tindikalikali
JF-Expert Member
- Jan 14, 2011
- 4,855
- 1,117
Je kuna mahali sahihi pa kukutana? Nilipata kuonana na dada mmoja njiani, nilisikia jina lake wakati akiitwa na mwenzake, hapo nikapata jinsi ya kumuingia, baada ya story za hapa na pale nilihitaji kumfahamu kwa ufupi, alinambia shule anayosoma,nilimuomba tuwe marafiki nikamuomba namba ya simu> jibu lilikuwa "yaani tumekutana njiani tu.....", nilimuhoji labda ni wapi mahali sahihi pa kukutana? Hakutoa jibu, aliniacha akaenda, bado namkumbuka lakini nitamuona tena jiji hili? Niliondoka na maswali, na bado najiuliza wapi ni mahali sahihi pa kukutana? Kipi cha kuongea unapokutana na mtu kwa mara ya kwanza?