Tunaitaka Tanganyika yetu! Wakati ni huu...

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Wakati tukiwa na Rais Kikwete ambae yeye ndie aliekuwa mpiganiaji wa jambo hili alipokuwa akisota bungeni, kinachohitajiwa ni kusituliwa tu na kuambiwa ule wakati ndio huu.

Tunaitaka Tanganyika.
Tunataka kufuta kasoro za Muungano.
Tunataka Rais wetu.
Tunataka Bendera yetu.
Tunataka Serikali Tatu.

1) Mkataba wa Muungano, 1964, ulitoa sura ya kuwepo kwa shirikisho la serikali tatu ambapo hapangekuwa na serikali moja iliyo na mamlaka makubwa kushinda nyingine.

2) Mkataba wa Muungano ulitaka kuwepo kwa serikali tatu au mamlaka ambazo zingeundwa kiuunganishi ambazo katika waraka huo zilitajwa kuwa ni mmoja wa mamlaka kuwa ni Tanganyika, Zanzibar na Jamhuri ya Muungano.

Hicho kifungu hakikuitaja CCM na wahafidhina wake kuwa ndio wamiliki wa nchi mbili hizi hivyo inatakiwa kutojihusisha kabisa na madai na kujifanya wao ndio walindaji wakubwa kumbe ni mafisadi wakubwa.

3) Serikali ya Muungano unapoilinganisha na kuipima na Zanzibar au Tanganyika ambayo haipo, ni salio la uzawa wa nchi hizo na haiwezi kuwa na mamlaka yake wenyewe, isipokuwa kwa yale mamlaka iliyomegewa. hapa kunaifanya Zanzibar iwepo kama Nchi yenye maamuzi yake na Tanganyika haina.

Sasa ni mfumo wa Vyama vingi na hivyo hivyo ili mambo yaende sambamba kunahitajika serikali nyingi , kwa vile Muungano wetu unashirikisha nchi mbili kunahitajika serikali Tatu , ili kuvutia nchi nyengine nazo ziweze kujiunga, jirani zetu wanataka kujiunga lakini wazo la kupoteza serikali yao ndio kikwazo kikubwa naamini kabisa ikiwa tutaamua kuweka serikali Tatu basi Muungano huu utakuwa na kuzivutia nchi nyingi jirani na hivyo kuweza kupata East African Block.

Hivi tujiulize kama Burundi atataka kujiunga na Muungano wa Tanzania atatakiwa afanye nini ? Na tutazame mfano wa European countries how they manage to get on top of their union na kuifanya fedha yao kuwa juu kuliko dola.

Leo Tunajulikana kama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania japo siku hizi neno Muungano limeondolewa kinyemela nyemela na Chama tawala ambacho kimejitangazia kushika hatamu ,sasa ukiangalia kuna Muungano wa East Africa.

Imewezekanaje kuwepo kwa Muungano huo wakati ndani yake kuna nchi mbili nazo zina Muungano? Ndio nikasema huu Muungano tulio nao sio sahihi kwa hapa tulipo ni lazima kuwepo na Tanganyika ili kuweka sawa mambo ya Muungano kwa eneo zima la East Africa.
 
Jamani Zanzibar ni nchi kamili, ina serikali yake, bunge lake, bendera yake,wimbo wake wa taifa, ina vikosi vyake vya ulinzi na usalama(majeshi), kwa hiyo hii ni nchi kamili.

Swali langu ni kuwa kwanini watanganyika tunakuwa dhaifu kushindwa kurudisha utaifa wetu badala yake tunaona fahari kujiita watanzania wakati kimantiki hakuna nchi inayoitwa Tanzania kwani Zanzibar imeendelea kubaki kuwa Taifa huru na hiki kinachoitwa Muungano ni usanii tu.

Matokeo yake nchi ya kigeni inayoitwa Zanzibar imejipenyeza katika nchi yetu mpaka kuwa na wabunge kwenye nchi yetu tena wanakuwa na guvu kuliko sisi wenye nchi.

Naomba wanasheria wasaidie kuhoji uhalali wa muungano huu feki.
 
Jamani mie nasema, tena nanena kwa uchungu...
Naililia nchi yangu, tena nalia kwa uchungu...
Nchi yangu Tanganyika, ulipotelea wapi...
Nchi yangu Tanganyika, je nikuwekee MATANGA...?

Hivi ulipoteaje, ilhali waliokupoteza - wameshatangulia mbele ya haki...

Nimezaliwa sijakukuta mpendwa wangu Tanganyika...
Nakusikia tu historiani, nikibaki naduwaa...
Hukudumu Tanganyika yangu, kweli hukudumu katu...
Ukapotea tu punde, pale ulipopewa uhuru ule wa kujitawala...
Nakuhitaji Tanganyika, nijivune kujiita Mtanganyika...

