ERoni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2013
- 43,528
- 89,643
Hello wana MMU!
Kuna mambo huwa yananitatiza, hasa katika maisha yetu ya kila siku. Binadamu lazima tuishi kwa kutegemeana, hakuna binadamu anayeweza kusema kuwa "mimi peke yangu naweza kuishi bila msaada wa ndugu/jirani/rafiki au mpita njia"
Lakini katika kuishi kwetu kwa kitegemeana, ni muhimu/lazima kujua mipaka yetu, wapi uwe karibu na mtu, wapi ujiweke pembeni, wapi unahitajika na wapi huhitajiki.
Mzee Nyerere alijitahidi sana katika ujamaa, aliamini katika ujamaa na alituaminisha(hasa sisi tuliokuwepo nyakati zake) kuwa ujamaa ndio suluhisho la maendeleo, hatuwezi kufika bila huo mfumo, sijui aliwaiga kina nani, China au Urusi? hata sijui. Lakini mfumo huu kwa maoni yangu ni mbovu na umeleta upuuzi mwingi sana kwa baadhi yetu.
Mifano midogo;
»Mtu amekuja mtaani ni mgeni, kila mtu atataka ajue ni nani, anatoka wapi.
»Mtaani kila mtu atataka ajue unaishi maisha gani, unafanya kazi gani, unatoka saa ngapi na kurudi saa ngapi
»Ukifanikiwa kidogo tu, kwa kitu kidogo ambacho hakina hata mantiki basi mtaani watu wataanza kukusema na vibaraza ili mradi tu siku ipite.
»Wanawake kukaa vibarazani toka asubuhi hadi jioni, kuongea mambo yasoyiwahusu.
Hiyo ni mifano michache tu.
Sasa najiuliza, ni mifumo ya JKN ndio inatufanya tusiwe watu wa ku-mind our business ila biznes za jirani zinakuwa zetu?
Je, nyie wenzangu mnaonaje hiyo tabia?