vipik2
JF-Expert Member
- Nov 24, 2011
- 2,803
- 2,185
Pesa ya manunuzi ilitokea mfuko gani?Au ni pesa walionyanganywa watuhumiwa wa kifisadi?
Jibu sahihi unaweza kulipata ukiongea na vijana wa pale HAZINA!
Pesa ya manunuzi ilitokea mfuko gani?Au ni pesa walionyanganywa watuhumiwa wa kifisadi?
Ndio ulimbukeni na ushamba wa matumizi,angekuwa born town asigejulikana hata kama ana Bajaj.Ila madalali wamefaidi sana tu aaaaiiisseee! Yaaani mkuu wa mkoa anamnunulia bmw mkewe zawadi ya birthday!!!! Brand New kabsa wanachana nylon kwenye seat
Katika mambo ni ya ajabu kwenye utawala wa Magufuli ni waliokuwa wabunge wa upinzani kuhamia chama chake kinyemera halafu yeye kama mwenyekiti alikaa kimya kama vile hausiki.Kwenye biashara yoyote usipokuwa makini unaangukia pua na kupata hasara kubwa, lakini si biashara tu tunakosea na kupatia mengi maishani mwetu kuanzia kwenye elimu, siasa, ajira mpaka mahusiano.
Ukikosea binafsi unaweza kujiadhibu ama kujisamehe mwenyewe lakini vipi kama ukikosea kitaasisi? Kwa hakika sheria itachukua mkondo hasa kwa mambo yale yaliyo rasmi.
Kwenye harakati hizi za siasa kama chama cha siasa kisipofuata taratibu na kanuni, mfumo huvurugika na matokeo yake kufanya mambo ambayo hata likitokea kosa ni vigumu kuwajibishana.
Mwaka 2018 ilianza biashara ya siri ya kununua viongozi wa upinzani katika kada mbalimbali, ni wazi lengo lilikuwa kuvuruga na pengine kuusambaratisha upinzani walioasisi mpango huo wakidhani upinzani ni viongozi wakatenga bajeti ya kueleweka kwa ajili ya kutimiza huo mradi.
Bajeti hiyo na mradi huo havikuwa rasmi ndani ya chama na kwa hisia za wengi hilo lilikuwa jambo la wachache na pengine kwa maslahi yao binafsi bila kutafakari ya mbeleni.
Hakuna biashara inayokosa dalali ama mtu wa kati duniani, HAKUNA. Hii ni ajira inayoendesha maisha ya wengi, chochote kikishakuwa biashara ni ngumu kuepuka dalali labda tu iwe ni moja kwa moja kati ya muuzaji na mnunuzi.
Kwenye siasa pia kuna madalali hasa pale siasa inapogeuka biashara, madalali wa kisiasa ndio waliochombeza kwa karibu na kusimamia zoezi zima la biashara ya waunga juhudi.
Leo ile biashara ya siri iko upenuni peupe, badala ya faida mradi umekula hasara kubwa lakini huku madalali wakivimbiwa percent! Kwakuwa haikuwa biashara rasmi na ya wazi hivyo tunawajibishana chini kwa chini na kisirisiri.
Halisi kamwe haiwezi kuongozwa na bandia leo ule wimbo maarufu wa waunga juhudi na tafrija za mapokezi hatuvioni tena na vimeshazikwa kwenye makaburi ya sahau, waunga juhudi wale waliokuwa na tambo za kila aina sasa wamekuwa kama wendawazimu ndio sasa wanajua nini maana ya ile methali ya Waswahel. Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti.
Fundisho hili gumu na muhimu tunalipata katika awamu hii na uwekezaji huu ulioshindwa na kutia hasara kubwa huku mwananchi akikosa huduma muhimu. Sasa ni wakati wa kuadhibu.
Adhabu ya kwanza ni kwa wale waliorubuniwa almaarufu kama waunga juhudi.
Adhabu ya pili ni kwa warubuni, hawa kiama chao ni kwenye sanduku la kura.
OHIO STREETHao wamejiuza mithili ya machangudoa.....
Hivi tangu lini changudoa akapata heshima ndani ya Jamii?
