ntinanigwamvuyekule
Senior Member
- Apr 24, 2019
- 130
- 123
Solution is the new Constitution that's ALL.Shida kubwa inayolikumba taifa letu ni kukosa priorities. Shida zetu, matatizo yetu yanafahamika vizuri sana. Mfano, kuna idadi kubwa sana ya watu wanaishi kando kando ya vyanzo vya maji lakini mpaka leo hawana maji safi na salama. Utashangaa kuona wanatumia maji hayohayo wao na mifugo wao. Tatizo lingine ni kuwaamini sana wanasiasa kwamba ndio watatuletea kila hitaji letu la maisha. Tatu ni kuwaza matukio ya kisiasa na kuyapa kipaumbele kuliko maisha yetu ya sasa na yajayo. Mtu anachaguliwa leo baada ya mwaka au miezi anaanza kujupanga kwamba atarudi au hatarudi kwenye uchaguzi ujao. Nne bado tuna viongozi wanaojisahau kuwatumikia watu. Kiongozi anachaguliwa anaacha eneo lake la kiutawala anahamia sehemu nyingine hasa mijini ili kukidhi matakwa yake binafsi. Tano bado wananchi hatuna nguvu za kuwawajibisha viongozi wetu. Mfano kiongozi anapiga kampeni anatoa ahadi kibao. Akishindwa kuzitekeleza hatuna namna ya kumuwajibisha. Sita bado chaguzi zetu zimejaa makandokando. Saba bado sheria zetu ni butu sana. Nane bado elimu yetu haijamuwezesha mtu kuwa critical thinker. Tisa ubinafsi. Unakuta mwananchi ana kipato kizuri tu. Lakini mtaani anapoishi hata barabara anayopita kwenda na kutoka nyumbani kwake haipitiki au hakuna maji. Akishajitengenezea mazingira mazuri yake yeye na familia yake, wwngine muisubiri serikali. Mengine ongezeni.