Tena nimepoteza utaifa wangu wa kujiita Mtanganyika... Leo hii mie naitwa - eti naitwa mtanzania...
Babu zangu waliokupoteza wengi wameshatoweka... Tumesaliwa na waijukuu, tena tusiokujua vema... Rudi Tanganyika rudi-tujivunie utaifa wetu...

RUDI TANGANYIKA RUDI, RUDI NASEMA TENA RUDI!

Kwanini Tanganyika upotezwe, ilhali mwenzako Zanzibar yupo...
Zanzibar leo yashamiri, Tanganyika twakusomea tu hitma...
RUDI TANGANYIKA RUDI, RUDI NASI TUKUFURAHIE

Muda sasa umefika, nasi kukuona Tanganyika...
Ee Mola tusikie, kuturejeshea Tanganyika yetu tena uliyotutunuku...
Mola wetu hukukosea kutupatia nchi yetu Tanganyika... lakini wanaadam tuna mambo kwa kuipoteza nchi yetu...
Tanganyika yangu njoo, njoo nami nikuone...
Njoo tena kwa uwazi, TUFURAHIE UHURU WETU...

Kwani mkoloni hakuona, kutuwekea mipaka na Zanzibar (lakini leo twang'ang'anizwa, eti shauri ya usalama)...
Rudi Tanganyika rudi, RUDI TUKUFURAHIE.

Wengi watajitokeza, kuubeze utanganyika wangu...
Waila imara nitasalia, kukulilia kwa simanzi...
Nakupenda Tanganyika yangu, na daima nitakupenda...
Na wakubwa wanisikie, juu yako Tanganyika...
Majukwaani twakupindisha, mithili hatukujui...
RUDI Tanganyika RUDI, tufarijike kiuzalendo wetu
 
hiyo tanganyika uliiona wapi?

nini asili ya neno tanganyika?

kwa nini ujivunie jina ulilopewa na wakoloni na kudhararu jina ulilopewa na baba zako?

je huamini kuwa dunia ni moja? au kuwa afrika ni moja?

ukitaka kuvunja muungano wa Tanzania na kurudi kwenye mipaka ya carl peters, na wewe tukuite mzalendo?

jamani, dunia na vyote viitazavyo ni mali ya Bwana, hakuna wazanzibari wala wazanzibara, watanganyika wala watanga na nyika, sote tu mali ya Bwana na alitupaa dunia iwe makazi yetu kuanzia alaska mpaka siberia, cape town mpaka ireland. mipaka yote ni man-made tu.

TUKISHINDWA KUIJENGA TANZANIA, HATA TANGANYIKA ITATUSHINDA
. mark carefully my words

ubarikiwe
 
Ok. there is something wrong with Mr. Lowasa, but there is something behind his political situation. He is not the most corrupt person in this country. There are others, why Lowasa and not Samwel Sitta who sold Loliondo Game reserve to Arabs. I think there is a political trick in the issues behind mr. Lowasa. Please in need your comment.
 
etiiii?
Sita ndo aliuza loliondo?
 
'Nilichukua TAN toka Tanganyika halafu ZAN toka Zanzibar na kuona kuwa nchi nyingi za Kiafrika zinaishia na IA hivo nikaunganisha na kupata TANZANIA'
Huyo ni MDOSI anaejivunia jina lake hilo!!!!!!!!!!
 
hiyo tanganyika uliiona wapi?

nini asili ya neno tanganyika?

kwa nini ujivunie jina ulilopewa na wakoloni na kudhararu jina ulilopewa na baba zako?

je huamini kuwa dunia ni moja? au kuwa afrika ni moja?

ukitaka kuvunja muungano wa Tanzania na kurudi kwenye mipaka ya carl peters, na wewe tukuite mzalendo?

jamani, dunia na vyote viitazavyo ni mali ya Bwana, hakuna wazanzibari wala wazanzibara, watanganyika wala watanga na nyika, sote tu mali ya Bwana na alitupaa dunia iwe makazi yetu kuanzia alaska mpaka siberia, cape town mpaka ireland. mipaka yote ni man-made tu.

TUKISHINDWA KUIJENGA TANZANIA, HATA TANGANYIKA ITATUSHINDA
. mark carefully my words

ubarikiwe
Uzuzu mtupu, yaani hujui Tanzania imetokana ni nini? Labda sio kosa lako ni kosa la waalimu wako.
 
