JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 625
- 938
Imeandikwa na: Jukwaa la Utu wa Mtoto - Children’s Dignity Forum (CDF)
Source: “Sikujua Nilipataje Mimba,” Utafiti Shirikishi kuhusu Mimba za Utotoni na kuwa Mama katika Umri mdogo uliofanywa Wilayani Mpwapwa, Tanzania: (2018)
Mimba za utotoni ni moja ya changamoto kubwa ya kiuchumi na kijamii nchini. Asilimia 27 ya wasichana kati ya umri wa miaka 15-19 wamepata ujauzito. Sababu kuu ya mimba za utotoni ni kipato cha chini cha kaya. Hali hii huwalazimisha wazazi kuwaozesha mabinti chini ya miaka 18 ili kupunguza majukumu ya kuwalea. Pia, husababishwa na matarajio ya familia ya binti kupata mahari inayotolewa na mume au familia ya mume.
Mambo mengine yanayochochea mimba za utotoni ni ukosefu wa miongozi ya wazazi kuhusu malezi ya watoto wao, biashara ya ngono na vishawishi kutoka kwa marafiki. Kuwepo kwa uelewa mdogo na huduma zisizo rafiki za afya ya uzazi kwenye jamii zao na pia vitendo vya ubakaji.
“Changamoto ya kuwa msichana au mwanamke kwenye jamii yetu ni kwamba wasichana hulazimishwa kuolewa katika umri mdogo ili walipiwe mahari ambayo inaweza kutumika kulipa mahari ya kaka yake anapooa. Jirani yangu aliozesha binti yake na mahari aliyopewa ilitumika kulipa mahari ya mke wa kaka yake.” (Sarah 13, Mpwapwa)
“Wavulana wana tabia ya kuwabaka wasichana, ambapo hujificha vichakani wakati wasichana wanapokuwa wanakwenda kutafuta kuni.” (Faith 16, Mpwapwa)