Sure! You are very right mkuuWamarekani wanavyopenda kuingilia cases kama hizi kwenye mataifa mengine, now wanaendelea kukusanya ushahidi tu. Siku utashangaa file linakuwa disclosed na mpaka waliokuwa wanamwagiza na kiasi cha pesa alichokuwa akikabidhiwa kitatajwa.
Hapo ndipo patakapokuwa patamu, kumbe kwa njia nyingine watu wanaichafua madhabahu unapofika muda wa kutubu wanalia haswa dhamira zikiwachoma ila madaraka yanapofusha
SureNdio ulimbukeni na ushamba wa matumizi,angekuwa born town asigejulikana hata kama ana Bajaj.
Imegeuka White elephant project kwa chama ni aibu,ni fedheha kwa chama kikongwe,lakini pesa imetumika.Biashara imefeli na mtaji umeliwa 😂😂😂😂
Madalali wa siasa CCM walikula huku na huku wanakula 10% pande zote kwa mnunuliwa na kwa mnunuziKwenye biashara yoyote usipokuwa makini unaangukia pua na kupata hasara kubwa, lakini si biashara tu tunakosea na kupatia mengi maishani mwetu kuanzia kwenye elimu, siasa, ajira mpaka mahusiano.
Ukikosea binafsi unaweza kujiadhibu ama kujisamehe mwenyewe lakini vipi kama ukikosea kitaasisi? Kwa hakika sheria itachukua mkondo hasa kwa mambo yale yaliyo rasmi.
Kwenye harakati hizi za siasa kama chama cha siasa kisipofuata taratibu na kanuni, mfumo huvurugika na matokeo yake kufanya mambo ambayo hata likitokea kosa ni vigumu kuwajibishana.
Mwaka 2018 ilianza biashara ya siri ya kununua viongozi wa upinzani katika kada mbalimbali, ni wazi lengo lilikuwa kuvuruga na pengine kuusambaratisha upinzani walioasisi mpango huo wakidhani upinzani ni viongozi wakatenga bajeti ya kueleweka kwa ajili ya kutimiza huo mradi.
Bajeti hiyo na mradi huo havikuwa rasmi ndani ya chama na kwa hisia za wengi hilo lilikuwa jambo la wachache na pengine kwa maslahi yao binafsi bila kutafakari ya mbeleni.
Hakuna biashara inayokosa dalali ama mtu wa kati duniani, HAKUNA. Hii ni ajira inayoendesha maisha ya wengi, chochote kikishakuwa biashara ni ngumu kuepuka dalali labda tu iwe ni moja kwa moja kati ya muuzaji na mnunuzi.
Kwenye siasa pia kuna madalali hasa pale siasa inapogeuka biashara, madalali wa kisiasa ndio waliochombeza kwa karibu na kusimamia zoezi zima la biashara ya waunga juhudi.
Leo ile biashara ya siri iko upenuni peupe, badala ya faida mradi umekula hasara kubwa lakini huku madalali wakivimbiwa percent! Kwakuwa haikuwa biashara rasmi na ya wazi hivyo tunawajibishana chini kwa chini na kisirisiri.
Halisi kamwe haiwezi kuongozwa na bandia leo ule wimbo maarufu wa waunga juhudi na tafrija za mapokezi hatuvioni tena na vimeshazikwa kwenye makaburi ya sahau, waunga juhudi wale waliokuwa na tambo za kila aina sasa wamekuwa kama wendawazimu ndio sasa wanajua nini maana ya ile methali ya Waswahel. Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti.
Fundisho hili gumu na muhimu tunalipata katika awamu hii na uwekezaji huu ulioshindwa na kutia hasara kubwa huku mwananchi akikosa huduma muhimu. Sasa ni wakati wa kuadhibu.
Adhabu ya kwanza ni kwa wale waliorubuniwa almaarufu kama waunga juhudi.
Adhabu ya pili ni kwa warubuni, hawa kiama chao ni kwenye sanduku la kura.
Matumizi ya hovyo kwa kutumia pesa zetu yalikuwa mengi mno...kuna siku tukiyajua yote ...tutaweka msiba wa kitaifaMkuu,
Mshana Jr,
Kumbe ndo maana deni la Taifa limekuwa kwa kasi.
Kumbe kulikuwa na biashara ya kununua wapinzaniBashiru na Polepole wanapashwa kulejeaha pesa ili tupungeze nadeni kwa mabebelu.