Uchaguzi 2020 Je, ni nani alikuwa nyuma ya biashara ya waunga juhudi? Je, imemlipa ama kala hasara kubwa?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,793
Kwenye biashara yoyote usipokuwa makini unaangukia pua na kupata hasara kubwa, lakini si biashara tu tunakosea na kupatia mengi maishani mwetu kuanzia kwenye elimu, siasa, ajira mpaka mahusiano.

Ukikosea binafsi unaweza kujiadhibu ama kujisamehe mwenyewe lakini vipi kama ukikosea kitaasisi? Kwa hakika sheria itachukua mkondo hasa kwa mambo yale yaliyo rasmi.

Kwenye harakati hizi za siasa kama chama cha siasa kisipofuata taratibu na kanuni, mfumo huvurugika na matokeo yake kufanya mambo ambayo hata likitokea kosa ni vigumu kuwajibishana.

Mwaka 2018 ilianza biashara ya siri ya kununua viongozi wa upinzani katika kada mbalimbali, ni wazi lengo lilikuwa kuvuruga na pengine kuusambaratisha upinzani walioasisi mpango huo wakidhani upinzani ni viongozi wakatenga bajeti ya kueleweka kwa ajili ya kutimiza huo mradi.

Bajeti hiyo na mradi huo havikuwa rasmi ndani ya chama na kwa hisia za wengi hilo lilikuwa jambo la wachache na pengine kwa maslahi yao binafsi bila kutafakari ya mbeleni.

Hakuna biashara inayokosa dalali ama mtu wa kati duniani, HAKUNA. Hii ni ajira inayoendesha maisha ya wengi, chochote kikishakuwa biashara ni ngumu kuepuka dalali labda tu iwe ni moja kwa moja kati ya muuzaji na mnunuzi.

Kwenye siasa pia kuna madalali hasa pale siasa inapogeuka biashara, madalali wa kisiasa ndio waliochombeza kwa karibu na kusimamia zoezi zima la biashara ya waunga juhudi.

Leo ile biashara ya siri iko upenuni peupe, badala ya faida mradi umekula hasara kubwa lakini huku madalali wakivimbiwa percent! Kwakuwa haikuwa biashara rasmi na ya wazi hivyo tunawajibishana chini kwa chini na kisirisiri.

Halisi kamwe haiwezi kuongozwa na bandia leo ule wimbo maarufu wa waunga juhudi na tafrija za mapokezi hatuvioni tena na vimeshazikwa kwenye makaburi ya sahau, waunga juhudi wale waliokuwa na tambo za kila aina sasa wamekuwa kama wendawazimu ndio sasa wanajua nini maana ya ile methali ya Waswahel. Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti.

Fundisho hili gumu na muhimu tunalipata katika awamu hii na uwekezaji huu ulioshindwa na kutia hasara kubwa huku mwananchi akikosa huduma muhimu. Sasa ni wakati wa kuadhibu.

Adhabu ya kwanza ni kwa wale waliorubuniwa almaarufu kama waunga juhudi.

Adhabu ya pili ni kwa warubuni, hawa kiama chao ni kwenye sanduku la kura.
 
Mungu awasamehe bure waliounga juhudi..malipo ni hapa hapa duniani na adhabu zingine huwa zimo kwenye kitendo ... Hawakujua walitendalo , ila waliowaingiza mkenge walijua bila kujua ya kesho... Ndo hasara ya kufanya biashara pasipo kufikiri kwa kina.
 
Umefika wakati ccm asili kujitambua. Yaani aje mgeni aliyelipwa hela nzuri na hapo ujue wakati yuko kule kila siku alikuwa akiporomosha lugha hatari eti leo ndiye DC na wewe mfia cvhama huna hata baiskeli.
Kuna difusion ilitaka kufanyika chamani..lakini kumbe wenye chama walikuwepo tu wakiangalia mchezo unavyokwenda ..halafu wakaja wakatuma salam kupitia wajumbe
 
Mungu awasamehe bure waliounga juhudi..malipo ni hapa hapa duniani na adhabu zingine huwa zimo kwenye kitendo ... Hawakujua walitendalo , ila waliowaingiza mkenge walijua bila kujua ya kesho... Ndo hasara ya kufanya biashara pasipo kufikiri kwa kina.
Wamesamehewa lakini wameshapata stahilj yao..
 
Hiii biashara iliasisiwa na baba na mwana( Cha zero),mtoto alikuwa anaratibu ununuzi kwa bei kubwa sana,huku akimdanganya baba yake kuwa atasambalatisha upinzani wote nchini. Na kila aliyempinga baba yake hadharani au kwa kificho alitishwa na Kama alikaidi alipotezwa( r.i.p Ben Saanane),kwa sababu mtoto nicha zero akawa anatumia hovyo vyombo vilivyo chini ya ofisi ya baba yake(tiss) kutekeleza utekaji na utesaji,na badae maiti kuokotwa Coco Beach, wakashindwana na Makungu aliyekuwa naibu Mkurugenzi wa tiss,ikabidi Makungu ahamushiwe Tabora kuwa Ras.

Mradi wa waunga juhudi kadri ulivyokolea BASHITE ndo kadri alivyozidi kubadili magari ya kifahari,kelele zikawa nyingi mradi ukarasimishwa rasmi Lumumba( kwa watu wachache)wakaujua wakausimamia,muulizeni baba Levo alifatwa akachomoa,pamoja na mbunge wa kilwa( Bwege).

Bashite akabaki na jukumu moja tu lililoendelea kumfanya awe na bond na baba yake wa kufikia na jukumu hilo ndilo ambalo Pompeo aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa CIA na Sasa waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani aliiambia dunia kuwa Bashite ananyima watu haki ya kuishi ( IN OTHER WORDS BASHITE NI MUUWAJI).
 
Hilo zoezi lilikuwa na baraka zote toka kwa jiwe,cjui kwa yaliyotokea kupitia kwa wajumbe amejifunza nn huyu mwamba kutokea Chato?
Hakuna la kujifunza hapo, Le Mutuz ni rafiki lia lia na mshauli wa Bashite, Halafu Bashite ni rafk lia lia na mshauri wa Chato. Unategemea Kuna kujifunza hapo? Nani wa kumshauri mwenzie kwenye huo utatu haramu? Ukumbuke Musiba aliunganishwa na Bashite kwenye ofisi namba moja
 
Biashara ile ilikuwa ni mradi halali ya mpangaji mkuu bila idhini ya wenye nyumba hivyo ilifanyika kwa siri bila ridhaa na mwisho ikawa ngumu sana kutakatisha faida aliyoipata kutokana na kuwa wenye mali hawakushirikishwa na mradi umekufa kimya kimya ili kwenda na wakati
 
Ila madalali wamefaidi sana tu aaaaiiisseee! Yaaani mkuu wa mkoa anamnunulia bmw mkewe zawadi ya birthday!!!! Brand New kabsa wanachana nylon kwenye seat
Biashara ile ilikuwa ni mradi halali ya mpangaji mkuu bila idhini ya wenye nyumba hivyo ilifanyika kwa siri bila ridhaa na mwisho ikawa ngumu sana kutakatisha faida aliyoipata kutokana na kuwa wenye mali hawakushirikishwa na mradi umekufa kimya kimya ili kwenda na wakati
 
Kwa ccm lengo halikuwa hao watu bali majimbo yao. Unadhani hayo majimbo yaliyokuwa ya hao waunga juhudi yatarudi upinzani kwa asilimia kubwa? Mengi yataenda ccm. Na hapondipo point ilipo. Nawashukuru wajumbe kwa kumkatilia mbali Joshua N. Wa armeru
 
Hao wamejiuza mithili ya machangudoa.....

Hivi tangu lini changudoa akapata heshima ndani ya Jamii?
 
Mkuu Mshana, walijaribu kuuaminisha umma wa watanzania kuwa John anapendwa na kukubalika, wakaiba trillion 1.5 yetu hazina, wakaifisadi!

Viongozi goi goi wa upinzani wakapata fungu, "waunge mkono juhudi" ionekane John anapendwa, wawalaghai watanzania wauchukie na kuukataa upinzani, waliona wamefanikiwa kwa kipindi kile kwa vile waliwapiga pin wapinzani wasifanye siasa yoyote, yani unajisifu una mbio ilihali unayekimbia naye umemfunga kamba miguuni!

Leo hii mchezaji hatari matata kaingia uwanjani, watawala wanaanza kuona rangi halisi ya watanzania! Hakuna aliyekubali ulaghai wa majizi na mafisadi, waliounga mkono juhudi wameenda wao kama wao, wafuasi wamebaki na msimamo wao upinzani, mafuriko ya Lissu yanawatesa watawala walidhani upinzani umekufa.

Zoezi la kununua waunga mkono juhudi limefeli, ni hasara tupu, aibu yao watawala, waunga mkono juhudi na madalali wao
 
Back
Top Bottom