Ni dhahiri shahiri kizazi kinacholitumikia taifa hili kwa kiasi kikubwa leo hii hawaijui Tanganyika, ujumbe uliopo kwenye sred hii ni mzito haswaaa tena wenye machungu kwa watu makini
 
Uzuzu mtupu, yaani hujui Tanzania imetokana ni nini? Labda sio kosa lako ni kosa la waalimu wako.

sasa hna wewe kwa kauli yako hii, unaamini kabisa kuwa umefanikiwa kuficha uzuzu?

hata nivyo nakuombea baraka tele

ubarikiwe sana

Glory to God!
 
kaeni tuu msidai tanganyika yenu.. tutawatuma kinoma.. zanzibar tuko kama 2 mills hivi lakini tunawaburuza watu milioni arubaini...dahhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh. yaani sisi tumepoa soon tunajichimbia mimafuta kimpango wetu than ya kwenu tunakula kama kawaida.. tulieni tuu mtaendelea kutufanyia makazi sisi zanzibar tunakula.. katiba inayokuja inaweka wazi namna gani tunakula vya kwetu na vya kwenu kama kawaida sio.. daeni chnu nyinyi watanganyika haraka kabisa la si hivyo kunatafuta vyote.. zazibar kidogo lakini smart kabisa...huku kwetu hapewi mtu kitu but kwenu tunajibebea tuu ma ardhi hayo... dahhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh amka jirani yangu mtanganyika amkaaaaaaaaaaaaaaa...
 
Tanganyika haiwezi kuja iwapo vyama vyote vikuu vya upinzani havitajiunga na kuwa chama kimoja kikubwa chenye nguvu.
 
hiyo tanganyika uliiona wapi?

nini asili ya neno tanganyika?

kwa nini ujivunie jina ulilopewa na wakoloni na kudhararu jina ulilopewa na baba zako?

je huamini kuwa dunia ni moja? au kuwa afrika ni moja?

ukitaka kuvunja muungano wa Tanzania na kurudi kwenye mipaka ya carl peters, na wewe tukuite mzalendo?

jamani, dunia na vyote viitazavyo ni mali ya Bwana, hakuna wazanzibari wala wazanzibara, watanganyika wala watanga na nyika, sote tu mali ya Bwana na alitupaa dunia iwe makazi yetu kuanzia alaska mpaka siberia, cape town mpaka ireland. mipaka yote ni man-made tu.

TUKISHINDWA KUIJENGA TANZANIA, HATA TANGANYIKA ITATUSHINDA
. mark carefully my words

ubarikiwe

Amen,Kubarikiwa kwafaa kwa wote bila ubaguzi, maoni yangu kwenu nyote ni kwamba, kama muungano unatakiwa kuendelea, basi ni wakati muafaka wa kuutafakari, je i nchi zipi zinazounda muungano, zingatia upand mmoja tu ndo unaonekana kung'ara, Zanzibar, Serikali, bunge n.k kasoro kutambuliwa kimataifa. Upande huu tunauitaje? Hauna bunge wala serikali yake, tunapotaka kujadili mambo yasiyo ya muungano inawezekana kweli kujadili ndani ya bunge la muungano? Tafakari kwanza, vitu vidogo vidogo ndivyo huleta mikwaruzano isiyoisha, amin nakwambia, suluhu ya kweli ya muungano huu ni kutatua kero, hasa zile ndogondogo ambazo wengi kwa kufikiria makubwa makubwa pekee wana zi (overlook).

Raia wa sasa wanauelewa mkubwa wa mambo, wanahitaji majibu ya maswali mengi sana ya muungano ambayo yakikosekana, uaminifu unapotea... Kuhusu Tanganyika kuwa jina la kikoloni hiyo itakusumbua sana, na Zanzibar ni jina gani, Ziwa Victoria, Dar es salaam, Kilimanjaro, olduvai gorge n.k. unatambua kwa majina gani yaliyopewa na babu zako? Haya, je uko makini? kwani Tanganyika ni jina ambalo bado linatumika, Lake Tanganyika ni ziwa pekee ambalo limebaki kuitabulisha Tanganyika. By the way majina siyo issue kwani ukisema Tanzania maanake ni muunganiko wa majina Tanganyika na Zanzibar, sasa kwa nini Zanzibar nalo lisife au Tanganyika lisiwe re-deemed? Wasiwasi wenu ni nini hapa?

Ni LAZIMA (eminent) kwamba mjadala huu uwe chanya, siyo kuhusisha kufikirimioyo (emotions) bila akili kufikiri.... Muhimu ni kwamba mjadala uendelee na muafaka ufikiwe, siyo mwenzio anajadili unamkejeli, huko ni kushindwa kwa hoja, toa hoja yako kwa unyoofu wake iipinge hoja ya mwingine, na namna hiyo tunaenda, si hoja ya kukashfu. Hata ikitokea an independent third party kuangalia credebility ya hoja zenu atavutwa kuwasoma.

I presented.
 
Kuvunja muungano hauwezi kuwa suluhisho la matatizo yetu.

Zaidi sana itachochea ubaguzi; tukisuluhisha matatizo yetu ya kichumi, kijamii, kimaendeleo mvutano kuhusu huu muungano utafutika kwa sababu hakuna mtu atakaye kuwa na lawama juu ya mwenzake.
 
'Nilichukua TAN toka Tanganyika halafu ZAN toka Zanzibar na kuona kuwa nchi nyingi za Kiafrika zinaishia na IA hivo nikaunganisha na kupata TANZANIA'
Huyo ni MDOSI anaejivunia jina lake hilo!!!!!!!!!!

Huyo mdosi anaitwa Mohamed Iqbal Dar
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom