Je!ni ruksa kufanya kilimo cha umwagiliaji pembezoni mwa ziwa victoria??

Si ruksa kufanya kilimo pembezoni mwa chanzo cha maji... Kuna mita kadhaa
 
Kilimo ni moja ya shughuli za kiuchumi kwa wakazi walio wengi nchini Tanzania. Pia kutokana mabadiliko ya uoto wa asili na kuongezeka kwa watu na tekinolojia Dunian imepelekea mabadiliko ya hali ya hewa kwa kuwepo na uhaba wa mvua.

Hivyo kilimo cha umwangiliaji ni mbadala na hauepukiki, isopokuwa una kikomo (not absolute, subject to limitations)

Kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira Na. 20/2004 kifungu cha 57 (1) kinazuia kufanya shughuli za kibinadamu kama kilimo ndani ya mita sitini (60M) kutoka chanzo cha maji kama ziwa.

"57(1) Kwa kuzingatia kifungu cha (2), ndani ya mita sitini hakutafanyika shughuli yoyote ya binadamu ya kudumu au ambayo kwa asili yake inaweza kuhatarisha au kuathiri vibaya ulinzi wa mazingira na, au utunzaji wa bahari au kingo za mto, bwawa, au miambao ya asili ya ziwa.

Hivyo basi, mkuu mbwewe, ni ruksa kufanya shughuli za kilimo cha umwagiliaji nje ya mita 60 na sio ndani ya mita 60 kutoka ukingo wa ziwa (HIGH TIDES).
 
Ahsante sana mkuu, unajua nipo huku kanda ya ziwa sasa kilichonishsngaza ni kutoona mashamba pembezoni mwa ziwa hta zaidi ya hyo mita 60..sasa nikawa najiuliza ina maana wananchi wameshindwa kutumia fursa ya ziwa kufanya kilimo cha umwagiliaji?
 
Back
Top Bottom