Uchaguzi 2020 Je, ni Mgombea Urais gani kati ya hawa anahitajika sana kwa sasa na Wananchi wa nchi ya Malawi ya Kaskazini?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,542
108,858
Je,....

1. Mgombea ambaye Sera zake ni Miundombinu, Usafirishaji, Utalii na Madini huku Vitisho / Mikwara vikitawala Ubongo wake 24/7?
2. Mgombea ambaye Sera zake ni Kuanza Kwanza kupambania Maisha Magumu ya wana Malawi ya Kaskazini na Haki zao Kiujumla?
3. Mgombea ambaye Sera zake ni Kushirikisha sana Wataalam katika Maeneo husika, Maendeleo na Utu wa Kisiasa na Amani?

GENTAMYCINE nikiwa kama Raia wa hapa nchini Malawi ya Kaskazini nina uhakika Majibu yenu ya hapa yatatupa Mshindi halali wa Uchaguzi huo.
 
Wa miundombinu alishasema kauli zifuatazo.

1. Nilisukumiziwa uRais
2. Hii kazi ni ngumu, nalala hadi na mafaili.
3. Mniombee maana kuna watu.

Ni vizuri akafanye kazi ambazo siyo ngumu, iliyo ngumu awaachie watakaoiweza.

Nimeropoka kwa kurudia alichoropoka kwenye ma-camera na mic.
 
Sera zake ni Kuanza Kwanza kupambania Maisha Magumu ya wana Malawi ya Kaskazini na Haki zao Kiujumla?
Fafanua hiyo vizuri kuonyesha ni jinsi gani serikali inaweza kupambania maisha magumu ya watu. Contract ya serikali na raia ni kwamba, raia watalipa kodi, halafu serikali itajenga miundo mbinu yote ambayo haiwezi kujengwa na watu binafsi ili kusurdi raia waitumie miundombinu hiyo kujipatia vipato vya kuendesha maisha yao.

Je, una maana kuwa serikali iwe inagawa hela kwa wanachi ili kurahisisha maisha yao au vipi? Uwepo wa hela za mkatomkato mitaani ni kati ya mambo yaliyoiruidisha nyuma sana nchi yetu na kusababisha upungufu wa ubunifu.
 
Mi nashangaa nyie Chadema tu ndo mnaona JPM siyo visionary leader. acheni kupotosha watu. Nchi bila miundo mbinu utafanyaje?? Ina maana hamjui maana ya trickle down effect of economy?? It doesn't come overnight. JPM could put down the blue print and economic design and future leaders would implement huko baadae.

Nchi ipo sisi ndio tunapita so kunaweza kusiwe na quick effect kwenye uchumi wa mtu mmoja mmoja ndani ya miaka hii kumi lakini infrastructures will be there for over 100 years so acheni kudanganya watanzania kwamba hii miundo mbinu haina maana.

Acheni ubinafsi wakujiwaza nyie kwamba ndani ta miaka huu kumi maisha yameenda kombo basi na labda una miaka 50 so you are concluding JPM hafai. Ukiona matunda wanayokula USA leo ni maono waliyokuwa nayo viongozi wao wa miaka karibia 250 iliyopita.
 
Mi nashangaa nyie Chadema tu ndo mnaona JPM siyo visionary leader. acheni kupotosha watu. Nchi bila miundo mbinu utafanyaje?? Ina maana hamjui maana ya trickle down effect of economy?? It doesn't come overnight. JPM could put down the blue print and economic design and future leaders would implement huko baadae...
Watu wenye akili wanatumia akili zao saa 24 kuwaza kukuza uchumi ili ulete maendeleo ya watu ndipo yachochee maendeleo ya vitu!
 
Mi nashangaa nyie Chadema tu ndo mnaona JPM siyo visionary leader. acheni kupotosha watu. Nchi bila miundo mbinu utafanyaje?? Ina maana hamjui maana ya trickle down effect of economy?...
Unapotosha au mahaba yamezidi,Kwan huwezi jenga miundombinu na Maisha ya watu yakaendelea kama kawaida, ni sawa na mtu analaza tatoto wake njaa,wanavaa malapulapu,wanaacha shule kisa unataka kununua gari na kujenga nyumba mazee hutaeleweka
 
Unapotosha au mahaba yamezidi,Kwan huwezi jenga miundombinu na Maisha ya watu yakaendelea kama kawaida, ni sawa na mtu analaza tatoto wake njaa,wanavaa malapulapu,wanaacha shule kisa unataka kununua gari na kujenga nyumba mazee hutaeleweka
Na ukiwaendekeza sana watoto watakuwa hawajishughulishi na wanasubiria tu mali ya urithi
 
Back
Top Bottom