Je katiba mpya ni hisani ya rais Magufuli au uamuzi wa wananchi?

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,129
2,918
Ndugu zangu wana JF naomba mnisaidie kujibu maswali kadha yanayonisumbua kuhusu katiba mpya.

1-Je katiba mpya ni hisani ya JPM kuamua iendelee au isiendelee?

2-Je JPM kuzuia mchakato wa katiba mpya isiendelee kutekelezwa kama lilivyokuwa limeamua bunge la katiba yupo sahihi kisheria?

3-Je mtu mmoja kuzuia jambo ambalo watu wengi wameridhia lifanyike ni kuwadharau wananchi na kuhisi yeye ni bora na mwenye hekima kuliko watananzia wote.

4-Je JPM anajua kuwa watanzania wametumia muda na pesa nyingi kuhusu mchakato huo?

5-Je mtu asiyeheshimu maamuzi ya mtangulizi wake, wananchi na bunge la katiba tumuiteje au tumueleweje?

Asante naomba tuchangie tusitoleane lugha chafu
 
Mbele ya wabunge wa CCM ambao wamezoea kuitikia kila kisemwacho na mwenyekiti wao, usitarajie wanaweza kutetea hoja yoyote bila kuambiwa na asiye pangiwa.
Zaidi ya yote, Katiba ni yetu wananchi wote na si hisani ya mtu mmoja asiyekatwa P.A.Y.E. Tatizo wa Tz wengi hawataki umoja kwenye kutetea maslahi mapana Yao na kizazi kijacho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Madikteta wote hawawezi kuridhia suala muhimu kama la kuwa na Katiba mpya mahali popote pale..

Hii ni kwasababu ule mkono wa chuma wanaoutumia katika kutawala ( sio kuongoza) utadhibitiwa ndani ya Katiba..

Lazima kuwe na shinikizo kubwa ili kuwezesha kupatikana kwa Katiba mpya. Bila hivyo tusitarajie kabisa kuwa na Katiba Mpya (ya wananchi) Tanzania kwa awamu ya 5.
 
Ndugu zangu wana JF naomba mnisaidie kujibu maswali kadha yanayonisumbua kuhusu katiba mpya.
1-Je katiba mpya ni hisani ya JPM kuamua ufanyike au usifanyike?

2-Je JPM kuzuia mchakato wa katiba mpya isiendelee kutekelezwa kama lilivyokuwa limeamua bunge la katiba yupo sahihi kisheria?

3-Je mtu mmoja kuzuia jambo ambalo watu wengi wameridhia lifanyike ni kuwadharau wananchi na kuhisi yeye ni bora na mwenye hekima kuliko watananzia wote.

4-Je JPM anajua kuwa watanzania wametumia muda na pesa nyingi kuhusu mchakato huo?

5-Je mtu asiyeheshimu maamuzi ya mtangulizi wake, wananchi na bunge la katiba tumuiteje au tumueleweje?

6-Je kama ni mzalendo kwa nini ameshindwa kuheshimu muda na pesa nyingi iliyotumika?

Asante naomba tuchangie tusitoleane lugha chafu
 
Mi nasema kila Wakati WaTz ni wanafki na waswahili. Jambo kubwa kama la katiba kuiachia ukawa na vyama vyake tu ni usaliti wa wananchi kwa ujumla wao.

Bahati mbaya kabisa wale wa CCM na serikali wanaona kiongoza kupitia katiba mbovu ni kukomoa wapinzani wao. Wakati hata watoto wao si wafuasi wao bali wapinzani wao.

Ifikie WaTz wakubali kufia haki yao kwa kuidai ndipo itakapopatikana. Vinginevyo italetwa tena kiinimacho

Cairo's
 
Madikteta wote hawawezi kuridhia suala muhimu kama la kuwa na Katiba mpya mahali popote pale..

Hii ni kwasababu ule mkono wa chuma wanaoutumia katika kutawala ( sio kuongoza) utadhibitiwa ndani ya Katiba..

Lazima kuwe na shinikizo kubwa ili kuwezesha kupatikana kwa Katiba mpya. Bila hivyo tusitarajie kabisa kuwa na Katiba Mpya (ya wananchi) Tanzania kwa awamu ya 5.

Kama kweli ana nia nzuri na mzeledno kwa nini anakataa mchakato mpya wa katiba kuendelea?
 
Nitashukuru kama mtaacha wana JF wajadili kwa maslahi ya taifa maana ni mijadala pekee yake ambayo inayoweza kujenga taifa lenye nguvu na umoja wa kweli.

Hivi maana ya neno uzalendo ni nini? maana nimekuwa nikilisikia kwa kasi kubwa neno hili? Je mtu anayegomea mchakato wa katiba kuendelea ni mzalendo? maana wote tunakumbuka jinsi ilivyotokea pale bunge la katiba lilipokuwa linaendelea na wapinzani kutoka nje na kugomea kuendelea watu waliwaita siyo wazalendo, sasa huyu mzalendo ambaye anatakaa mchakato wa katiba ni mzalendo kivipi?
 
Tatizo liko wazi. viongozi wa kupigania hili wamebaki kupayuka tu na matusi kibao, huku wakionesha umwamba wao mahakamani wanasahau dhamana waliyopewa na wananchi. Cha ajabu wananchi nao hawajitambui, wanashangilia tu utadhani hao wawakilishi wao ndio waliwatuma kufanya hivyo
 
Wapiganie nini wakati mchakato ulishaanzishwa na upo wazi? hivi ni busara kwa kiongozi kama Rais kudharau mawazo ya wananchi kiasi cha kusema katiba mpya siyo agenda yangu?
 
Wapiganie nini wakati mchakato ulishaanzishwa na upo wazi? hivi ni busara kwa kiongozi kama Rais kudharau mawazo ya wananchi kiasi hiki?
Raisi hashikilii mchakato. Mchakato umewekwa kwa mujibu wa sheria. Kubalini tu viongozi wenu wanapuyanga tu hawajitambui, msimsingizie Raisi.
 
Raisi hashikilii mchakato. Mchakato umewekwa kwa mujibu wa sheria. Kubalini tu viongozi wenu wanapuyanga tu hawajitambui, msimsingizie Raisi.

Umewekwa kwa mujibu wa sheria kivipi? kwa hiyo Rais amekiuka hiyo sheria maana alisema katiba mpya siyo agenda yake na hataki izungumziwe wala kuendeleza mchakato wake
 
Umewekwa kwa mujibu wa sheria kivipi? kwa hiyo Rais amekiuka hiyo sheria maana alisema katiba mpya siyo agenda yake na hataki izungumziwe wala kuendeleza mchakato wake
Alosema sio ajenda yake sababu haikuwa kipaumbele kwenye kampeni zake. Raisi hawezi kuzuia mchakato wa Katiba mpya sababu mchakato wake upo kwa mujibu wa sheria
 
Back
Top Bottom