Je, ni REAM au RIMS of paper? Nisaidieni tafadhali

Danniair

JF-Expert Member
Feb 18, 2011
360
66
Leo nimekwenda Zanaki Sec School, upande ule wa madarasa enye 'Kombi' ya KLF. kule kuna duka la vifaa vya maofisini. Kilichonishangaza ni tangazo llinalosomeka hivi, 'TANGAZO; RIMS ZA PHOTOCOPY ZINAPATIKANA'. Je, jambo hili linatufundisha nini? Je hakuna walimu makini hata wanafunzi, kwani tangazo lenyewe laonekana ni la siku nyingi. H
 
Ni Rim (bunda moja la karatasi), ukienda stationary na ukaagiza kwa kusema " Naomba RIM moja la karatasi!" hapo ukiwa na maana ya RIM moja yenye karatasi kama mia tano hv.
 
Hapana mkuu, ni REAM of paper, sio RIM of paper. Rim ni ukingo wa kitu kilicho wazi mf. kikombe (rim of a cup) au ndoo (bucket rim).
 
Leo nimekwenda Zanaki Sec School, upande ule wa madarasa enye 'Kombi' ya KLF. kule kuna duka la vifaa vya maofisini. Kilichonishangaza ni tangazo llinalosomeka hivi, 'TANGAZO; RIMS ZA PHOTOCOPY ZINAPATIKANA'. Je, jambo hili linatufundisha nini? Je hakuna walimu makini hata wanafunzi, kwani tangazo lenyewe laonekana ni la siku nyingi. H
Hata mimi nakereka sana na kiingereza kibovu. Umakini umepungua sana. Juzi nimepita mjini nikaona matangazo ya wagombea uongozi wa wanafunzi IFM ,aibu tupu.
 
Leo nimekwenda Zanaki Sec School, upande ule wa madarasa enye 'Kombi' ya KLF. kule kuna duka la vifaa vya maofisini. Kilichonishangaza ni tangazo llinalosomeka hivi, 'TANGAZO; RIMS ZA PHOTOCOPY ZINAPATIKANA'. Je, jambo hili linatufundisha nini? Je hakuna walimu makini hata wanafunzi, kwani tangazo lenyewe laonekana ni la siku nyingi. H
Kama wewe ni msomi basi utajua jibu linakopatikana.
Hivi hata dictionary hamna hapo shuleni?
 
Hapa nina 'a standard english- swahili dictionary' inasema bunda la jumla ya karatasi 480 pamoja inaitwa ream of papers. Pale pale nilamwita KLF student na kumuuliza umeona neno hilo rims? Naye ananiuliza kwani haliandikwi hivyo? Nilimjibu katafute dictionary. Lakini hawa si ndo wake wa marais wetu wa kesho?
 
nadhani hilo tangazo limeandikwa RIMS ZA PHOTOCOPY ZINAPATIKANA KWENYE STATIONARY HII

Kwenye red ni makosa tunayokutana nayo kila siku! me naona sio lazima utumie lugha ya wageni ili uonekane umeelimika
 
stationEry v. stationAry ni janga. Sina hakika kama wa kupewa lawama ni wenye biashara au wenye kuandika haya mabango (sign writers)
 
Mantiki hapa ni kwa nini kosa la lugha linafanyika penye lango la wanafunzi wanao soma lugha hali walimu wao na wao wakiangalia. Ikumbukwe pale ndipo zilipo ngazi za kuelekea madara ya KLF. Na wageni wengi hufika pale kushauriana na wanafunzi wale. Je, sio kuonyesha kuwa uanafunzi wao ni bora miaka iende? Hasa kama hawako makini kuifundisha jamii iachane na makosa madogo madogo kama haya?
 
nadhani hilo tangazo limeandikwa RIMS ZA PHOTOCOPY ZINAPATIKANA KWENYE STATIONARY HII

Kwenye red ni makosa tunayokutana nayo kila siku! me naona sio lazima utumie lugha ya wageni ili uonekane umeelimika

tupe kwa kiswahili basi
 
Usijali, tatizo hata kutamka kasheshe. mf. Management{menejimenti} X
good afternoon {gudyiaftanun}X
Makosa ya sarufi na semantiki
Teacher John,X
Teacher Irene X

Wellcome X
 
Back
Top Bottom