi atavuna kwa wingi)..3.lipeleke tatizo hili kanisani,waliombee huku wakiendelea kuwapatanisha.4.jaribu kumdadisi ujue chazo cha mwanamke kukutendea ufisadi huo harafu endana na anavyohitaji, ikishikana kwa mawazo yangu hasi wahenga wanasema 'uvumilivu hula mbivu 'elewa mvumlivu hula mbovu na mvumilivu ni msumari binadam anachoka.nadhan kwa kipindi hicho chote ulikuwa na majibu, mungu akuzidishie hekima na maarifa'
   
 3. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #3
  Jan 19, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Suluhisha kwanza migogoro yenu. Tendo hili linahusisha na hisia pia sasa kama mna hisia za chuki atawezajefungua miguu yake?
   
 4. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nionavyo mimi, kunyimwa tendo la ndoa si sababu ya msingi ya kuvunja ndoa, lakini inapokuwa kwa muda wote huo, basi naona hiyo ndoa ilishavunjika zamani sana na anachofanya hapo mume ni kujaribu kuifufua tena ipate uhai kwani ilishakufa. kinachowadanganya kufikiri kuwa bado wana ndoaa ni cheti walichopewa.

  fikiri kuwa kama upweke ndiyo sababu ya ndoa kama walivyoshauriwa, inawezaje wasiwe wapweke kama hawatumii kitanda kwa miezi sita? hapo si tu upweke bali majaribu, makwazo na mengine kama hayo.

  kama wana watoto tayari, basi wamebaki kama partiners katika kulea watoto, basi.

  asijaribu kvunja ndoa kwani technically tayari ilishavunjika! labda kama anataka kuifufua, anaweza kuihangaikia lakini kuiokoa kishachelewa. tuelewane kwanza hapo.
   
 5. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  ndugu yangu mm nimeona hyo hali kwa ndugu yangu mmoja mke wake alikuwa ataki kufanya tendo la ndoa kabisa yani anamwona mme kama kichefuchefu na ilikuwa ni zaidi ya one year baada ya usuluhishi kushindikana jamaa akagiveup but thanx god alikwenda kanisani akaokoka akaenda om kufanyiwa maombi na mke akaombewa yani aibu kumbe mke alikuwa ameolewa na jini na lile jini likawa alimpendi yule mme alisi na lilimfanya yule mke awe na tabia za kiume so walikuwa ni wanaume wawili ndani wakati pepo linatoka likaongea mambo mengi sana
   
Loading...